Sio yeye tu kuna watanzania wengi tu wamekufa kwa sababu ya kupata huo mshtuko wa Mbowe kukamatwa kwa UgaidiFamilia ya Freeman Aikael Mbowe wametangaza kifo cha Baba Mdogo wa Mbowe aitwaye Manase Alphayo Mbowe aliyefariki baada ya kupata mshtuko baada ya kupata taarifa za mwanaye kutuhumiwa Ugaidi
Amefariki Hospitali ya Machame Julai 23, alikopelekwa baada ya kupata mshtuko
Freeman Mbowe ametuhumiwa kupanga njama za ugaidi na kuua viongozi wa serikali
MANASE Alphayo Mbowe, baba mdogo wa Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe, amefariki dunia asubuhi ya leo Ijumaa, tarehe 23 katika Hospitali ya Machame mkoani Kilimanjaro, alikokuwa anapatiwa matibabu.
Taarifa ya kifo hicho imetolewa leo Ijumaa na James, mtoto wa Freeman wakati akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu akisema, alishtushwa baada ya kusikia tuhuma zinazomkabili mwanae za ugaidi
James amesema, babu yake huyo alifariki dunia akipatiwa msaada wa kupumua kwa kutumia mashine ya oksijeni, hospitalini hapo lakini “leo asubuhi akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo amefariki dunia.”
James amesema, taratibu za mazishi yake zitatangazwa baadae baada ya familia kukutana.
Amesema, enzi za uhai wake, babu yake huyo aliwahi kufanya kazi serikalini ikiwemo ofisi ya Rais. Ameacha watoto watano, wa kike mmoja na wa kiume wanne.
View attachment 1864583
Manase Mbowe enzi za uhai wake
Goliati na Farao kufa, haimaanishi Daudi na Musa wasingekufa, walikuwa na kiburi cha uzima, elewa tofauti...Nyumbx walisema wanaokufa ni wale wenye roho mbaya tu, vipi baba mdogo na yeye alikuwa katili sana?
Alale anapostahili baba mdogo wa Mbowe.
CCM ni chama cha kishetani, kidhalimu, kiharamia na kinajisi kinacholenga kuidhoofisha nchi yetu nzuri ajabu na tajiri aliyotupa MUNGU Mwenyezi. Ee Mungu, Muumba wa Mbingu na nchi na vyote vinavyoonekana na visivyoonekana, uturehemu.RIP Manase
Jumong akituma pole tena mnitag
Acha tu anamfananisha Mandela na takataka.Usimfananishe Mandela na upuuzi
Si walisema gaidi?Tunategemea tweet ya pole toka kwa mama
Kweli. May his soul rest in eternal peaceAh ni ukuu wa mungu ulio muondoa mwendazake ndio ulio muondoa na huyu pia sivyo?
Pole kwa familia
Hakuna cha natural death wala nini, baba mdogo sasa naye ni mwendazake tu.Hii ni natural death ila mwendazake sio natural death CCM mna vinyesi kichwani mwenu
Mbali ya mambo mengine Makuzi pia yanachangia kwenye ujasiri wa mtu.Mwamba majanga yanamuandama ila anapambana hadi mwisho. Huyu mwamba simuelewagi kabisa ana moyo wa namna gani yaani hadhoofishiki. Hata hili litapita na atakuwa imara kuliko jana.
Ndiyo ni mwendazake amekufa kama jiwe alivyokufaHakuna cha natural death wala nini, baba mdogo sasa naye ni mwendazake tu.
Sasa shida iko wapi?Ndiyo ni mwendazake amekufa kama jiwe alivyokufa
Shida ipo pale vichenchede mnapokataa kuwa sio natural deathSasa shida iko wapi?
Hamna lolote lile. Baba mdogo ndio keshakuwa mwendazake, kubali kataa haijalishi.Shida ipo pale vichenchede mnapokataa kuwa sio natural death
Ni natural death au Mbowe Kahusika??Hamna lolote lile. Baba mdogo ndio keshakuwa mwendazake, kubali kataa haijalishi.
Ahusike au asihusike mimi sijui.Ni natural death au Mbowe Kahusika??
Mtungi wa gesi ya oxygen aliopatiwa baada kupata changamoto la upumuaji baaa ya kutoka kwenye msiba wa marehemu kaka yake na F. Mbowe. Jamaani hili janga la corona tusilifanyie mzaha. Tuchuke tahadhari zote tunazoshauriwa na watalamu wa afya. Misangamano ya watu iwe marufuku na wala kusiwe na kibali cho chote kuruhusu misongamano. Iwe kwenye nyumba za ibada, viwanja za michezo, sherehe za arusi, kwenye daladala, kwenye mabasi, majumbani na kwenye masoko iwe marufuku.Umetumia kipimo gani kujua chanzo cha kifo chake?