Baadhi ya waislam kama tumeshachanyikiwa

Baadhi ya waislam kama tumeshachanyikiwa

Umechanganyikiwa mwenyewe muislam hawezi kuchanganyikiwa kizembe, vyote vya mbingu na ardhi na kati kati yake ni vyake Mwenyezi Mungu
Kwahy kitimoto ni haram Ila uzinzi, mauaji, uongo na kumla mke wa ndugu yako nk ni halal?
 
Kalenda ya Gregorian ilianzishwa mwaka 1582 na Papa Gregory XIII ili kurekebisha makosa ya kalenda ya Julian iliyoanzishwa na Julius Caesar mwaka 45 KK, kalenda hiyo ilikosea urefu halisi wa mwaka wa jua kwa takribani dakika 11 kwa mwaka. Na majina ya kalenda hii yalipewa kutokana na miungu ya kale ya Kiroma na majina ya namba za kilatini kama vile:-
Januari (January) - Asili: Janus – mungu wa Kirumi wa milango, mwanzo na mwisho
Februari (February) - Asili: Februa – sherehe ya utakaso kwa Warumi
Machi (March) - Asili: Mars – mungu wa vita wa Kirumi
Aprili (April) - Asili: Aperire (Kilatini) – kufungua
Mei (May) - Asili: Maia – mungu wa uzazi na ukuaji
Juni (June) - Asili: Juno – mungu wa ndoa na ulinzi wa wanawake
Julai (July) - Asili: Julius Caesar
Agosti (August) - Asili: Augustus Caesar
Septemba (September) - Asili: Septem (Kilatini) – saba
Oktoba (October) - Asili: Octo – nane
Novemba (November) - Asili: Novem – tisa
Desemba (December) - sili: Decem – kumi

Kwa nini kuna mkanganyiko wa namba?
Miezi Septemba–Desemba ina majina ya namba 7–10 kwa sababu, katika kalenda ya awali ya Warumi, mwaka ulianza Machi, Januari na Februari ziliongezwa baadaye.

Hata Yesu mwenyewe hajawahi tumia hizo kalenda za Julian au Gregory, bali alitumia kalenda ya Kiyahudi ambayo ni lunisolar, inafuata mwezi muandamo lakini sikukuu zao zinafuata majira (Jua).
Miezi ya kiyahudi ni :-
1 - Nisan
2 - Iyar
3 - Sivan
4 - Tammuz
5 - Av
6 - Elul
7 - Tishrei
8 - Cheshvan
9 - Kislev
10 - Tevet
11 - Shevat
12 - Adar (na Adar II)

Hii Adar II ni mwezi wa ziada kama mwaka ukiwa Leap Year.

Waislamu wao wanafuata kalenda ya mwezi (Lunar) pekee kwa ajili ya tarehe za ibada zao, kama vile hija, kufunga Ramadhaan, Eid mbili na mambo yao ya zaka.

​

Kalenda ya Hijria
1 - Muharram
2 - Safar
3 - Rabi‘ al-Awwal
4 - Rabi‘ al-Thani
5 - Jumada al-Ula
6 - Jumada al-Akhirah
7 - Rajab
8 - Sha‘ban
9 - Ramadhan
10 - Shawwal
11 - Dhu al-Qa‘dah
12 - Dhu al-Hijjah

Hapo unaweza kuona huyo shehe alichomaanisha hizi tarehe zimewekwa na kuasisiwa na upagani lakini tunaweza zitumia kwani aliyeumba Jua na mwezi ni Mwenyezi Mungu Muumba wa vyote na katika mzunguko wa mwezi tunapata kujua siku na kwa mzunguko wa jua huwa tunapata vipindi vya majira kwa ajili ya shughuli zetu mbalimbali za kilimo na nyinginezo. Sisi tunaweza kuita miezi kwa namba ikiwa tutaona kuna ukakasi wa hayo majina ya kigeni kama vile mwezi wa kwanza hadi mwezi wa kumi na mbili.
Kalenda ya zamani, mwaka ulikuwa unaanza March Au April?
Navyojua mm n April, Ndo mana Kuna ile fool April Ili wale waliokuwa wanasheherekea mwaka mpya 1 April badala ya 1 January waonekane n wajinga
 
Shehe anasema kaeni mbaali na mwaka mpya ni sherehe ya makafiri na mwaka wa makafiri ila vyeti vyake vya kuzaliwa vina mwaka wa kikafiri Tarehe anatumia za kikafiri

Tunakufa makaburi yanaanidikwa tarehe za kikafiri yaani tupo kama mandumiyakuwili[emoji23][emoji23]
Usiposoma na ukakubali dini yako akusomee Sheikh au kuchukua mtandaoni ndio utapata tabu kama hizi , yote ni uchache wa elimu .

Sherehe kwa mujibu wa Uislamu ni ibada na kama ibada lazima basi uhalali wake Sherehe yeyote lazima ukute kwenye Kitabu kama hamna basi si katika Uislamu na inakuwa mbaya zaidi Sherehe zenyewe zikihusisha ibada za dini nyingine au mambo mengine haramu kama vile pombe , miziki, Fujo nk.

Nikitumia hivyo vyeti hapo Nakuwa nafanya Sherehe gani au nafanya ibada gani isiyokuwa ya Kiislamu ?

Tufanye sawa ni haramu je , Uislamu unasema nini kwenye dharura na mtu akitezwa nguvu ? mbona Nguruwe imeruhusu kula wakati wa dharura kuokoa uhai wa mtu ? Kama hauwezi kupata huduma muhimu ukiwa ndani ya nchi mpaka uwe na hivyo vyetu harafu ikiwa kidini haramu Uislamu unaelekezaje mtu akiwa katika situation kama hiyo ?
 
Shehe anasema kaeni mbaali na mwaka mpya ni sherehe ya makafiri na mwaka wa makafiri ila vyeti vyake vya kuzaliwa vina mwaka wa kikafiri Tarehe anatumia za kikafiri

Tunakufa makaburi yanaanidikwa tarehe za kikafiri yaani tupo kama mandumiyakuwili[emoji23][emoji23]

Hii ni lugha gani ??

Baadhi ya waislam kama tumeshachanyikiwa​

 
Waislam wana IQ ndogo, hawawezi kupambanua mambo kwa fikra huru
 
😄😄😄 Kila mtu atachanganyikiwa Kwa wakati wake ova.
 
Kuna muda naona baadhi ya masheikh wetu kama wana utindio wa ubongo vile
 
Hawa waliojipa utumishi wa Allah wawe wanaenda shule kwa kweli. Ona sasa hata majina yao yanatumia herufi za kikafir lakin wanatupigia kelele tukae mbali na mwaka mpya.
 
Huyo mwehu hata tamasha lake la mashindano ya kuhifadhi Qur'an tarehe inayotangazwa ni ya kikafiri.

NB:Huwezi kuwaepuka makafiri kwenye maisha ya kila siku,hiyo misikiti yenyewe ukichambua ujenzi wake ni full makafiri.
Ule msikiti wa Makkah hakuna muislam aliyeweza kubuni ile miavuli hadi wakamsilimisha kafir abuni na yule kafir wa kijeruman alivyomaliza akarudia ukafir😂😂
 
Back
Top Bottom