Baadhi ya Watanzania Waishio Marekani wampongeza JK

Salimia

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
665
103
Hivi hawa ni walewale waliotaka kuandamana??











JMK(26).jpg

Rais Jakaya Kikwete


Watanzania waishio Marekani wamesifia jitihada za Rais Kikwete za kuwashirikisha katika maendeleo ya Tanzania kwa lengo la kukuza uchumi.
Hayo yalisemwa jana kwenye kilele cha Kongamano la Tatu la Watanzania Waishio Ughaibuni mjini hapa ambapo Watanzania zaidi ya 500 wamehudhuria pamoja na makampuni, mashirika ya umma na binafsi zaidi ya 15 kutoka Tanzania yamehudhuria kongamano hilo .

Miongoni mwa mambo yaliyowavutia ni hotuba ya Rais Kikwete ambayo alifafanua masuala ya uraia pacha na haki ya kupiga kura kwa Watanzania walioko nje ya nchi kuingizwa kwenye mjadala wa Katiba mpya.

Rais Kikwete aliwasihi Watanzania wasirudi nyuma katika kujiletea maendeleo hata kama wako mbali na nyumbani.

Rais wa DICOTA Dk. Ndaga Mwakabuta ,alisema: "Tumeguswa na ujio wa Rais Kikwete na Mawaziri walioongozana naye na Makatibu Wakuu hapa Marekani.

Tumeona jinsi Rais anavyojali mchango wetu, ana imani na sisi, ametushirikisha na kuelekeza wasaidizi wake na watendaji waungane na sisi kwenye suala zima la uraia wa nchi mbili, hii ni faraja kubwa kwetu."

Wengine walisema Kongamano hili limewabadilisha fikra zao kuhusu utendaji kazi wa Serikali, ambapo sasa wana imani ya kupata mafanikio kutokana na jitihada zinazofanywa na serikali ili kuwasaidia kupeleka maendeleo yao nyumbani na hatimaye kuinua uchumi wa nchi.

Kongamano la DICOTA (Baraza la Watanzania Waishio Ughaibuni Marekani) hufanyika kila mwaka kuanzia mwaka 2009 kwa kuwaleta pamoja Watanzania kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo.

source: Nipashe ippmedia
 
Aibu kubwa sana kwani ukweli ni kwamba Kikwete alipokewa na mabango machafu ajabu na ujumbe ulifika ila waandishi wa habari hawakufanya kazi yao bali hongo ilitawala
 
Wana njaa sana wale jamaa. Wengi wao wanafanya kazi za kuosha vyombo mahotelini na kufagia mabarabara. Ukiwaambia warudi kufagia barabara za huku bongo wanaona sio dili. Ndio maana wameamua kujipendekeza kwa JK kutimiza ile sera ya CCM ya JIKOMBE UKOMBOLEWE
 
kwa kweli naapa sina imani na watanzania waishio huko ughaibuni.

Mkuu kumbuka wahenga walisganena"alieshiba hamjui mwenye njaa".Cha msingi sisi tunaoishi hapa Tz tuangalie namna ya kuwang'oa hawa mafisadi Wa ccm ifikapo 2015 na tusisahau uundwaji Wa KATIBA MPYA KABLA YA 2015.
 
Msilete hoja zenu hapa za facebook(chadema vs ccm).hapa tunathink beeore arguing sio mnakurupuka.wamemshukuru coz anawashirikisha ktk dvt ya nchi yao.kuna ubaya gani hapo?.wanamshukuru kutaka kuanzisha uraia wa nchi 2 nalo ni kosa?.tujadili haya sio ujinga wenu wa kimagwanda gwanda na ukomandoo.kikwete is the best president ambaye tumempata,anatuletea katiba mpya hata hili mnaponda?.
 
Wasiache kumsifia kwa jeuri gani waliyonayo wakati wazazi wao wanahemea kwa bwana mkubwa? Statistically, wengi wa watanzania walioko nje ni wale wale - the elite.

Wangekuwa na ujasiri wa Shyrose Bhanji wa kusema beleshi sio kijiko lingekuwa jambo la maana. Hizi artificial pongezi ni kumhadaa rais! Kwa bahati mbaya sana washauri wa rais wetu wamekuwa wanaweka nguvu kubwa sana kumjenga nje ya nchi kuliko kwa walalahoi -wapiga kura! Na yeye rais anaonekana kabisa kuridhika na mikakati hii ya kumjengea sifa kwa watu ambao hawana direct knowledge ya kile kinachowapa watu hasira. Chanzo cha yeye (rais) kupoteza umaarufu ni hapa nyumbani na sio huko kwa wazungu! Sasa hizi porojo wanazopeana huko majuu zitabadilisha nini kama sio kuwapa critics wake mtaji wa kumkosoa zaidi?

Kati ya hao 500 waliotoa sifa ni nani anayeshi kwenye masaa 12 ya giza kila siku? Ni nani aliyeonja joto ya mgomo wa wauza mafuta huku safu ya watendaji wakuu (rais akiwepo) wakiwa kimya? Ni nani anayenunua sukari kwa Tshs 2,500? Inflation ya Tanzania kwa sasa tuko above 14% mwaka 2005 ilikuwa chini ya 5%!

Kwa nini wasitumie nafasi waliyopata ya kuonana na rais kwa kumueleza mikakati mbadala ya kuondokana na adha hii ya maisha magumu? Kichekesho ukiongea (privately) na baadhi ya waliodhuria mkutano huo wa kusifiana wanamponda rais kimoja lakini hapa tuaambiwa wamempongeza! unafiki!
 
Hivi hawa ni walewale waliotaka kuandamana??

Kongamano la DICOTA (Baraza la Watanzania Waishio Ughaibuni Marekani) hufanyika kila mwaka kuanzia mwaka 2009 kwa kuwaleta pamoja Watanzania kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo.
source: Nipashe ippmedia

Hapo ndipo panaponipa shida kidogo. Ingekuwa vyema kama wangetumegea hayo masuala ya maendeleo wanaliyoyajadili. Uraia wa nchi pacha wawezi kuwa miongoni, lakini isiwemo kwenye mjadala kwani hata kina Rostitamu tunasikia wanazo mbili
 
Wasiache kumsifia kwa jeuri gani waliyonayo wakati wazazi wao wanahemea kwa bwana mkubwa? Statistically, wengi wa watanzania walioko nje ni wale wale - the elite.

Wangekuwa na ujasiri wa Shyrose Bhanji wa kusema beleshi sio kijiko lingekuwa jambo la maana. Hizi artificial pongezi ni kumhadaa rais! Kwa bahati mbaya sana washauri wa rais wetu wamekuwa wanaweka nguvu kubwa sana kumjenga nje ya nchi kuliko kwa walalahoi -wapiga kura! Na yeye rais anaonekana kabisa kuridhika na mikakati hii ya kumjengea sifa kwa watu ambao hawana direct knowledge ya kile kinachowapa watu hasira.

Chanzo cha yeye (rais) kupoteza umaarufu ni hapa nyumbani na sio huko kwa wazungu! Sasa hizi porojo wanazopeana huko majuu zitabadilisha nini kama sio kuwapa critics wake mtaji wa kumkosoa zaidi?

Kati ya hao 500 waliotoa sifa ni nani anayeshi kwenye masaa 12 ya giza kila siku? Ni nani aliyeonja joto ya mgomo wa wauza mafuta huku safu ya watendaji wakuu (rais akiwepo) wakiwa kimya? Ni nani anayenunua sukari kwa Tshs 2,500? Inflation ya Tanzania kwa sasa tuko above 14% mwaka 2005 ilikuwa chini ya 5%!

Kwa nini wasitumie nafasi waliyopata ya kuonana na rais kwa kumueleza mikakati mbadala ya kuondokana na adha hii ya maisha magumu?


Kichekesho ukiongea (privately) na baadhi ya waliodhuria mkutano huo wa kusifiana wanamponda rais kimoja lakini hapa tuaambiwa wamempongeza! unafiki!

Mkuu ahasante kwa kusema mambo ambayo hawa jamaa wanaojifanya wako ughaibuni hawafahamu. Unajua hawa MENDE/MAPANYA hawajui namna tunavyoteseka huku nyumbani kwa utawala wa mafisadi. Karne hii bado Usiku tunakaa gizani kama yule mnyama aitwaye muhanga kwa sababu ya umeme. Jana nilikuwa namsiliza Afisa uhusiano wa Tanesco anadai wanalalamikiwa bure wakati watu wanaostahili lawama ni Pan African Energy kwa kusupply gas kidogo.

Anadai serkali isilaumiwe, Nilishangaa kusikia kauli hiyo inayooonyesha jinsi serikali yetu ilivyoishiwa mikakati ya kuongoza hii nchi.Sasa aingii akilini watu wanaokula milo yote kila siku na hawaguswi na matatizo ya watanzania wanaanza kumsifia jk kuwa analeta maendeleo. Hii serikali imefilisika pamoja na wananchi wake.

Kila kona njaa, ugumu wa maisha, hakuna sukari, mafuta bei juu, ufisadi umeshamiri, hakuna maji, reli imekufa, usafiri juu, hakuna ndege, bandari inaperform under capacity, gutter politics, wanafunzi hawapati mikopo, elimu imeshuka nk. Mkuu kama ulivyosema hapo juu hawa jamaa wa ugaibuni ni watoto wa mafisadi walioiba hela za walala hoi wakaenda kuishi huko marekani na sasa hivi wanalipa fadhila kwa pongezi za kinafiki.

Mungu ibariki Tanzania, tuwezeshe tufike huko tunakotaka
Amen
 
Msilete hoja zenu hapa za facebook(chadema vs ccm).hapa tunathink beeore arguing sio mnakurupuka.wamemshukuru coz anawashirikisha ktk dvt ya nchi yao.kuna ubaya gani hapo?.wanamshukuru kutaka kuanzisha uraia wa nchi 2 nalo ni kosa?.tujadili haya sio ujinga wenu wa kimagwanda gwanda na ukomandoo.kikwete is the best president ambaye tumempata,anatuletea katiba mpya hata hili mnaponda?.

Du! kweli tutafika? Hebu tueleze amewashirikisha vipi katika maendeleo ya nchi yao? Huo uraia wa nchi mbili umeanza kujadiliwa lini na mpaka leo hakuna kitu? Yaani unasifia katiba mpya bila ya kujali ndani yake kuna nini?

Hiyo sehemu niliyopigia mstari ndio umeniacha hoi kabisa. WaTanzania tunadanganyika kirahisi sana. No wonder rasilimali zetu zinauzwa kwa bei ya kutupa.
 
Mh!kaazi kweli kweli..mtanzania wa kawaida ambaye hata shule ni mungu asaidie, hatoweza kuelewa alipo, wala anapoelekea maana tunayumbishwa na vyombo vya habari regardless ni old media or new media like social media. Hawa wanasema hivi wale vile, wengine hawaelewi which is which, sometimes i dont believe media!damn!they are just confusing innocent,ordinary citizens!!!
 
Mbona ni aibu kubwa kwa watu wetu walihuko kumpokea kwa heshima wakati mamilioni ya wa tz hapa wako gizani, Songea mafuta hakuna, sukari haishikiki nchi nzima, njaa kali sana sehemu nyingi za nchi hii huyu aliopaswa kupokelewa na mabango na kuelezwa hisia za wananchi wake.
 
Aibu kubwa sana kwani ukweli ni kwamba Kikwete alipokewa na mabango machafu ajabu na ujumbe ulifika ila waandishi wa habari hawakufanya kazi yao bali hongo ilitawala

Mkuu kwani wewe au wenzako mlikosa Camera au Simu.... ?
au vyote vilikuwa Blocked...?
Mhh this is insulting peoples intelligence..
 
Haowote ni mabecktatu wa huko Marekani Suala la Suit, si hata mchukuzi anaweza nunua? mi nawaona waouuzi tuu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom