Kwanza aliyejitambulisha kama baba mzazi wa binti alikuja juu.. kunilaumu ''kwa nini nimeidharirisha familia yake''....akadai nimeharibu maisha ya binti yake hivyo lazima nimuoe na nilipe fidia ya ushenzi nilosababisha...
Mda wote nilikuwa mpole nimenyea ka sio mimi, nikiwasikiliza huku kichwa kikiwa chini.. kama ishara ya kuonekana mkosaji!
Ikaamuriwa haraka sana nije nitoe mahari na nimchukue binti, ili nihararishwe kuwa nae...''nikawaambia niko tayari kutoa mahari hivyo waniambie ni kiasi gani''....Kwanza baba mkwe alikohoa kidogo na akaendelea....''binti yangu makapa ulivyomkuta nimegharamika kwa mambo mengi sana hivyo na kwa aibu hii, Utatoa milioni 2....ikiwa laki 5 ya shangazi, laki 5 ya mama na inayobaki ni kama mahari''
Kwakweli kiasi cha pesa hizo kwa mda ule ilikuwa mtihani kwangu hivyo nikaomba wanipunguzie kidogo na nitawalipa hivi karibuni!....baba mkwe alikuja juu safari hii akiwa kasimama kunielekea...''kijana mtoto wangu sio bidhaa ya mtumba mpaka uombe punguzo....Tena Ukifanya mchezo nitakufunga''...akazidi kng'aka.....''labda hilo la kukupa mda ila mda wenyewe ni wiki mbili uwe tayari umekamilisha hili suala!
Hapo kidogo nikapata nguvu..nikawaambia ''nimewaelewa, baada ya wiki mbili kila kitu kitaenda poa''..wakaniambia nije nimchukue binti siku hiyo nitakayoleta mahari!
Wakaniacha na mawazo kichwani kama..nilihisi kuchanganyikiwa kwakweli hasa nikifikiria hela inayotakiwa nami sina msaada wowote...wakati huo nilikuwa na akiba ya laki tano nilizokuwa nakusanya kidogo kidogo kwenye vibarua kwa ajili ya masuala ya shule.
Nikafiria hatimaye nikaona mtu pekee anayeweza kunisaidia ni mama yangu na rafiki yangu Bogoso..hivyo nilichoona kinafaa kwa mda huo, ni kuwashirikisha na ikibidi wanichangie kiasi chochote walichonacho
nikaanza kwa kumpigia sim mama yangu na kwakuwa alishajua kinachonisibu...alinielewa na akahaidi kunisaidia ila akasema nisubiri baada ya siku 3 atanitafuta
nikamtafuta rafiki yangu Bogoso ambaye tulisoma nae , alinisaidia kwa mambo mengi kwa kweli... kwani mwenzangu kwao kidogo walikuwa na uwezo, hivyo nilitegemea kupata msaada wake
****