Sasa uwanja wa ndege bila kuwa na vivutio hauna maana. Sioni kosa hapo. Rubondo kuna wanyama. Wakiongezea maeneo mengine yenye wanyama ukanda huo kuna shida gani?Pamoja na kwamba jiwe ni mbinafsi, ila kwa hili sioni kama ni kosa. Kwangu huu naona ni utaratibu wa kawaida kuhamisha wanyama kwenda mbuga nyingine. Kwa hili kupitia ubinafsi wake naona kapatia.
Nimeona hiyo clip na ninakuwa mgumu kuamini kwamba hapo ni 'chuttle' na hao wanyama wanaletwa hapo toka kungineko. Kama hii ni kweli basi wataalamu watasema yao lakini mimi nitaendelea kuamini zaidi na zaidi kuwa kwa hakika wako watendaji wateule ambao ni wapu.mbavu!Ndugu zangu tuwe makini tusije kuamka kesho tukasikia mlima Kilimanjaro unahamishiwa wilaya pendwa, maana hifadhi za wanyamapori zimeanza kuhamishiwa wilaya pendwa.
Mkuu unachosema kinaweza kuwa sahihi, lakini kwa nini iwe Chato, nasio hifadhi nyingine yeyote nchini?.
we nae ni kilaza kama walivyo vilaza wengine hivi hilo jambo la wanyama kuhamishwa ndo unaliskia leo?
mbona lipo siku nyingi sana?
Au kwasabu ni chato ndo imekua shida?
Uko sahihi hasa ubinafsi ndio hoja yamsingi hapa, hasa kwa sasa au kipindi hichi ambapo inaonekana kama kuna baadhi ya maeneo yanapendelewa hasa yanayotoka wakubwa.Ndugu hii ndio Africa wakati mwingine hayo huwezi kuyakwepa japo kweli yanakera. Kwenye nchi ambayo rais yuko juu ya katiba na sheria hakuna namna unaweza kukwepa. Ili miradi jambo hilo halina athari kwenye haki za binadamu na halikupungizii lolote unalipotezea. Ninachojaribu ni kuangalia positive impact ya jambo hilo, kwangu naona huko mbeleni litakuwa na tija. Narudia tena, kwa hili japo ni la ubinafsi wa wazi lakini rais kapatia.
Watanzania sometimes tunapenda kulalamika bila kufanya uchunguzi na kujudge picha na video za kwenye mitandao,nilikuwa kwenye hiyo mbuga miezi miwili iliyopita na kweli kuna baadhi ya wanyama ambao ni wengi kwenye hiyo mbuga na baadhi kupunguzwa na kuhamishwa kwenye mbuga nyingine mpya,mbuga mpya imefunguliwa,wanyama wanaongezwa ili waende kuzaliana kwenye mbunga hiyo mpya .
Hayo ni maendeleo,kuna misitu mingi sana hii Tanzania na Mapori ambayo bado hazijaitwa mbuga na kuna wanyama wachache mno,,kuongeza wanyama au kuanzisha mbuga mpya ni akili nzuri sana.
Tuangalie hata baadhi ya mbuga za Africa kusini.
Serengeti ina nyumbu zaidi ya million moja na nusu,unaona wivu nyumbu kumi jinsia tofauti kukamatwa na kupelekwa kwenye mbuga mpya?swala wako wangapi mikumi?Twiga wapo wangapi?
Hatari Sana ,Watu wana force CHATO iwe kama Brooklyn.

Ndugu zangu tuwe makini tusije kuamka kesho tukasikia mlima Kilimanjaro unahamishiwa wilaya pendwa, maana hifadhi za wanyamapori zimeanza kuhamishiwa wilaya pendwa.
Kama hii ni kawaida ni jambo jema sana! Sasa kwa nini hii iwe habari?
Umeongea vizuri sana kaka. Kwa sisi wana ikolojia na wanamazingira huu ni mkakati mkubwa na mzuri katika kuhakikisha tunalinda na kuhifadhi ikolojia. Hilo eneo lilikuwa eneo la jumuiya (WMA) so faida zitakazopatikana baada ya kuwa National Park ni kubwa, kwetu sisi wanaikolojia na mazingira tunasema wazo zuri na litasaidia kukuza pia kipato kwa wananchi wanaoishi kando kando ya hifadhi hiyo mpya.