Baadhi ya Vitabu nilivyosoma mwaka 2021 – Zitto Kabwe

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,880
Baadhi ya Vitabu nilivyosoma mwaka 2021 – Zitto Kabwe

Mwaka 2021 nimejaaliwa kusoma vitabu 29 (2020:16, 2019:34). Nimesoma vitabu zaidi mwaka huu unaokwisha kwa sababu nilipata muda mzuri wa kutosha kusoma vitabu na majarida mbalimbali ya kitaalamu. Vile vile nimesoma ripoti nyingi za Serikali, mashirika ya kimataifa kama Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, IMF na majarida ya jumla yenye maarifa mengi kama Foreign Affairs na The Economist ambalo ninalisoma kila wiki. Vitabu kadhaa pia nimenunua na nimeshindwa kuvianza na nitavianza mapema mwaka 2022 Mungu akipenda.

Napenda kuwajulisha wasomaji wa safu hii ya kila mwaka ya #BooksIread kuwa Mwaka 2021 nimeanza kuandika kitabu kinachosimulia Maisha yangu katika Siasa za Tanzania katika kipindi miaka 15 iliyopita. Kitabu hicho kiitawacho A Transient Democracy: A Legislator reflects on Tanzanian journey towards Authoritarianism and what to do about it kinatarajiwa kuwa dukani mwaka 2022 Mungu atupe uhai, In Sha Allah.

PHOTO-2021-12-17-11-54-51.jpg

Vitabu nilivyosoma 2021

Riwaya
Mwaka 2021 nimesoma riwaya 12 na kwa hakika nimefurahi sana. Watunzi wengi ni kutoka Afrika Mashariki. Huu ni mwaka ambao pia Mtanzania-Mzanzibari Abdulrazak Gurnah alipata tuzo ya Nobeli katika fasihi. Nilikuwa nimesoma kazi za Gurnah chache kabla ya tuzo yake. Baada ya Tuzo niliamua kusoma Riwaya zake zaidi. Riwaya za Watanzania zimeendelea kuwa katika orodha zangu kwa mwaka wa tatu mfululizo sasa. Nimefurahi sana kusoma Riwaya ya kwanza katika miaka zaidi ya arobaini ya Mshindi wa Tuzo ya Nobeli katika fasihi wa kwanza kutoka Afrika Prof. Wole Soyinka. Ndio kitabu nilichofungia mwaka.

Riwaya nilizosoma Mwaka huu ni Pamoja na;
  • The First Woman: Jeniffer Nansubuga Makumbi
  • Kololo Hill: Neema Shah
  • Abyssinian Chronicles: Moses Isegawa
  • Chronicles from the Land of the Happiest People on Earth: Wole Soyinka
  • Maji Mandiga: Mohamed Hamie Rajab
  • Chochoro za Madaraka: Lello Mmassy
  • Memory of departure: A Gurnah
  • Desertion: A Gurnah
  • Admiring Silence: A Gurnah
  • The Last Gift: A Gurnah
  • AfterLives: A Gurnah
  • Uhuru Street: M.G Vassanji
Wasifu (Biographies and Autobiographies)

Viongozi wastaafu nchini wameendelea kutoa vitabu vyao na mwaka 2021 tulitunukiwa Kitabu cha Maisha ya Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kitabu chenye mafunzo mengi katika kipindi kigumu cha mageuzi ya kiuchumi na kisiasa nchini. Kwangu Mimi, Mzee Mwinyi alikuwa ni kama Deng Xiaoping wa Tanzania na zaidi kidogo ya Deng kwani angalau Deng alifanya mageuzi Mao akiwa ameshafariki. Mwinyi alifanya mageuzi Mwalimu Nyerere akiwa hai.

Vile vile nilipata nafasi ya kutembelea nchini Zambia kwa shughuli za kiuchaguzi, ambapo Rafiki yangu aligombea na kushinda Urais wa Taifa hilo. Huko niliweza kupata vitabu viwili vya viongozi wa Zambia ambao nilitamani sana kuwasoma na kuwafahamu zaidi. Nilisoma kuhusu marehemu Mzee Levy Mwanawasa, Rais wa Tatu wa Zambia na Bwana Guy Scott, Makamu wa Rais wa Zambia, mzungu. Nje ya Afrika nilipata nafasi ya kumsoma Waziri Mkuu David Cameron wa Uingereza.

Wasifu niliosoma Mwaka huu ni Pamoja na;
  • Mzee Rukhsa: Ali Hassan Mwinyi
  • Levy Mwanawasa, An Incentive for prosperity: Amos Malupenga
  • Adventures in Zambian Politics: Guy Scott
  • Revolution Will Not Be Televised: Joe Trippi
  • For the Record: David Cameron
  • Fighting Corruption Is Dangerous: Ngozi Okonjo-Iweala
  • Mwanamke Mwanamapinduzi, Biubwa A Zahor: Zuhura Yunus
Kila mwaka, nikiwa na uwezo, huwa ninasafiri nje ya Tanzania pamoja na familia kwa ajili ya kufunza watoto wetu kuhusu nchi nyingine. Mwaka huu mimi na mke wangu, Anna Bwana pamoja na watoto wetu Aaron, Wiza-Chachage, Josina-UmmKulthum (Josina Machel) na Alaa-Angelika (Alaa Salah) tulisafiri kwenda Rwanda kwa ajili ya kutembelea Genocide Memorial na kuwafunza vijana wetu kuhusu Mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini humo. Katika kuwajua zaidi Wanyarwanda, tulisoma vitabu mbalimbali kuhusu Rwanda. Vitabu nilivyosoma ni pamoja na;
  • I am not leaving: Carl Wilkens
  • Rwanda Inc.: Patricia Cristafulli na Andrea Redmount
  • Stepp’d in Blood: Andrew Wallis
  • Do Not Disturb: Michela Wrong
Nilisoma pia Mchanganyiko wa vitabu mbalimbali kama kawaida. Ni katika kuongeza maarifa na kuendelea kujifunza kutoka sehemu mbalimbali za Dunia. Eneo hili mara nyingi ni vitabu vya eneo maalumu la kujifunza ama historia au uchumi nk. Vitabu mchanganyiko mwaka huu ni pamoja na;

Vitabu Mchanganyiko
  • Rai ya Jenerali Ulimwengu: J T Ulimwengu
  • Selous, The lost sanctity: Attilio Tagalile
  • Why Comrades Go to War: Philip Roessler na Harry Verhoeven
  • White Power, the rise and fall of the National Party of South Africa: Christi Van der Westhuizen
  • Expensive Poverty: Greg Mills
  • Poverty Within Not on the skin: Erasmus Mtui
Nimeandika orodha hii mapema kabla ya mwaka kuisha kwani nimepata nafasi bila kutarajia. Jana nimepima na kukutwa na virusi vya Korona (COVID 19). Sina maumivu yoyote mpaka sasa zaidi ya mafua tu, lakini nimekutwa positive. Naomba tuendelee kuchukua tahadhari.

Nawatakia kheri katika kumaliza mwaka 2021 na kila la kheri katika mwaka 2022. Nawashawishi kupata muda wa kujisomea japo kitabu kimoja kila mwezi. Kusoma ni kurutubisha ubongo.

Tunaoweza kuandika pia tuandike. Mungu akiniweka hai nitauanza mwaka na Kitabu cha Prof. Mark Mwandosya: Regulatory Challenges in Africa, an empirical analysis. Nitakisoma kwanza kwa ujumla kupata maudhui kisha kwa utaratibu ili kujifunza maana hiki ni kitabu rejea.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Dodoma
Disemba 17, 2021
 
Sawa mkuu. Hongera,mimi ni dereva wa shirika lisilo la kiserikali,mwaka mzima nimeumaliza kwa kulenga madaraja pamoja na mshahara kidogo sana,changamoto za maisha ni kubwa zinanizidia kutokana na kipato,japo napambana kiume
 
Nakutafuta

USSR
 
Hii inatusaidia nini wanyonge ambao pesa ya mlo mmoja tu ni shida na kila siku mafuta ya kula, petroli, vifaa vya ujenzi na mahitaji mengine muhimu yanapanda bei na vipato vya watu viko palepale au vimeporomoka kutokana na kuzorota hali ya uchumi na mzunguko wa pesa, mambo mengine muwe mnapiga kimya tu.....
 
Karibu CCM kaka.....

Huku utazidi kung'aa kuliko ilivyo Sasa....

Ni ushauri tu mkuu wangu Komredi ZZK!

#Siempre CCM
 
Huyu ndio Kiongozi bana. Anatafuta maarifa katika maandishi. Sasa uliza Maria, martini, lema na wenzao watakuwa wamesoma megabites zaidi.
Martin Maranya yeye jazba tu kama Mzee wao Benson Kigailla.......

Anataka kutuletea SIASA za US kwa nchi ya wazaramo ,wakurya na wapare 🤣🤣🤣
 
Hii inatusaidia nini wanyonge ambao pesa ya mlo mmoja tu ni shida na kila siku mafuta ya kula, petroli, vifaa vya ujenzi na mahitaji mengine muhimu yanapanda bei na vipato vya watu viko palepale au vimeporomoka kutokana na kuzorota hali ya uchumi na mzunguko wa pesa, mambo mengine muwe mnapiga kimya tu.....
Basi vitabu visingeandikwa ,kuuzwa na kusomwa hadi pale hao wanyonge wote duniani watakapopata mlo mmoja na maisha nafuu.......
 
Kila mmoja akija kutangaza hapa alivyosoma itakuwa ni vurumai, yeye kama mwanasiasa aongelee na kuleta suluhisho nini kifanyike kupunguza ugumu wa maisha kwa wananchi wengi ambao wanahangaika kwa sasa, siyo kufanya cheap politics zilizojaa unafiki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom