Wasiache kumsifia kwa jeuri gani waliyonayo wakati wazazi wao wanahemea kwa bwana mkubwa? Statistically, wengi wa watanzania walioko nje ni wale wale - the elite.
Wangekuwa na ujasiri wa Shyrose Bhanji wa kusema beleshi sio kijiko lingekuwa jambo la maana. Hizi artificial pongezi ni kumhadaa rais! Kwa bahati mbaya sana washauri wa rais wetu wamekuwa wanaweka nguvu kubwa sana kumjenga nje ya nchi kuliko kwa walalahoi -wapiga kura! Na yeye rais anaonekana kabisa kuridhika na mikakati hii ya kumjengea sifa kwa watu ambao hawana direct knowledge ya kile kinachowapa watu hasira.
Chanzo cha yeye (rais) kupoteza umaarufu ni hapa nyumbani na sio huko kwa wazungu! Sasa hizi porojo wanazopeana huko majuu zitabadilisha nini kama sio kuwapa critics wake mtaji wa kumkosoa zaidi?
Kati ya hao 500 waliotoa sifa ni nani anayeshi kwenye masaa 12 ya giza kila siku? Ni nani aliyeonja joto ya mgomo wa wauza mafuta huku safu ya watendaji wakuu (rais akiwepo) wakiwa kimya? Ni nani anayenunua sukari kwa Tshs 2,500? Inflation ya Tanzania kwa sasa tuko above 14% mwaka 2005 ilikuwa chini ya 5%!
Kwa nini wasitumie nafasi waliyopata ya kuonana na rais kwa kumueleza mikakati mbadala ya kuondokana na adha hii ya maisha magumu?
Kichekesho ukiongea (privately) na baadhi ya waliodhuria mkutano huo wa kusifiana wanamponda rais kimoja lakini hapa tuaambiwa wamempongeza! unafiki!