Baba mkwe, kuwadi wa mke wangu

Baba mkwe, kuwadi wa mke wangu

Majigo

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
5,519
Reaction score
1,831
Kabla Sijadondokea Kiini cha tatizo, niwape mkasa mfupi Ili muweze kunielewa.Naimani ushauri wenu utaniongoza vyema.

Ni Binti ambaye sasa ni Mke Wangu.Nilisumbuka kidogo kumpata kwani nilipomuaproch alidai ana Mtu wake na anampenda sana hivyo niachane naye, kwakweli kwa mda wote sikuwahi kumuona huyo mtu wake hiyo ikazidi kunipa udadisi juu yake.''Kwa nini anikatae?''.Nikajipa kazi ya kiintelejensia, kumjua Mpinzani wangu.Nikagundua ni kweli ana Jamaa ila yuko Ughaibuni.

Angalau hii ikanipa matumaini na kurudisha kasi ya kuendeleza mashambulizi . Maneno Matamu hayakukauka Kichwani mwangu.Lengo ni kumshawishi Binti akubali ombi langu

Binti aliendelea na msimamo wake na safari hii alikuwa mkali kidogo,kuona hivyo nikaibuka na ombi la Urafiki wa kawaida. Alinielewa na nikafanya kila mbinu ili kumfanya ajisikie fahari kuwa nami.Ingawa sikuwa na Hela kivile,lakini ''izawadi ndogondogo''. Nilihakikisha havikomi kwake.

Maisha yakaendelea na tukawa tunaelewana sana.mida mingine anakuja gheto anapika na tunakula pamoja,kwa mtu wa nje angezani ni wapenzi kumbe lah!kwani mda mwingi tuliutumia tukiwa pamoja

Kuna siku mida ya jioni alikuja gheto akionekana kutokuwa sawa, nilijaribu kuuliza tatizo nini alidai yuko sawa nikajaribu kumdodosa akasisitiza nimuache na anaomba alale.

*******
Maisha yakasonga, Akili bado ilisumbuliwa na huyu binti, huku mara kwa mara nikiendelea kumkumbusha na kuonesha hisia za wazi kwake lakini sikufanikiwa

Nikaanza kuhisi tabia zake zikibadirika polepole mfano akaanza kuonesha kutofurahishwa, Anaponisaka Hewani usiku wa wanane na kukuta niko bize, basi atalalamika.
ooh! Majigo unajua siku hizi sikuelewi! unaongea na nani?

Hasa akiniona nimesimama na jinsia ya kike utamuona anavyokuwa mkali! hii kitu haikuwa kawaida yake. Kabla ilikuwa akiniuliza na kunitania kuwa tunapendezana na msichana huyo na angependa kupata wifi ka yule!! nilimjibu ''sina girl hivyo aache hayo maswali''

Kama Ilivyoada Siku nyingine tukiwa gheto, tunacheki Seres ya kifilipino huku tukitupia Popcon, Kuna kipengele katika ile seres kilihusu mapenzi tukajikuta tumeingia katika mjadala wa mahusiano.

Majigo unajua mpaka sasa sikuelewi, vipi umeshapata mwenzi?''aliuliza binti wakati huu kanigeukia na tunatazamana ana kwa ana''

''Hapana!''nilimjibu huku nami nikimtazama kwa jicho la nakutamani ujue''

''Unangoja nini?''aliendelea kuuliza binti wakati huo akiwa kaegemeza mikono yake mabegani mwangu

******

Siku hiyo tukajikuta tumefanya mchezo husiofaa kwa watoto wadogo basi ikawa zetu, tunajifungia Ndani na kumaliza yote humo

Maisha yalikuwa matamu sana hata kimasomo nilikuwa vizuri kwani hapo kabla ufaulu wangu haukuwa mzuri mi na mtoto mzuri kila kona ya mji, yeye mimi mimi yeye namna tulivyokuwa tunapeana mahaba, wakatupachika jina la ''njiwa'

Mambo yanabadirika baada ya jioni moja niko nae gheto huku tukiendelea kutomasana na kucheza michezo kama Wafanyavyo paka wadogo!...binti Akanipa taarifa iliyonistua sana alidai ana mimba yangu.

lilinipa wakati mgumu ukizingatia bado nlikuwa nasoma na mzazi wangu ni mtata sana endapo atasikia habari hizi itakuwaje.

Nililikabili Kiume kwani sikujutia kwa namna yoyote tena nikamwambia sitaki kusikia habari za kuitoa hiyo mimba nitafanya juhudi zote ili kusolv mambo.

******

sikumjulisha mtu.. Ila nilishangaa siku kuitwa na kuwekwa kikaangoni na mzee akintuhumu kumpachika mimba binti wa watu, na kusahau kilichonipeleka shule....akawa mbogo na kudai kuanzia siku hiyo hatotoa hela yake kwa masuala yangu ikiwamo ada!.

Sikuamini kama hii mzee angetoa maamuzi ya namna hiyo, ukizingatia tulikuwa karibu kufanya mitihani ya kuhitimu Chuo.. hivyo ningehitaji sana mchango wake kama mzazi

Nilijaribu kuwashirikisha watu mbalimbali ikiwamo mama ili kumshawishi mzee...lakini Haikusaidia

wakati huo tayari kitumbo cha binti kinaendelea kuchanua, kutokana na mgogoro na mzee, hata chuo nikasimama nikaanza kufanya vibarua ili kuweza kujijenga kimaisha kwani nilishajua naenda kuwa baba mda si mrefu

siku moja binti alikuja gheto akiwa analia ...Nilishajua kimenuka kwao kwani amekuwa akiniambia wazazi wake walianza kumuhisi tofauti Hivyo nikamuuliza nini kinaelendea...akaniambia ''wazazi wanataka kumjua muhusika wa ujauzito ule'' nikamwambia awape ukweli wala hasihofu kuhusu hilo

basi basi siku ya siku nikapata ugeni ,nilifaham kinachoendelea kwani wazazi waliongozana na bint...akili yangu ilishavurugika hivyo nikawa tayari kwa lolote.


Ni mkasa unaoniumiza sana hivyo naomba nitulize akili kwa mda itaendelea Wakuu.

Asanteni JIgo.
 
Na iendelee iishe isije ikwa kama Isidingo the need
 
Kabla Sijadondokea Kiini Cha Tatizo, Niwape Mkasa Mfupi Ili Muweze Kunielewa...Naimani Ushauri Wenu Utaniongoza Vyema

Ni Binti ambaye Sasa Ni Mke Wangu..Nilisumbuka Kidogo Kumpata Kwani Nilipomuaproch Alidai Ana Mtu Wake Na Anampenda Sana Hivyo Niachane Naye, Kwakweli Kwa Mda Wote Sikuwahi Kumuona Huyo Mtu Wake Hiyo Ikazidi Kunipa Udadisi Juu Yake..''Kwa Nini Anikatae?''..... Nikajipa Kazi Ya Kiintelejensia, Kumjua Mpinzani Wangu..Nkagundua Ni Kweli Ana Jamaa Ila Yuko Ughaibuni!

Angalau Hii Ikanipa Matumaini Na Kurudisha Kasi Ya Kuendeleza Mashambulizi !.. Maneno Matam Hayakukauka Kichwani Mwangu..Lengo Ni Kumshawishi Binti Akubali Ombi Langu

Binti Aliendelea Na Msimamo Wake Na Safari Hii Alikuwa Mkali Kidogo...Kuona Hivyo Nikaibuka Na Ombi La Urafiki Wa Kawaida, Alinielewa Na Nikafanya Kila Mbinu Ili Kumfanya Ajisikie Fahar Kuwa Nami!..Ingawa Sikuwa Na Hela Kivile.... Lakin ''Vijizawadi Vidogovidogo'' Nilihakikisha Hazikomi Kwake

Maisha Yakaendelea Na Tukawa tunaelewana sana..mida Mingine anakuja gheto anapika Na tunakula pamoja!..kwa mtu wa nje angezani ni wapenzi... kumbe lah!.....Kwani mda mwingi tuliutumia tukiwa pamoja

Kuna siku mida ya jioni alikuja gheto akionekana kutokuwa sawa, nilijaribu kuuliza tatizo nini!...alidai yuko sawa...nkajaribu kumdodosa ...akasisitiza nimuache na anaomba alale.....

Ni mkasa unaoniumiza sana hivyo naomba nitulize akili kwa mda.....Itaendelea Wakuu!

AHSANTE JIGO

dogo umeoa lini ??

Hii sio haki kabisa.

Kwangu anabana. Eti mpaka ndoa.


Kumbe kuna boya linakula wakati mimi nawekewa vimulimuli.

Yaani unaweza ukaua mtu hivihivi na usijutie Lolote.
Hapa hujaoa

Nlishazoea Tabia yake Ya Kuchunguza Simu Yangu Na Kuwatusi Wanaonipigia Hasa Kama Ni Sauti Ya Kike Ndo Kabisaaa....Atatukana Matusi Yote Unayoyajua

Kama Kawaida Wikend Hii Alinibana Sana Nitoke Nae , Nikaona Hisiwe Tabu..Nkaruka Nae Kiwanja Changu Cha Kila Siku..Joto Ni Pale Alipokuja Muhudumu Anayenihudumia Kila Nikiwa Hapo

Kwakwel Huyu Dada Nina Mazoea Nae Sana Nashindwa Kuelewa Siku Hiyo Aliingiwa Na Nini Si Ndo Akaja Akaniita ''Dear''.....Wee! Palizuka Vagi Ambalo Sijapata Kuliona Maishani

Nashukuru Walinzi Waliwahi Na Kumtoa Nje Waifu, Bahati Mbaya Dada Wa Watu Aliumizwa Baada Ya Kupigwa Na Kiti....Hivyo Bado Natuliza Hii Kesi Kwani Alishaipeleka Polisi

Ntawataarifu Kinachoendelea Wakuu!

Ahsante Jigo

hapa mkeo anataka kuua watoto kisa wivu
Lazima mkubali kuwa mimi ni mteja kwenu na ninyi ni watoa huduma kwangu, hivyo baada ya malipo yote... nina haki ya kutumia nyumba yako vile nitakavyo ilimrad sisababishi uharibifu wa mali zako.

Godoro ni langu na hela za kuigharamia mahusianio ni zangu, sasa kwanini unanibania mimi mteja wako nisiye na mke, kutotumia kitanda changu kujistarehesha?

Wakati wala siibughudhi familia yako na wapangaji wengine kwa namna yoyote ile, naomba msininyanyapaae nami ni mteja na nina haki kama wengine!!

mwenye nyumba analalamika kisa hujaoa
toka DAR,
Salam kwenu wakuu
Ni kwamba hivi karibuni natarajia kuanza masomo ktk chuo flan hapa mjini....

mbali na Ada, nina Shiling LAKI 8 hivi kama mtaji wa biashara,

sasa wakuu naomba mnishauri kitu/biashara gani naweza fanya ambayo haitanibana ukizingatia sina kazi na nategemea kuizungusha hii hela ili niweze kuendesha maisha nikiwa chuo bila kuathiri masomo yangu
MDA CHUONI NI MASAA MATANO ,TUNAINGIA SAA 6 MCHANA KUTOKA SAA 11 JIONI
NB:Tafadhari!! Kama huna ushauri kuwa msomaji tu!!!

AHSANTEN!!
ushauri endelea na masomo kuliko kutuumiza vichwa ili tukushauri uongo
 
nimeedit Hiyo Mnaweza Endelea Na Mkasa Ulionisibu
 
dogo umeoa lini ??


Hapa hujaoa



hapa mkeo anataka kuua watoto kisa wivu


mwenye nyumba analalamika kisa hujaoa

ushauri endelea na masomo kuliko kutuumiza vichwa ili tukushauri uongo

achana Na Mimi Wewe!...we unazani utasoma maisha yote?...unaweza ukasoma na ukawa ndani ya ndoa
Malizia mkasa ndo ujue kisa cha mimi kukatiza masomo
 
dogo umeoa lini ??


Hapa hujaoa



hapa mkeo anataka kuua watoto kisa wivu


mwenye nyumba analalamika kisa hujaoa

ushauri endelea na masomo kuliko kutuumiza vichwa ili tukushauri uongo

!
!
ukisikia unoko ndio huu. Sasa mkuu kumkonalia mwenzio kiasi hiki kisa nini? yeh teh teh teh I wish ningekuwa natumia pc ningekupa like ila haka ka tecno hakanaga hayo.
 
achana Na Mimi Wewe!...we unazani utasoma maisha yote?...unaweza ukasoma na ukawa ndani ya ndoa
Malizia mkasa ndo ujue kisa cha mimi kukatiza masomo

umeoa lini ??
 
!
!
ukisikia unoko ndio huu. Sasa mkuu kumkonalia mwenzio kiasi hiki kisa nini? yeh teh teh teh I wish ningekuwa natumia pc ningekupa like ila haka ka tecno hakanaga hayo.

chief Threesixteen Himself ....achana na MO11 .....hajui kuna kuwa shule, kupanga na kukutana na masaibu ya baba mkwe!
Tatizo Liko Wapi hapo?
 
Last edited by a moderator:
Inaendelea.....

Siku hiyo tukajikuta tumefanya mchezo husio faa kwa watoto wadogo ...basi ikawa zetu, tunajifungia ndani na kumaliza yote humo...

Maisha yalikuwa matam sana hata kimasomo nilikuwa vizuri kwani hapo kabla ufaulu wangu haukuwa mzuri..mi na mtoto mzuri kila kona ya mji, yeye mimi.. mimi yeye...namna tulivyokuwa tunapeana mahaba, wakatupachika jina la ''njiwa''...

Mambo yanabadirika baada ya jioni moja niko nae gheto huku tukiendelea kutomasana na kucheza michezo kama Wafanyavyo paka wadogo!...binti Akanipa taarifa iliyonistua sana ...alidai ana mimba yangu

lilinipa wakati mgumu ukizingatia bado nlikuwa nasoma na mzazi wangu ni mtata sana... endapo atasikia habari hizi itakuwaje?

Nililikabili Kiume kwani sikujutia kwa namna yoyote tena nikamwambia sitaki kusikia habari za kuitoa hiyo mimba...nitafanya juhudi zote ili kusolv mambo!



Itaendelea Wakuu

Hadithi ni nzuri na ina mafunzo ndani yake...!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom