Kiapo cha Baba Mkwe; Upendo wa Baba Kwa Binti Yake; Moja ya sharti atakalompa Mkwe wake(atakayeoa binti yake)

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
KIAPO CHA BABA MKWE; UPENDO WA BABA KWA BINTI YAKE, MOJA YA SHARTI ATAKALOMPA MKWE WAKE(ATAKAYEOA BINTI YAKE).

Anaandika, Robert Heriel

Hakuna atakayebisha kuwa Baba yeyote anaupendo mwingi Kwa mabinti zake.

Halikadhalika, mabinti wengi huwapenda Baba zao zaidi kuliko Mama zao.

Wakati kina Mama wakitupenda Vijana wao zaidi kuliko. Pia Sisi Vijana tunapenda Mama zetu zaidi kuliko tunavyopenda Baba zetu.

Taikon nasemaga ni ngumu Sana Kwa Kijana wa kiume kuwa Win, kuwa-Master wanawake Kama hapendani na Mama yake. Au yupo mbali na Mama yake. Yaani ana-distance na Mama yake.

Kijana, kitendo cha kumuweka Mama yako mzazi mbali ni kuwaweka wanawake mbali kwenye mizania ya kuwaelewa.

Ili umuelewe Mkeo lazima umuelewe Mama yako Mzazi au Mwanamke aliyekulea tangu ukiwa mdogo. Kama haumuelewi mama Yako huwezi muelewa mwanamke yeyote Yule katika hii Dunia. Na ili umuelewe Mama yako mzazi itakupasa utumie zaidi akili kuliko Hisia zako. Maisha anayoishi mama Yako na Baba yako kuna uwezekano wa 90% ndivyo Wewe utakavyoishi na Mkeo.

Maneno ambayo uliambiwa na Mama yako kuhusu Baba yako kuna uwezekano 90% ndiyo watakayoambiwa watoto wako na Mkeo.

Michezo yote ya mama Yako uliyokuwa unaiona ukiwa mdogo wakati Baba hayupo au mama kumzunguka Baba yako ndivyo hivyohivyo Mkeo atakayoifanya.

Mpende mama Yako hata kama utagundua anatabia mbaya mbaya Fulani hivi Kwa sababu kupitia tabia hizo zitakusaidia kuwajua Wanawake.

Vile mama Yako alivyokuwa anawachukulia mawifi zake, kuna uwezekano Asilimia 90% Mkeo akawa na mawazo hayohayo Kwa Dada zako.

Kumbuka, Wamama wako very-technic wafanyapo mambo Yao Kwa watoto wao.
Wamama wengi hulenga zaidi kuzigusa hisia za watoto wao kuliko Akili za watoto wao.
Ilhali wababa wengi hulenga kugusa Akili za watoto wao kuliko Akili zao. Sasa unaanza kunielewa.

Binti, ili umuelewe mume wako itakupasa umuelewe Baba yako. Huwezi muelewa Mumeo kama hukumuelewa Baba yako. Utabaki kumlaumu na kumuona hakufai lakini kimsingi Wewe ndio humfai Kwa sababu umeshindwa kumuelewa.

Wanawake wengi Kama sio wote waliokaribu na Baba zao huishi Kwa Raha mustarehe katika ndoa zao. Ni ngumu Sana Kwa binti anayepatana na kupendana na Baba yake ndoa imshinde. Hiyo ni ngumu kabisa.
Unaweza kuchunguza hata kwenye familia yenu. Mabinti waliopatana na kupendana na Baba zao wengi wao ndoa haziwasumbui. Na wanawaheshimu Waume zao.

Hii ni tofauti na Wanawake wanaopendana na Mama zao zaidi kuliko na Baba zao. Hawa wengi huwa washindani wa waume zao. Wengi wao ndoa zinawashinda na mara Kwa mara huwa na ugomvi na waume zao. Unaweza kuchunguza mwenyewe.

Hii inatuambia kuwa kuishi na kulelewa na Baba na Mama ni muhimu Kwa sababu inasaidia watoto kujua tabia za wanawake na wanaume tangu wakiwa wadogo.

Ni ukweli usiopingika kuwa Wababa wengi tunauchungu na mabinti zetu. Tunawapenda na tunatamani waishi maisha MAZURI.

Wababa tunatamani mabinti zetu watakapoolewa wawe Wake Bora, Mama Bora na ndio maana Sisi kina Baba tunakuwa wakali tunapolea mabinti zetu kuliko Vijana wetu.

Tunaumia Sana mabinti zetu wanapotuangusha Kwa kuwa na tabia mbaya na kupata madhara Kama mimba au kuzalia NYUMBANI.

Wanaume wote Duniani tunafanana katika Hilo. Tunachukia Sana kuona mabinti wakituangusha na hii ni Kwa sababu tunawapenda Sana binti zetu. Wanasema ukipenda Sana basi utachukia Sana.

Hata hivyo tunapenda mabinti zetu waolewe na wanaume kamili wanaojielewa. Wanaume kweli sio wanaume kama mabinti.

Waolewe na Vijana wenye akili, hekima, ucha Mungu na uchapakazi Kwa bidii na maarifa.
Lakini pia Vijana wenye tabia njema na kuweza kujizuia na tamaa ya Mwili.

Embu tupitie kisa hiki; zingatia Aya zilizokolezwa hasa ya 50

Mwanzo 31:43 “Labani akajibu, akamwambia Yakobo, Hao binti ni binti zangu, na wana ni wanangu, na wanyama ni wanyama wangu, na yote uyaonayo ni yangu; nami naweza kuwatendea nini leo binti zangu na wana wao waliowalea

44 Haya! Na tufanye agano, mimi na wewe, liwe kwa ushahidi kati ya mimi na wewe.

45 Yakobo akatwaa jiwe akalisimamisha kama nguzo.

50 Ukiwatesa binti zangu, na ukitwaa wake zaidi ya binti zangu, wala hapana mtu pamoja nasi, tazama, Mungu ni shahidi kati ya mimi na wewe?

44 HAYA! NA TUFANYE AGANO, MIMI NA WEWE, liwe kwa ushahidi kati ya mimi na wewe.

45 Yakobo akatwaa jiwe akalisimamisha kama nguzo.”

Hicho ni kisa cha Labani na Yakobo mkwewe.
Yakobo kaoa mabinti wawili wa Labani.
Labani Kwa kuwa anawapenda mabinti zake anaona mahari pekee yake haitoshi kumuamini Yakobo mkwewe, anaona wafanye Agano na Kula kiapo Kati yake Labani na Yakobo mkwewe Kwa manufaa ya Mabinti zake.
Huo ni Upendo mkubwa Sana WA Baba Kwa Binti zake.

Moja ya masharti ya Labani ambayo anayataka kutoka Kwa Yakobo mkwewe ni haya;

1. Usitese mabinti zangu
2. Usitwae au kuongeza mke/wake wengine zaidi ya mabinti zangu.

Huyo ndio Baba. Na ndivyo Wababa wengi walivyo Kwa mabinti zao.
Kinaitwa kiapo cha Baba Mkwe na Mkwewe kwa upendo wake Kwa mabinti zake.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mabinti mnaowapa mimba nao wana baba zao mnaowaumiza, kama umewahi mfanyia binti wa watu ivo...aisee ile laana upatilizwa kizazi hadi kizazi la sivyo sali sana kuvunja huo mnyororo
 
Mabinti mnaowapa mimba nao wana baba zao mnaowaumiza, kama umewahi mfanyia binti wa watu ivo...aisee ile laana upatilizwa kizazi hadi kizazi la sivyo sali sana kuvunja huo mnyororo

Karma haizuiwi na maombi.

Utasamehewa lakini lazima ulipwe haki yako.

Hata Daudi aliomba na kusali Sana alipoiba mke wa mtumishi wake lakini haikusaidia Jambo lolote.

Tuelewe kuwa kabla ya kufanya Jambo lazima tujue matokeo yake. Kwa maana mara nyingi maisha hayatusamehi ingawaje Mungu anatusamehe.

Yaani Maisha yameshasetiwa kabisa kuwa ukipanda mahindi lazima uvune mahindi
 
Karma haizuiwi na maombi.

Utasamehewa lakini lazima ulipwe haki yako.

Hata Daudi aliomba na kusali Sana alipoiba mke wa mtumishi wake lakini haikusaidia Jambo lolote.

Tuelewe kuwa kabla ya kufanya Jambo lazima tujue matokeo yake. Kwa maana mara nyingi maisha hayatusamehi ingawaje Mungu anatusamehe.

Yaani Maisha yameshasetiwa kabisa kuwa ukipanda mahindi lazima uvune mahindi
Hakika
 
Back
Top Bottom