Baadhi ya wanaojiita Manabii, wachungaji wanasababisha ndoa nyingi kuvunjika

Ralphryder

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
4,933
1,294
Hao mitume na manabii, wakiwapata wanawake wenye shida za aidha uzazi, migogoro ya ndoa, au magonjwa, wanawatoa ufahamu kabisa na kuwaaminisha kwamba wao ni bora kuliko imani walizokua nazo hao wamama, kama mama alikuwa aidha mkatoliki, au kkkt au Lutheran au muislam, anabadilika na anakosa heshima hata kwa mumewe na ndoa yake anaaminishwa haikua nzuri na anaanza kufundishwa ujinga ujinga wa imani mpya mpaka ndoa zinavunjika.

Mke anakuwa kiburi, hana tena imani na dini aliyozaliwa nayo na anakuwa kama msukule kwa hao mitume na manabii , yuko radhi atekeleze maelekezo ya wachungaji hao kuliko ya mume, watu wa ustawi wa jamii fanyieni uchunguzi jambo hili, ndoa nyingi sana zinavunjika kwa sababu ya watu hao.
 
Hao mitume na manabii, wakiwapata wanawake wenye shida za aidha uzazi, migogoro ya ndoa, au magonjwa, wanawatoa ufahamu kabisa na kuwaaminisha kwamba wao ni bora kuliko imani walizokua nazo hao wamama, kama mama alikua aidha mkatoliki, au kkkt au Lutheran au muislam, anabadilika na anakosa heshima hata kwa mumewe na ndoa yake anaaminishwa haikua nzuri na anaanza kufundishwa ujinga ujinga wa imani mpya mpaka ndoa zinavunjika. Mke anakua kiburi, hana tena imani na dini aliyozaliwa nayo na anakuwa kama msukule kwa hao mitume na manabii , yuko radhi atekeleze maelekezo ya wachungaji hao kuliko ya mume, watu wa ustawi wa jamii fanyieni uchunguzi jambo hili, ndoa nyingi sana zinavunjika kwa sababu ya watu hao.
uko sahihi kabisa mkuu,, mm hili jambo limetokea kwenye familia yetu ilipelekea mpaka watoto tukagawanyika wengine kwa baba wengine kwa mama na ndio chanzo Cha mzee wangu kufariki kifo Cha mateso sana, huwa inaniumiza sana nikiikumbuka hili jambo na tokea hapo sina Imani na hawa manabii wachumia tumbo
 
Pole mkuu
 
Pepo Toka, Shidwa Na Ulegee Haraka
Haa!! Manabii, Mitume, Wafalme Wanapita Kwenye Hii Thread Wanadonya Tu
 
Wewe mleta mada sema hela huna

Unataka uheshimiwe wakati kufa

Hata ungekuwa dini moja katoliki,uislamu,KKKT nk kama lofa usingeheshimiwa usistafute visingizio tafuta hela.Heshima itarudi
 
Sio manabii tu. Ukiwa wewe mkeo ni mlokole na wewe sio mlokole, ujue mchungaji wake ni rahisi avunje ndoa yake. Kwasababu wanahesabu we ni km kikwazo ktk dini yao. Mkeo anashindwa kumtumikia mchungaji na wewe mume,, mwisho anashauriwa aachane na mume huyo alafu Mungu atakupa mume mwingine ambaye ni mlokole mwenzake. Baada ya ushauri huo utaona mkeo anabadilika tabia hasikii wala hakutii ili atafute sababu za kuachana.
 
Kila sehemu inahitaji akili,yaani za kuambiwa unachanganya na za kwako,alafu mi kinachonishangaza unaeza kuta mtu ni msomi lakini kashikwa na akili na mtu ambaye hajaenda hata shule,
 
MTU ANASALI KUANZIA JUMATATU MPAKA JUMAPILI NA NI MKE WA MTU.
MUDA WA KUHUDUMIA FAMILIA HANA, ILA ANA MUDA WA KUTOSHA KUFUA, KUOSHA VYOMBO, NA KUFANYA USAFI NYUMBANI KWA MTUME/NABII
 
Sio manabii tu. Ukiwa wewe mkeo ni mlokole na wewe sio mlokole, ujue mchungaji wake ni rahisi avunje ndoa yake. Kwasababu wanahesabu we ni km kikwazo ktk dini yao. Mkeo anashindwa kumtumikia mchungaji na wewe mume,, mwisho anashauriwa aachane na mume huyo alafu Mungu atakupa mume mwingine ambaye ni mlokole mwenzake. Baada ya ushauri huo utaona mkeo anabadilika tabia hasikii wala hakutii ili atafute sababu za kuachana.
Huu ulioleza hapa ni uongo uliopitiliza mkuu...
 
Back
Top Bottom