Baadhi ya wanaume kiuhalisia wanatufanya tuonekane wote ni wapumbavu hapa JF

passion_amo1

JF-Expert Member
Dec 3, 2023
1,578
3,148
Wakuu habari za uzima?

Unajua Jamii forums ni ni sehemu ya kuvuna maarifa, kuburudika, na hata kutengeneza marafiki na uhusiano miongoni mwetu.

Ndugu zangu na wapendwa wote jamii forum, kuna baadhi ya mambo huenda yakawa yanachukuliwa katika hali ya utani lakini yakawa na madhara hasi pasi na mtu kulitambua hilo.

Embu Tazama mfano;
Kijana mmoja anasema, singo maza ndio wanaongoza kutoa mbususu hovyo, na pia singo maza ndio wanaongoza kujiuza kwenye madanguro?

Fikiria hii sentensi ameandika akitaka kuonyesha kwamba yupo sahihi lakini kinyume chake ni kuendelea kuvua wanaume nguo.

Kama singo maza chanzo chake kikubwa ni sisi WANAUME, mwanamke mtu kamzalisha wameshindwana labda kwa sababu mwanamke ajatulia sawa, je hayo majukumu ya mtoto wako unamuachia nani?

Huyu singo maza kila atakapoenda kutafuta kazi ataombwa rushwa ya ngono, mwanaume tayari kashakimbia na hakuna huduma yoyote anayoitoa kwa mtoto wake.

Unafikiri huyu mwanamke atafanya nini kuendelea kumpa huduma muhimu mtoto wake? Mwisho wa siku ataishia kutafuta njia za kujirahisisha ili tu aendelee kumtunza mtoto wake kwasababu tu ya mwanaume mpumbavu asiyejua kwamba kuwa mwanaume kuna ambatana na majukumu mazito.

Wanasema chizi hufurahisha anapokuwa si nduguyo, ila kama ni nduguyo hicho ni kilio. Tumuulize tu kama dada yake akamkuta katika madanguro sababu ya mwanaume ambaye alimtelekeza yeye atajisikiaje?

Kama kijana huyu sasahiv ngozi bado imenyooka, damu bado ya moto, ananyoa anapendeza akifikiri kwamba ujana utakuwepo tu basi ni kujidanganya.

Ipo siku mtoto wako wakike na yeye atakuwapo katika madanguro kwa sababu ya mwanaume mpumbavu kama wewe ambaye ulishindwa kutimiza majukumu yakiume.

Embu fikiria huu mfano;
KATAA NDOA, UMIZA MWANAMKE.

Huyu ni mtu ambaye anasema umiza mwanamke, ambaye kaja kwa kupitia kati kati ya mapaja ya mwanamke huyo!
sasa tumuulize kama amesema umiza mwanamke je mama yake aliyemzaa alishamuumiza? Hivi wanaume huwa mnajaribu kufikiri mnachoandika hapa?
Je huyu aliyesema umiza mwanamke yupo tayari kumuona mama yake akinyanyasika mbele yake na akampongeza huyo anayemnyanyasa?

Jamani ndugu zangu embu tujaribu kufikiri japo kwa uchache mambo tunayoongea, hii sehemu inafika watu wengi sana.

Tunaweza kuonekana wengi ni wapumbavu wasio na maana sababu tu ya wachache ambao wanahitaji watu wakuwaweka busy kwa kusoma maoni yao.

Kama unahitaji kuumiza mwanamke aidha kwa kihisia, hawa wanawake wasipokuwapo unafikiri tutaendelea vipi kuongezeka?

Hao watu wakufanya kazi ya kuliendeleza taifa watatoka wapi na tayari mtu anasema umiza mwanamke?

Naomba tu ndugu zangu tujaribu kufikiri tunachokiandika hata kama ID tunazotumia ni feki, embu tujitahidi tu.

Yaani kila siku wanaume tunaendelea kuvuliwa nguo sababu ya watu wachache , tunaendelea kuonekana si lolote sababu ya mambo haya!
 
Attachments

  • 92A495E1-7464-4195-A6EA-4F23948F4D04.jpeg
    92A495E1-7464-4195-A6EA-4F23948F4D04.jpeg
    43.7 KB · Views: 6
  • 4F2CC595-FFE1-42DA-99C3-46719B406C90.jpeg
    4F2CC595-FFE1-42DA-99C3-46719B406C90.jpeg
    62 KB · Views: 5
si wanataka usawa, inawashinda nini kulisha watoto
acha ujinga wewe
waelimishe hao wadada watulie walee watoto, waache mapepe
Mkuu Mtu,
Hakuna kitu ulichojibu zaidi ya ushabiki tu, ila nitakuuliza kwa muono huo.
Kama wanataka usawa kwa maana ya 50/50 kwanini wanaume wanakimbia na kuacha mzigo wa kulea mtoto wakati wote wanapaswa changia malezi ya mtoto nusu kwa nusu?

Unafahamu vyema kuhusu dhana ya 50/50 ni katika mazingira gani? Au tu umejibu kufurahisha watu?

Mkuu Mtukutu,
Nashukuru kwa mchango wako ila nilijaribu tu kusema niyaonayo.
 
Kwa nn afanye ukahaba na sio kazi nyingine ?
Maisha mangumu hayawezi kuhalalisha mtu kufanya huo uovu.

Mwanaume aliye terekeza mtoto ni mpumbavu lakini ww mwanamke utakaye anza kujiuza hovyo kwa kisingizio cha kulea mtoto ni mpumbavu zaidi.
 
Duuh! Ki jf jf hao ni wa kuwazowea tu sababu kiuhalisia sidhani kama kuna mtu anapenda kuzalishwa na kisha kuachwa.
Sio kweli maana kuna wanawake wanafuatwa na vijana wazuri wenye future watengeneze familia yao wanawakataa na kudengua ,lakini cha kushangaza anaenda kuwa hawala wa mme wa mtu tena sio mmoja sasa kama sio kujitafutia usingo maza kwa nguvu ni nn?
 
Wakuu habari za uzima?

Unajua Jamii forums ni ni sehemu ya kuvuna maarifa, kuburudika, na hata kutengeneza marafiki na uhusiano miongoni mwetu.

Ndugu zangu na wapendwa wote jamii forum, kuna baadhi ya mambo huenda yakawa yanachukuliwa katika hali ya utani lakini yakawa na madhara hasi pasi na mtu kulitambua hilo.

Embu Tazama mfano;
Kijana mmoja anasema, singo maza ndio wanaongoza kutoa mbususu hovyo, na pia singo maza ndio wanaongoza kujiuza kwenye madanguro?

Fikiria hii sentensi ameandika akitaka kuonyesha kwamba yupo sahihi lakini kinyume chake ni kuendelea kuvua wanaume nguo.

Kama singo maza chanzo chake kikubwa ni sisi WANAUME, mwanamke mtu kamzalisha wameshindwana labda kwa sababu mwanamke ajatulia sawa, je hayo majukumu ya mtoto wako unamuachia nani?

Huyu singo maza kila atakapoenda kutafuta kazi ataombwa rushwa ya ngono, mwanaume tayari kashakimbia na hakuna huduma yoyote anayoitoa kwa mtoto wake.

Unafikiri huyu mwanamke atafanya nini kuendelea kumpa huduma muhimu mtoto wake? Mwisho wa siku ataishia kutafuta njia za kujirahisisha ili tu aendelee kumtunza mtoto wake kwasababu tu ya mwanaume mpumbavu asiyejua kwamba kuwa mwanaume kuna ambatana na majukumu mazito.

Wanasema chizi hufurahisha anapokuwa si nduguyo, ila kama ni nduguyo hicho ni kilio. Tumuulize tu kama dada yake akamkuta katika madanguro sababu ya mwanaume ambaye alimtelekeza yeye atajisikiaje?

Kama kijana huyu sasahiv ngozi bado imenyooka, damu bado ya moto, ananyoa anapendeza akifikiri kwamba ujana utakuwepo tu basi ni kujidanganya.

Ipo siku mtoto wako wakike na yeye atakuwapo katika madanguro kwa sababu ya mwanaume mpumbavu kama wewe ambaye ulishindwa kutimiza majukumu yakiume.

Embu fikiria huu mfano;
KATAA NDOA, UMIZA MWANAMKE.

Huyu ni mtu ambaye anasema umiza mwanamke, ambaye kaja kwa kupitia kati kati ya mapaja ya mwanamke huyo!
sasa tumuulize kama amesema umiza mwanamke je mama yake aliyemzaa alishamuumiza? Hivi wanaume huwa mnajaribu kufikiri mnachoandika hapa?
Je huyu aliyesema umiza mwanamke yupo tayari kumuona mama yake akinyanyasika mbele yake na akampongeza huyo anayemnyanyasa?

Jamani ndugu zangu embu tujaribu kufikiri japo kwa uchache mambo tunayoongea, hii sehemu inafika watu wengi sana.

Tunaweza kuonekana wengi ni wapumbavu wasio na maana sababu tu ya wachache ambao wanahitaji watu wakuwaweka busy kwa kusoma maoni yao.

Kama unahitaji kuumiza mwanamke aidha kwa kihisia, hawa wanawake wasipokuwapo unafikiri tutaendelea vipi kuongezeka?

Hao watu wakufanya kazi ya kuliendeleza taifa watatoka wapi na tayari mtu anasema umiza mwanamke?

Naomba tu ndugu zangu tujaribu kufikiri tunachokiandika hata kama ID tunazotumia ni feki, embu tujitahidi tu.

Yaani kila siku wanaume tunaendelea kuvuliwa nguo sababu ya watu wachache , tunaendelea kuonekana si lolote sababu ya mambo haya!
Tatizo Jf na mitandao mingine imejaa watu wenye misongo ya mawazo na walio Data
 
Kwa nn afanye ukahaba na sio kazi nyingine ?
Maisha mangumu hayawezi kuhalalisha mtu kufanya huo uovu.

Mwanaume aliye terekeza mtoto ni mpumbavu lakini ww mwanamke utakaye anza kujiuza hovyo kwa kisingizio cha kulea mtoto ni mpumbavu zaidi.
Mkuu ITR,
Labda kama ni mgeni kuanzia serikalini, makampuni binafsi, ajira za watu n.k

Popote sisi wanaume huwa ni waharibifu kwa 98%. Mwanamke anahangaika kutafuta kazi na huko kote akiombwa rushwa ya ngono.
Unafikiri ana survive vipi kulea mtoto ambaye mwanaume mpumbavu kashindwa kulea hata robo ya malezi?

Mkuu ITR,
Mimi nimejaribu tu kusema kwa muono wangu unaondelea JF, ni tofauti hata na nairaland.
Nafikiri unaelewa mkuu wazazi hawa wakike changamoto wanazopitia, kuuza uji, kutembeza mboga barabarani na mtoto kichwani, na bado wanaume hawa wanaendelea kuwa abuse.
 
Kwa nn afanye ukahaba na sio kazi nyingine ?
Maisha mangumu hayawezi kuhalalisha mtu kufanya huo uovu.

Mwanaume aliye terekeza mtoto ni mpumbavu lakini ww mwanamke utakaye anza kujiuza hovyo kwa kisingizio cha kulea mtoto ni mpumbavu zaidi.
Ushawahi jiuliza kwanini ukienda kuomba kazi na mwanamke na boss akiwa mwanaume kwanini uwezekano wa wewe kidume kupata ni nadra sana
 
Uzi wako hauna research,hauna uzoefu kwasabu wew ni mwanaume kwahyo syo single mother.

Ukiuliza mwanamke yoyote ambae anajiita single mom kuhusu yeye kuishi maisha hayo atakwambia hataki kuishi kwa ratiba za saa ngapi awe home kupika na kufanya majukumu mengine kama mama wa familia na mke wa mtu.

Kiufupi hao single mothers hawapo hivyo walivyo kwasababu ya kuachwa au wanaume kukimbia majukumu ya kulea kwa mujibu wa maelezo yako,bali ni wao wenyewe na ndyo life style waliyochagua kuishi.

Ishu kubwa na inayoharibu taswira nzima ya dignity ya mwanamke kama ya single mother hukupaswa kuileta humu ndani koshabiki namna hyo na badala yake ulipaswa kuifanyia utafiti kutoka kwao wenyewe(single mothers) ili uzi wako ukae kisomi zaidi kwasababu syo kila mwanamke wa hivyo katelekezwa.
 
Back
Top Bottom