Baadhi ya wanyama wahamishiwa hifadhi ya Burigi

Watanzania sometimes tunapenda kulalamika bila kufanya uchunguzi na kujudge picha na video za kwenye mitandao,nilikuwa kwenye hiyo mbuga miezi miwili iliyopita na kweli kuna baadhi ya wanyama ambao ni wengi kwenye hiyo mbuga na baadhi kupunguzwa na kuhamishwa kwenye mbuga nyingine mpya,mbuga mpya imefunguliwa,wanyama wanaongezwa ili waende kuzaliana kwenye mbunga hiyo mpya .


Hayo ni maendeleo,kuna misitu mingi sana hii Tanzania na Mapori ambayo bado hazijaitwa mbuga na kuna wanyama wachache mno,,kuongeza wanyama au kuanzisha mbuga mpya ni akili nzuri sana.
Tuangalie hata baadhi ya mbuga za Africa kusini.
Serengeti ina nyumbu zaidi ya million moja na nusu,unaona wivu nyumbu kumi jinsia tofauti kukamatwa na kupelekwa kwenye mbuga mpya?swala wako wangapi mikumi?Twiga wapo wangapi?
Majibu mepesi kwa hoja ngum
 
Ndugu zangu tuwe makini tusije kuamka kesho tukasikia mlima Kilimanjaro unahamishiwa wilaya pendwa, maana hifadhi za wanyamapori zimeanza kuhamishiwa wilaya pendwa.
Katika awamu ambayo imejaa majanga ni hii.... waTz tuamke
 
Mkoa wa kagera una mapori 5 ambayo yamebadilishwa na kupewa hadhi ya hifadhi ya wanyama toka mwaka Jana. Mapori hyo ni burigi, biharamulo, kimisi. Rumanyika n.k sasa HV wanaimplant species za wanyama tofauti ili kuvutia watalii na utalii
Mkuu tupe angalau utafiti uliyofanywa kuhusu ili
 
Uwanja wa ndege wakimaifa, bandari yakisasa,JS hotel, bohari ya dawa, bank kubwa ya crdb( ingawa nasikia ishafungwa), nasasa kuhamisha wanyama kuelekea huko.

Je bajeti hii ilipitishwa na bunge?.
Bajeti hii imetoka huku
TANAPA YATENGA BILIONI 3.9 KUENDELEZA HIFADHI TANO ZILIZOPANDISHWA HADHI NA KUWA HIFADHI ZA TAIFA
 
Si bora huyo amepeleka chato, nyalandu yye aliwapeleka Ulaya.....commission akaipiga bata pamoja na ant ezekieli
 
Kwetu sisi wakaazi wa kanda ya ziwa tunampongeza sana mh prezida kutuongezea fursa
Ndugu zangu tuwe makini tusije kuamka kesho tukasikia mlima Kilimanjaro unahamishiwa wilaya pendwa, maana hifadhi za wanyamapori zimeanza kuhamishiwa wilaya pendwa.
 
Nnaomba kuuliza hivi mtu akishakua Rais au kiongozi yoyote ktk Sekta ya Umma haruhusiwi kuendeleza kwao, au kwao sio sehemu ya nchi
 
Pamoja na kwamba jiwe ni mbinafsi, ila kwa hili sioni kama ni kosa. Kwangu huu naona ni utaratibu wa kawaida kuhamisha wanyama kwenda mbuga nyingine. Kwa hili kupitia ubinafsi wake naona kapatia.
Aisee nadhani nyerere angehamishaga adi popo lkn hakuwa ivosifa sifa sifa
 
Ndugu zangu tuwe makini tusije kuamka kesho tukasikia mlima Kilimanjaro unahamishiwa wilaya pendwa, maana hifadhi za wanyamapori zimeanza kuhamishiwa wilaya pendwa.
Afadhali yake anahamisha ndani ya nchi, kutoka sehemu moja ya nchi kwenda sehemu nyingine ndani ya nchi.

Kuna wengine walipandisha Twiga ndege kwenda nje ya nchi,(Lazaro Nyalandu )ambae amehamia kwenu na ni lulu kwenu kwa sasa
 
Back
Top Bottom