Baadhi ya waislam kama tumeshachanyikiwa

Baadhi ya waislam kama tumeshachanyikiwa

bikira latifah

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2016
Posts
836
Reaction score
2,805
Shehe anasema kaeni mbaali na mwaka mpya ni sherehe ya makafiri na mwaka wa makafiri ila vyeti vyake vya kuzaliwa vina mwaka wa kikafiri Tarehe anatumia za kikafiri

Waislam tukifa makaburi yetu yanaanidikwa tarehe ya kufa na siku uliyozikwa katika mfumo wa tarehe za kikafiri yaani tupo kama mandumiyakuwili[emoji23][emoji23]
 
Shehe anasema kaeni mbaali na mwaka mpya ni sherehe ya makafiri na mwaka wa makafiri ila vyeti vyake vya kuzaliwa vina mwaka wa kikafiri Tarehe anatumia za kikafiri

Tunakufa makaburi yanaanidikwa tarehe za kikafiri yaani tupo kama mandumiyakuwili[emoji23][emoji23]
Muulielze huyo shekh lao ni Tarehe ngali? Atakwambia tare 2
 
Huyo mwehu hata tamasha lake la mashindano ya kuhifadhi Qur'an tarehe inayotangazwa ni ya kikafiri.

NB:Huwezi kuwaepuka makafiri kwenye maisha ya kila siku,hiyo misikiti yenyewe ukichambua ujenzi wake ni full makafiri.
 
Shehe anasema kaeni mbaali na mwaka mpya ni sherehe ya makafiri na mwaka wa makafiri ila vyeti vyake vya kuzaliwa vina mwaka wa kikafiri Tarehe anatumia za kikafiri

Tunakufa makaburi yanaanidikwa tarehe za kikafiri yaani tupo kama mandumiyakuwili[emoji23][emoji23]
Kalenda ya Gregorian ilianzishwa mwaka 1582 na Papa Gregory XIII ili kurekebisha makosa ya kalenda ya Julian iliyoanzishwa na Julius Caesar mwaka 45 KK, kalenda hiyo ilikosea urefu halisi wa mwaka wa jua kwa takribani dakika 11 kwa mwaka. Na majina ya kalenda hii yalipewa kutokana na miungu ya kale ya Kiroma na majina ya namba za kilatini kama vile:-
Januari (January) - Asili: Janus – mungu wa Kirumi wa milango, mwanzo na mwisho
Februari (February) - Asili: Februa – sherehe ya utakaso kwa Warumi
Machi (March) - Asili: Mars – mungu wa vita wa Kirumi
Aprili (April) - Asili: Aperire (Kilatini) – kufungua
Mei (May) - Asili: Maia – mungu wa uzazi na ukuaji
Juni (June) - Asili: Juno – mungu wa ndoa na ulinzi wa wanawake
Julai (July) - Asili: Julius Caesar
Agosti (August) - Asili: Augustus Caesar
Septemba (September) - Asili: Septem (Kilatini) – saba
Oktoba (October) - Asili: Octo – nane
Novemba (November) - Asili: Novem – tisa
Desemba (December) - sili: Decem – kumi

Kwa nini kuna mkanganyiko wa namba?
Miezi Septemba–Desemba ina majina ya namba 7–10 kwa sababu, katika kalenda ya awali ya Warumi, mwaka ulianza Machi, Januari na Februari ziliongezwa baadaye.

Hata Yesu mwenyewe hajawahi tumia hizo kalenda za Julian au Gregory, bali alitumia kalenda ya Kiyahudi ambayo ni lunisolar, inafuata mwezi muandamo lakini sikukuu zao zinafuata majira (Jua).
Miezi ya kiyahudi ni :-
1 - Nisan
2 - Iyar
3 - Sivan
4 - Tammuz
5 - Av
6 - Elul
7 - Tishrei
8 - Cheshvan
9 - Kislev
10 - Tevet
11 - Shevat
12 - Adar (na Adar II)

Hii Adar II ni mwezi wa ziada kama mwaka ukiwa Leap Year.

Waislamu wao wanafuata kalenda ya mwezi (Lunar) pekee kwa ajili ya tarehe za ibada zao, kama vile hija, kufunga Ramadhaan, Eid mbili na mambo yao ya zaka.

Kalenda ya Hijria
1 - Muharram
2 - Safar
3 - Rabi‘ al-Awwal
4 - Rabi‘ al-Thani
5 - Jumada al-Ula
6 - Jumada al-Akhirah
7 - Rajab
8 - Sha‘ban
9 - Ramadhan
10 - Shawwal
11 - Dhu al-Qa‘dah
12 - Dhu al-Hijjah

Hapo unaweza kuona huyo shehe alichomaanisha hizi tarehe zimewekwa na kuasisiwa na upagani lakini tunaweza zitumia kwani aliyeumba Jua na mwezi ni Mwenyezi Mungu Muumba wa vyote na katika mzunguko wa mwezi tunapata kujua siku na kwa mzunguko wa jua huwa tunapata vipindi vya majira kwa ajili ya shughuli zetu mbalimbali za kilimo na nyinginezo. Sisi tunaweza kuita miezi kwa namba ikiwa tutaona kuna ukakasi wa hayo majina ya kigeni kama vile mwezi wa kwanza hadi mwezi wa kumi na mbili.
 
Usipozielewa Dini,zitakupa tabu sana!!

Hakuna Dini iliyokamilka coz binadamu anahusika katika mchakato wa dini kuwepo Kwa waamini na kuaminika!!

Dini nyingi ni project za umma ulio na akili zaidi ya ku manipulate wenye akili kidogo japo ni kweli IPO nguvu ya kipekee iliyopangilia uwepo was viumbe vyote iitwayo MUNGU kiswahili!ukiamini hivyo yatosha kabisa bila kuwa mfia Dini wa upande wowote na unaweza kuomba Mungu kwa lugha yoyote na Kwa namna yoyote na sio lazima ukariri vifungu Toka kwenye lugha nyingine Ili kutilia mkazo maombi yako!!

Tuwe huru kiimani coz Mungu mwenyezi Hana upande wa Dini yoyote ile! Na anasikia lugha zote na anatuonea huruma Kwa mahangaiko yetu kuhusu Imani na kuwa mateka was Imani tofauti tofauti hapa ulimwenguni!!
 
Umechanganyikiwa mwenyewe muislam hawezi kuchanganyikiwa kizembe, vyote vya mbingu na ardhi na kati kati yake ni vyake Mwenyezi Mungu
 
Back
Top Bottom