Baba Askofu Dr. Benson Bagonza: Tuheshimu nguvu ya hoja

Baba Askofu Dr. Benson Bagonza: Tuheshimu nguvu ya hoja

Msambwata Happy Birthday Tanganyika kwa sababu Zanzibar ipo na ina Bendera na wimbo wa Taifa.

Why are you all guys shy to mention Tanganyika what’s wrong. Kama ziliungana Tanganyika na Zanzibar ikazaliwa Tanzania we have either to become one country with one name Tanzania but as long as Zanzibar has its own constitution we demand to have another constitution for Tanganyika and bury the union or have a federation. Vinginevyo CCM can’t keep on fooling around!
Mi nimemnukuu baba askofu tu mkuu
 
Askofu wa waasi KKKT anapojaribu kumsemea askofu wa kikatoliki...
 
Bishop Bagonza siku zote ananyoosha, nampenda Bure...hata nae kama atahojiwa uraia kama mwenzake NiweMugizi, ujumbe utakuwa tayari umefika....bado nakumbuka ile clip yake iliyosambaa sana siku chache zilizopita kuhusu "kuwafukuza shule watoto wa kike kila wanapopata ujauzito" akisema..."viongozi wetu wa juu serikalini ni matunda ya kukosea, bahati nzuri walipewa nafasi ya pili na ndo maana wamefikia hapa walipofikia...bahati mbaya sana wao waliopewa nafasi ya pili wanawafungia nafasi hiyo watoto wa wenzao"

Barikiwa mababa zetu.
 
Ukiona nguvu nyingi (siyo akili), zinatumika kulinda watu badala ya kulinda uhuru, ujue taifa hilo linakaribia mwisho wa kufikiri. Tujadili.

Tujadili bila kugombana wala kukashifiana. Utaifa hujengwa kwa fikra pevu. Utaifa na uzalendo haujengwi ...... bunduki.
Baba Askofu, Mungu azidi kukubariki. Ni sauti ya Nabii kwa Taifa!
 
Nimefarijika sana na maneno yenye busara kutoka kwa mtu mwenye busara na hekima,
Nchi inaongozwa na mabashite wawili wasio na huruma wala dira,
Na wanalindwa kuliko uhuru uliopiganiwa toka kwa wakoloni
 
SOMO LA URAIA: UHURU MIAKA 56.

Tuheshimu Nguvu ya hoja.

1. Hadi Desemba 1961, tulikuwa tunapigania kupata uhuru, siyo serikali. Kwa hiyo kilichopatikana siku hiyo usiku ni "Uhuru", si serikali. Serikali ilikuwapo hata kama hatukuwa tunaipenda. Wakati wote tunaenda mpaka Umoja wa Mataifa (UNO), serikali ilikuwapo lkn hatukuwa na uhuru. Siku hizi serikali ni muhimu kuliko uhuru. Tujadili kwa nini?

2. Katika utawala wa kikoloni, serikali ndiyo huinyoosha nchi, na nchi ni wananchi. Katika utawala bora, (uongozi), wananchi ndio wanaoinyoosha serikali. Kunyoosha ni dhana ya kikoloni inayoamini wananchi wana tatizo! Wakoloni walidai wanatunyoosha ili kutuendeleza. Kumnyoosha aliyekupigia kura inahitaji uagane na ustaarabu au kuuweka pembeni kwa makusudi maalum. Tujadili.

3. Uhuru hauna sura wala umbo; ni dhana na tunu kwa taifa. Ktk za nchi za kidemokrasia, uhuru ndicho kitu cha kipekee kinacholindwa kwa nguvu zote. Ukiona nguvu nyingi (siyo akili), zinatumika kulinda watu badala ya kulinda uhuru, ujue taifa hilo linakaribia mwisho wa kufikiri. Tujadili.

4. Kwa mantiki ya niliyosema juu, utakuta vijana wengi wana kumbukumbu nyingi kuliko ndoto. Kumbukumbu zikiwa nyingi kuliko ndoto ni dalili ya taifa kuwa limesimama. Jana haiwezi kuwa bora kuliko kesho tukawa salama. Vijana wanahitaji ndoto nyingi kuliko kumbukumbu. Tujadili bila kugombana wala kukashifiana. Utaifa hujengwa kwa fikra pevu. Utaifa na uzalendo haujengwi kwa matofali, zege wala bunduki.
 
ANAANDIKA BABA ASKOFU DR BENSON BAGONZA WA KKKT DAYOSISI YA KARAGWE
SOMO LA URAIA: UHURU MIAKA 56.

Tuheshimu Nguvu ya hoja.

1. Hadi Desemba 1961, tulikuwa tunapigania kupata uhuru, siyo serikali. Kwa hiyo kilichopatikana siku hiyo usiku ni "Uhuru", si serikali. Serikali ilikuwapo hata kama hatukuwa tunaipenda.

Wakati wote tunaenda mpaka Umoja wa Mataifa (UNO), serikali ilikuwapo lkn hatukuwa na uhuru. Siku hizi serikali ni muhimu kuliko uhuru. Tujadili kwa nini?

2. Katika utawala wa kikoloni, serikali ndiyo huinyoosha nchi, na nchi ni wananchi. Katika utawala bora, (uongozi), wananchi ndio wanaoinyoosha serikali.

Kunyoosha ni dhana ya kikoloni inayoamini wananchi wana tatizo! Wakoloni walidai wanatunyoosha ili kutuendeleza. Kumnyoosha aliyekupigia kura inahitaji uagane na ustaarabu au kuuweka pembeni kwa makusudi maalum. Tujadili.

3. Uhuru hauna sura wala umbo; ni dhana na tunu kwa taifa. Ktk za nchi za kidemokrasia, uhuru ndicho kitu cha kipekee kinacholindwa kwa nguvu zote.

Ukiona nguvu nyingi (siyo akili), zinatumika kulinda watu badala ya kulinda uhuru, ujue taifa hilo linakaribia mwisho wa kufikiri. Tujadili.

4. Kwa mantiki ya niliyosema juu, utakuta vijana wengi wana kumbukumbu nyingi kuliko ndoto. Kumbukumbu zikiwa nyingi kuliko ndoto ni dalili ya taifa kuwa limesimama. Jana haiwezi kuwa bora kuliko kesho tukawa salama.

Vijana wanahitaji ndoto nyingi kuliko kumbukumbu. Tujadili bila kugombana wala kukashifiana. Utaifa hujengwa kwa fikra pevu. Utaifa na uzalendo haujengwi kwa matofali, zege wala bunduki.

Belated Happy Birthday Tanzania.


Note: Naona maaskofu wameanza kuamka
Daaah my school mate Bagonza sasa unayarejea yale maisha ya shule!! Hakika unazirejea akili zako.

Hili bandiko zito sana!!!!
 
Back
Top Bottom