Baadhi ya Watanzania Waishio Marekani wampongeza JK

Msilete hoja zenu hapa za facebook(chadema vs ccm).hapa tunathink beeore arguing sio mnakurupuka.wamemshukuru coz anawashirikisha ktk dvt ya nchi yao.kuna ubaya gani hapo?.wanamshukuru kutaka kuanzisha uraia wa nchi 2 nalo ni kosa?.tujadili haya sio ujinga wenu wa kimagwanda gwanda na ukomandoo.kikwete is the best president ambaye tumempata,anatuletea katiba mpya hata hili mnaponda?.
Karibu JF naona umekaa ki-facebook zaidi. Mmepata rais?
 
Nyie ni "Warusha Mawe" Kumbukeni Wakati wa ukombozi kule South na vilevile sasa hivi Palestina kuna wale wa nje na wale so called Warusha Mawe..Punguzeni kulia lia kama watoto ..na endeleeni kuwarushia mawe police
 
Ukiwa na ubongo kama wa wa-akina twahil, hesabu maumivu yamekolea!!! Mtu bila haya anasema JK ni best prsident we have ever had!!!

My foot, JK ni janga la kitaifa...
 
Nilieleze masikitiko yangu kuhusu the so called "Great Thinkers" wa JF! Nilipojiunga na JF nilikuwa nimevutiwa na maoni na mijadala mbalimbali kuhusu mustakabali wa taifa letu. Kadri ninavyoendelea kushiriki hususan kwa kusoma maoni yanayojitokeza hapa, ninazidi kukata tamaa kwamba taifa hili halina wakaombozi (angaa wa kifikira). Kuhusu suala la Watanzania waishio Marekani: ni kweli vyombo vya habari vimehabarisha kuhusu walichokiona pale DC. Kwanza kabisa, na kwa bahati mbaya, waandishi au watoa taarifa hawakujishughulisha kubainisha makundi yaliyokuwa katika hadhira ile ambapo kwa mahesabu ya harakaharaka wajumbe kutoka Tanzania walifikia takribani nusu ya hadhira.
Lakini hoja muhimu ninayotaka kuelezea hapa ni kwamba Watanzania waishio ughaibuni ni kama Watanzania waishio nyumbani: tumeshuhudia Mhe Raisi Dkt JK anapohitisha mkutano pale Jangwani uwanja ukifurika hadi Magomeni. Hiyo hadhira ni sehemu ndogo sana ya Watanzania na hatuwezi kuhitimisha kuwa Watanzania wote waishio nyumbani wanaunga mkono Rais JK. Vivyo hivyo, hata kama hadhira iliyohudhuria mkutano wa DICOTA ingekuwa ni watu elfu moja na wote wakamsifia JK, huwezi kuhitimisha kuwa Watanzania waishio ughaibuni wote wana mtazamo mmoja! Jamani jaribuni angaa tujaribu ku-pretend tu kuwa Great Thinkers tunapochambua au kutoa maoni kuhusu matukio nk., haka kama sio kweli kwamba tu ma-Great Thinkers. :confused:
 
Hivi alikutana na Watanzania wote wenye shida na malalamiko?

Au alikutana na wote waliopata faida ya Serikali Mlango wa nyuma na wengine kwa kujuana who's who?

Angalia hiyo kamati...

Kuna watanzania ambao wanahitaji Msaada walichaguliwa kwenda kusoma Marekani na walipofika Masomoni pesa zilikatwa na kupewa Mtoto wa Who's Who

Kuna watanzania ambao wako huku hakuna Msaada wa Serikali au Ubalozi na wana biashara kubwa na halali lakini hawakuweza kuchaguliwa au hawakupewa Meza sababu maendeleo yao hakuna waliotarajia kati ya hao ambao wako kwenye Kamati.

Kamati yenyewe ina wivu; wao ndio Kikwete na kila kitu ...

It is a damn shame...
 
Unaposoma maoni ya GT, jaribu kufikiri na baadaye uelewe katika 3D. Anyway, siku u Baby ukiisha utaelewa.

Amemtaja wapi mama wa mtu?...au na wewe ni mmoja ya wale wanaofikiri kwa masaburi??....nyambafu
 
Sizani kama kuna haja ya msingi ya kuwalaumu watanzania waishio nje ya nchi kwa kuwajumuisha,wengi wa hao wanaopongeza serikali ya JK ni wale wale wanaofaidika moja kwa moja na dhuluma za serikali kwa wananchi ama kwa kupitia jamaa zao.Kwa hiyo kwa namna moja ama nyingine lazima waipongezi serikali ya Jk kwani ndio inayowalinda.Ila ukweli ni kwaba hao ni tone la maji baharini ,watanzania wameshachoka na utawala wa kiimla usio na mwelekeo wala dira wa JK.Huyu bwana ameshachokwa na hata baadhi ya wapenda maendeleo waliopo kwenye chama chake.
Wengi wanaojikomba kwake ni wale maswahiba ambao amewapa vyeo aidha wao wenyewe ama ndugu zao.
Suala la msingi hakuna mtanzania anayekubaliana na hali ya aisha inavyokuwa ngumu hata tulio nje ya nchi ,kwani tulizoea kutuma 200$ kwa mwezi nyubani kwa sasa haiwezekani(Haitoshi) kutokana na inflation iliyopo ,ambayo kimsingi imesababishwa na mipango mibovu isiyo na mwelekeo ya serikali ya JK.Kwa hiyo hali ya Maisha ya watanzania inatugusa sote na kama wapenda maendeleo hatuungi mkono ufisadi ufedhuli na unyanyasaji unaofanywa na Serikali ya CCM.
 
Mimi naona watu wengi wameanza kuwa na pumba siku hizi. Dicota sio chombo cha siasa na kitaalika raisi wa Tanzania ambaye yuko madarakani kutupa hali ya Tanzania bila kujali chama alichotoka. Siasa sio kila kitu na hatuwezi kuacha kuongea na raisi kwasababu ya matatizo yaliyopo nyumbani bila kujali mambo ya siasa. Pili ni lazima muelewe raisi ni mtu ambaye anaongea dakika 20 tu na kuondoka kwenye huu mkutano raisi amepongezwa kwa kufika kwani alikuwa akialikwa kila mwaka. Watu ambao ni muhimu na watu walitaka kujua zaidi ni Gavana wa Tanzania, Katibu mkuu wa ardhi, Banks, NSSF, PPF, TRA, World Bank, MC Fund ya Marekani, Non Profits zinazofanya kazi Tanzania, Wizara ya mambo ya nje na Wafanyabiashara wa Tanzania ukweli hawa watu ndiyo waliotumia muda mrefu kujadili mambo mbali mbali. Nchi yetu haiwezi kuendelea kwa ushabiki wa uongo kama hatujui mambo tuulize.
 
Watanzania achaneni na usanii huu. Picha za kongamano la watu 500 ziko wapi?
Hiyo idadi ya makampuni 15 kutoka Tanzania yalikuja kwenye mkutano huo ndio waliojaza chumba pamoja na wafanyakazi wa ubalozi wa DC na NY.

Kama walihudhuria basi ni watoto wa vibosile, wengine hawana muda na kasumba hiyo. Kazi huko wanahesabu hadi secunde ndipo ulipwe chako, nani yuko tayari kupotezea muda mikutano ya kujitanua watumishi wa serikali?

Ukitaka kuhakiki niliyosema, kama una mtu au rafiki mtanzania anayeishi Marekani umwulize habari hiyo utaona wote hawajui ni kitu gani na kimetokea wapi. Kama wapo wachache ni wale wale akina
@New York City wenye mtandao wao na hao watanuaji wa bongo.
 
Aibu kubwa sana kwani ukweli ni kwamba Kikwete alipokewa na mabango machafu ajabu na ujumbe ulifika ila waandishi wa habari hawakufanya kazi yao bali hongo ilitawala

Mkuu haikosi ulipiga picha za tukio la watz waliobeba mabango huko u es ei; unaonaje basi ukizimwaga hapa ili tuone mkulu wa kayaa alivyodharirshwa huko kwa braza Baraka?!
 
DICOTA na members wote wanajua mgao wa umeme,ukosefu wa ajira,njaa,huduma mbovu za kijamii,umaskini,unyanyasaji etc vitu vinavyo wasumbua watanganyika?danganya toto
 
Back
Top Bottom