Baba mkwe, mahari hii imenishinda

Tukio la mahari linaudhi sana kwetu sisi vijana tunajipanga eti demu kaniambia mahari yake milioni moja na nusu cash, demu mwenyewe form four failure na anajifunza cherehani anajiproud eti yy beauty na bikra nikapiga chini
 
Nakumbuka Mwaka huu Rafki yangu alifanywa hivyo ukweni akasusa na kuondoka ila walikuja kumletea binti baada ya Jamaa kukaaa kimya miezi miwili na hawakumdai tena pesa waliokuwa wanataka aongezee
 
Yaan umenikumbusha braza wangu mmoja hiv mtoto wa dingi mkubwa, alienda kupangiwa Mahari wakataka Milioni 3 jamaaa akawa nayo milioni 1. Wakakomaa weee, mshenga kajaribu kuwapangua lkn mashangazi wamekaza hawaelewi kitu. Basi wakamuita bwana harusi mtarajiwa atoe suluhisho kama ataongeza, broo alipoenda akasema kua ana milioni moja tu, hana pesa ya kuongeza hata hivo kajitahidi sana, ila kama hawataki hiyo milioni basi yupo tayari kumuacha binti yao aolewe na mwingine jmaa akaishia hapo. Kumbe binti alikua ndani anasikia akaanza kuangua kilio wakimbembeleza ndo anazidisha sauti. Ilibaki kua aibu tu.
Waliporudi Jamaaa alikaa kimya ikapita miezi 3 hapaeleweki binti anasumbua anataka kuolewa, anashinda kwa broo kila siku ili asije kurafuta mke mwingine wakakubali tu Hiyohiyo milioni moja.
 
Kuna baadhi ya wazazi wa binti wanakaza mpka umalize ndo umchukue binti yao
Mnakomplicate bure,mahali kupangwa haimaanishi utoe yote. Unatoa uliyonayo afu unaendelea kuzaa watoto. Mbona watu wanapenda kulalamikia mahali?! Mnataka bure?
 
Yaani hapo ndo nawakubali ndugu zetu waisilamu binti ndo anapanga ko mnajadili kabisa kwamba usipange kubwa. Akikuelewa utakuata kakupangia laki au laki 2 au kutokana na mapato yako
 
Aiseeeee,hao ndio Wanaume wa sasa ndio maana wakishaoa wanagongewa wake zao. Safi sana Mkuu kwa kumpa makavu huyu mbuzi Kifutu
 
Ndugu, ukiwa na msimamo thabiti wala hutopelekeshwa. Kongole kwa braza mkubwa.
 
Walikuwa wanakuuzia kabisa kabisa,aaah hiyo ni hatari sana
 
Familia inayozingatia uislamu.
Hapo safi vijana wa kiislamu kama hajaoa atakuwa anamatatizo yake binafsi au binti hajapenda kuolewa na wewe.
 
watupe
 
Mafala sana hao wapozee mkuu,hiyo 280k bora ungeenda kufunga bar tu na masela na papuchi za kununua siku ikaisha,acha wamwoe wenyewe yani mahari M5 duuu anatoa tanzanite nini kwenye papuchi!!
 
For sure ni changamoto usikubali upuuzi wao wabaki na binti yao. ila wewe na bado umeshamjaza mimba hatari ila weka mbali na watoto.
 
Familia inayozingatia uislamu.
Hapo safi vijana wa kiislamu kama hajaoa atakuwa anamatatizo yake binafsi au binti hajapenda kuolewa na wewe.
Wagalatia mahari kwao wanafanya kukomoa. Harusi ndo balaaa. Takbiiir
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…