Baba mkwe amekataa mahari yangu

Baada ya kuweka mizizi mizuri ukweni na kuwa na mahusiano mazuri na ukweni kwangu, niliamua nikatoe mahari baada ya miezi kadhaa kutoa posa, mshenga alimuuliza baba mkwe wajipanga vipi siku wakitaka kurudi hatua inayofuata.

Baba mkwe alisema nataka kuona hao wawili wana mahusiano mazuri.

Basi baada ya miezi kadhaa kupita ilibidi nitoe taarifa kwa mshenga kwamba nataka tukatoe mahari.

Taarifa ilimfkia baba mkwe na tulipanga siku ya kutoa mahari.

Ikiwa imesalia wiki moja kufika siku ya tukio, bibie alitangulia kwao ili kupokea wageni wake.

Ajabu baba mkwe aliomba kuongea na mimi, akanimbia anataka mimi niende kwanza kabla ya tukio.

Basi nilipohitikia wito wa baba mkwe, aliniuliza maswala mengi na tuliongea kama masaa 3 hivi na mchanganyiko wa story za huku na kule.

Baada ya maongezi, baba mkwe akasema sioni sababu za wewe kutoa mahari kikubwa ni kuzingatia hayo tuliongea na kumtanguliza Mungu.

Asema baba mkwe, naona kabisa ni jinsi gani mwenzio umemtunza na naona kabisa mabadiliko ya maisha kwa mwanangu, sikuwah kujua kama mwanangu ni mtu mwenye furaha hivi, siku hzi naona kabisa amechangamka tofauti na zamani.


Baada ya kurudi home,simu yangu moja kwa moja kwa mshenga kwamba ukweni hawataki mahari ila tutaenda kufamiana na maongezi zaidi lakini tusipeleke cent yeyote.


Mwenzenu nimeoa ndoa ya kanisani, licha bado tunaishi tofauti. hapa nafatilia maswala ya huakika cheti cha ndoa.
hiyo para ya meisho umeandika nini?
 
Namuunga mkono kabisa. Sikupokea magari ya binti yangu na vijana wangu nimewambia hakuna kupokea mahari kwa mabinti zao. Kifupi mwanangu aishi kwa furaha na asisimangiwe mahari. Na ukweli mkwe wangu ananiheshimisha kwa mambo ya hapa na pale bila hata kumuomba maana najitosheleza. Yapo mengi amefanya kwa familia kirafiki kuzidi hata mahari. Hivyo Tuwaone vijana wanaokuja kuoa mabinti zetu kama sehemu ya maisha ya familia kuliko waoaji. Tena ninamuita kwa jina lake la mwanzo kabisa. Kuna kipindi alitupeleka family vacation ya kibabe kabisa kutoka mfukoni kwao na binti yangu. Yaani tulilazwa 5 star hotel nje ya Tanzania. By the way mabinti zetu worth more than the pride price. They can't have real valued price tag.
 
Huyo Mzee ni Mtibeli.
Watibeli ndio tupo hivyo. Hatuwezi uza Binti zetu kama watumwa.
Ni Binti zetu, Binti wa Tibeli ni Binti huru.
Mtibeli kashadandia uzi na hakuna kitu mleta uzi unaweza kumfanya🤣🤣😇.. Nakubali sana pigo za Mtibeli by the way.💪💪💪
 
Afu ulipaswa ujiongeze,nunua blangeti la bibi na baba na mama na,Kanga na vitenge vya mashabgazi muulize mwenzio atakupa idadi ya wanaostahili kupata hivyo na mazaga mengine mwambie mkwe umeleta zawadi.Mama mkwe wako na shangazi watajua anagawaje hivyo kwa watu wana.

Usisahau shangazi ni baba,Shangazi apewe kitenge kizuri na shati la mumewe.

Ukimaliza kuja kunishukuru.
 
Afu ulipaswa ujiongeze,nunua blangeti la bibi na baba na mama na,Kanga na vitenge vya mashabgazi muulize mwenzio atakupa idadi ya wanaostahili kupata hivyo na mazaga mengine mwambie mkwe umeleta zawadi.Mama mkwe wako na shangazi watajua anagawaje hivyo kwa watu wana.

Usisahau shangazi ni baba,Shangazi apewe kitenge kizuri na shati la mumewe.

Ukimaliza kuja kunishukuru.

Umetisha sana mkue
 
Hongera mkuu.
Kuna nyinyi mnasamehewa mahari ,kuna wale wanapewa mahari na watoto wa kike halafu kuna kina sisi wa mahari mtajijua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom