Baadhi ya Vitabu nilivyosoma mwaka 2021 – Zitto Kabwe

Huku mitaani watu tunavitabu vingi ktk mashelves na pdf lakini huwezi kusoma kitabu Kama huko sawa mfukoni. Ndiyo maana huku mtaani being intellect haina maana bila material . Nyie endeeleni tu.
 
Ulipotaja viongozi wastaafu ukitoa Mwl Nyerere pekee hawa wengine achana nao kabisa sitaki hata kusoma wasifu wao ni watu wa hovyo sn wametuletea umaskini wa kutubwa bora hata ungesoma neno la MUNGU, kwanza wanatakiwa wanyongwe
 
Kila mmoja akija kutangaza hapa alivyosoma itakuwa ni vurumai, yeye kama mwanasiasa aongelee na kuleta suluhisho nini kifanyike kupunguza ugumu wa maisha kwa wananchi wengi ambao wanahangaika kwa sasa, siyo kufanya cheap politics zilizojaa unafiki.
Ni kosa mwanasiasa kutangaza vitabu alivyosoma?!!!

Unampangia cha kufanya?!!😳😳

Kwani ndg. Zitto hadadavui mambo mengine ya KISIASA NA KIUCHUMI ZAIDI ya kutangaza hivyo vitabu alivyovisoma?!!

Leo ametangaza kupata maambukizo ya UVIKO 19 ,je nalo pia ni kuhusu hivyo vitabu?!!!

Why are we so judgemental with grandeur delusion?!!!
 
Baadhi ya Vitabu nilivyosoma mwaka 2021 – Zitto Kabwe

Mwaka 2021 nimejaaliwa kusoma vitabu 29 (2020:16, 2019:34). Nimesoma vitabu zaidi mwaka huu unaokwisha kwa sababu nilipata muda mzuri wa kutosha kusoma vitabu na majarida mbalimbali ya kitaalamu. Vile vile nimesoma ripoti nyingi za Serikali, mashirika ya kimataifa kama Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, IMF na majarida ya jumla yenye maarifa mengi kama Foreign Affairs na The Economist ambalo ninalisoma kila wiki. Vitabu kadhaa pia nimenunua na nimeshindwa kuvianza na nitavianza mapema mwaka 2022 Mungu akipenda.

Napenda kuwajulisha wasomaji wa safu hii ya kila mwaka ya #BooksIread kuwa Mwaka 2021 nimeanza kuandika kitabu kinachosimulia Maisha yangu katika Siasa za Tanzania katika kipindi miaka 15 iliyopita. Kitabu hicho kiitawacho A Transient Democracy: A Legislator reflects on Tanzanian journey towards Authoritarianism and what to do about it kinatarajiwa kuwa dukani mwaka 2022 Mungu atupe uhai, In Sha Allah.

Vitabu nilivyosoma 2021

Riwaya
Mwaka 2021 nimesoma riwaya 12 na kwa hakika nimefurahi sana. Watunzi wengi ni kutoka Afrika Mashariki. Huu ni mwaka ambao pia Mtanzania-Mzanzibari Abdulrazak Gurnah alipata tuzo ya Nobeli katika fasihi. Nilikuwa nimesoma kazi za Gurnah chache kabla ya tuzo yake. Baada ya Tuzo niliamua kusoma Riwaya zake zaidi. Riwaya za Watanzania zimeendelea kuwa katika orodha zangu kwa mwaka wa tatu mfululizo sasa. Nimefurahi sana kusoma Riwaya ya kwanza katika miaka zaidi ya arobaini ya Mshindi wa Tuzo ya Nobeli katika fasihi wa kwanza kutoka Afrika Prof. Wole Soyinka. Ndio kitabu nilichofungia mwaka.

Riwaya nilizosoma Mwaka huu ni Pamoja na;
  • The First Woman: Jeniffer Nansubuga Makumbi
  • Kololo Hill: Neema Shah
  • Abyssinian Chronicles: Moses Isegawa
  • Chronicles from the Land of the Happiest People on Earth: Wole Soyinka
  • Maji Mandiga: Mohamed Hamie Rajab
  • Chochoro za Madaraka: Lello Mmassy
  • Memory of departure: A Gurnah
  • Desertion: A Gurnah
  • Admiring Silence: A Gurnah
  • The Last Gift: A Gurnah
  • AfterLives: A Gurnah
  • Uhuru Street: M.G Vassanji
Wasifu (Biographies and Autobiographies)

Viongozi wastaafu nchini wameendelea kutoa vitabu vyao na mwaka 2021 tulitunukiwa Kitabu cha Maisha ya Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kitabu chenye mafunzo mengi katika kipindi kigumu cha mageuzi ya kiuchumi na kisiasa nchini. Kwangu Mimi, Mzee Mwinyi alikuwa ni kama Deng Xiaoping wa Tanzania na zaidi kidogo ya Deng kwani angalau Deng alifanya mageuzi Mao akiwa ameshafariki. Mwinyi alifanya mageuzi Mwalimu Nyerere akiwa hai.

Vile vile nilipata nafasi ya kutembelea nchini Zambia kwa shughuli za kiuchaguzi, ambapo Rafiki yangu aligombea na kushinda Urais wa Taifa hilo. Huko niliweza kupata vitabu viwili vya viongozi wa Zambia ambao nilitamani sana kuwasoma na kuwafahamu zaidi. Nilisoma kuhusu marehemu Mzee Levy Mwanawasa, Rais wa Tatu wa Zambia na Bwana Guy Scott, Makamu wa Rais wa Zambia, mzungu. Nje ya Afrika nilipata nafasi ya kumsoma Waziri Mkuu David Cameron wa Uingereza.

Wasifu niliosoma Mwaka huu ni Pamoja na;
  • Mzee Rukhsa: Ali Hassan Mwinyi
  • Levy Mwanawasa, An Incentive for prosperity: Amos Malupenga
  • Adventures in Zambian Politics: Guy Scott
  • Revolution Will Not Be Televised: Joe Trippi
  • For the Record: David Cameron
  • Fighting Corruption Is Dangerous: Ngozi Okonjo-Iweala
  • Mwanamke Mwanamapinduzi, Biubwa A Zahor: Zuhura Yunus
Kila mwaka, nikiwa na uwezo, huwa ninasafiri nje ya Tanzania pamoja na familia kwa ajili ya kufunza watoto wetu kuhusu nchi nyingine. Mwaka huu mimi na mke wangu, Anna Bwana pamoja na watoto wetu Aaron, Wiza-Chachage, Josina-UmmKulthum (Josina Machel) na Alaa-Angelika (Alaa Salah) tulisafiri kwenda Rwanda kwa ajili ya kutembelea Genocide Memorial na kuwafunza vijana wetu kuhusu Mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini humo. Katika kuwajua zaidi Wanyarwanda, tulisoma vitabu mbalimbali kuhusu Rwanda. Vitabu nilivyosoma ni pamoja na;
  • I am not leaving: Carl Wilkens
  • Rwanda Inc.: Patricia Cristafulli na Andrea Redmount
  • Stepp’d in Blood: Andrew Wallis
  • Do Not Disturb: Michela Wrong
Nilisoma pia Mchanganyiko wa vitabu mbalimbali kama kawaida. Ni katika kuongeza maarifa na kuendelea kujifunza kutoka sehemu mbalimbali za Dunia. Eneo hili mara nyingi ni vitabu vya eneo maalumu la kujifunza ama historia au uchumi nk. Vitabu mchanganyiko mwaka huu ni pamoja na;

Vitabu Mchanganyiko
  • Rai ya Jenerali Ulimwengu: J T Ulimwengu
  • Selous, The lost sanctity: Attilio Tagalile
  • Why Comrades Go to War: Philip Roessler na Harry Verhoeven
  • White Power, the rise and fall of the National Party of South Africa: Christi Van der Westhuizen
  • Expensive Poverty: Greg Mills
  • Poverty Within Not on the skin: Erasmus Mtui
Nimeandika orodha hii mapema kabla ya mwaka kuisha kwani nimepata nafasi bila kutarajia. Jana nimepima na kukutwa na virusi vya Korona (COVID 19). Sina maumivu yoyote mpaka sasa zaidi ya mafua tu, lakini nimekutwa positive. Naomba tuendelee kuchukua tahadhari.

Nawatakia kheri katika kumaliza mwaka 2021 na kila la kheri katika mwaka 2022. Nawashawishi kupata muda wa kujisomea japo kitabu kimoja kila mwezi. Kusoma ni kurutubisha ubongo.

Tunaoweza kuandika pia tuandike. Mungu akiniweka hai nitauanza mwaka na Kitabu cha Prof. Mark Mwandosya: Regulatory Challenges in Africa, an empirical analysis. Nitakisoma kwanza kwa ujumla kupata maudhui kisha kwa utaratibu ili kujifunza maana hiki ni kitabu rejea.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Dodoma
Disemba 17, 2021
Rubbish!
Unajidai kusoma vitabu vingi bila kuongezeka elimu kichwani. No wonder unashinda mitandaoni ukihangaika kurudi kwenye siasa. Wewe siyo mwanazuoni, ulistahili utueleze umefanyakazi gani kwa mwaka mzima kuinua pato la familia yako. Wewe unasimulia kusoma waliyoandika wengine, ili iweje?
 
Ubarikiwe sana.
 
Ni kosa mwanasiasa kutangaza vitabu alivyosoma?!!!

Unampangia cha kufanya?!!😳😳

Kwani ndg. Zitto hadadavui mambo mengine ya KISIASA NA KIUCHUMI ZAIDI ya kutangaza hivyo vitabu alivyovisoma?!!

Leo ametangaza kupata maambukizo ya UVIKO 19 ,je nalo pia ni kuhusu hivyo vitabu?!!!

Why are we so judgemental with grandeur delusion?!!!​
Watanzania wanahangaika na hali mbovu za vipato na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu, atwambie namna hivyo vitabu alivyosoma vinaweza kuboresha hali yao ya sasa, siyo kutuorodheshea majina. Eti ametangaza kupata UVIKO, yeye ndo mtu wa kwanza kupata uviko nchi hii.......watanzania wangapi wameugua na kupona bila hata kujua walikuwa na uviko na wengine kufariki? msilete dhihaka kwenye mambo ya msingi.​
 
Nimemaliza mwaka kwa kuvunjiwa duka langu na wezi, na baada ya miezi 2 wakavunja nyumbani.

Nafurahi naumaliza mwaka nikiwa mwenye afya tele na tabasamu usoni licha ya mapito mengi.

Mungu akijaalia mwakani nitaendelea kusoma "Tumwabudu Mungu, na Biblia Takatifu" kama miaka mingine.
Amen
 
Rubbish!
Unajidai kusoma vitabu vingi bila kuongezeka elimu kichwani. No wonder unashinda mitandaoni ukihangaika kurudi kwenye siasa. Wewe siyo mwanazuoni, ulistahili utueleze umefanyakazi gani kwa mwaka mzima kuinua pato la familia yako. Wewe unasimulia kusoma waliyoandika wengine, ili iweje?
Binafsi siko ACT Wazalendo ila wewe jamaa michango yako mingi dhidi ya ndg.Zitto Kabwe huwa ni KUMSHAMBULIA in person......

Jana ulicomment kuwa ndg.Zitto ni MDINI.....anamsapoti mh.Rais SSH kwa muktadha huo.....

Ukazidi kuonesha ulivyojaa ULEVI WENU WA KIDINI kwa kudai kuwa ndg.ZZK hana hata rafiki mkristo.....totally ignorance🤣🤣

Mzee punguza ARGUMENTUM AD HOMINEM na PTSD......

#Siempre CCM!
 
Pamoja na kusoma vitabu vingi,lakini bado akili yako ilishindwa kubaini Mbowe haitaji kuombewa msamaha kwakuwa hana kosa lolote.
 
Watanzania wanahangaika na hali mbovu za vipato na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu, atwambie namna hivyo vitabu alivyosoma vinaweza kuboresha hali yao ya sasa, siyo kutuorodheshea majina. Eti ametangaza kupata UVIKO, yeye ndo mtu wa kwanza kupata uviko nchi hii.......watanzania wangapi wameugua na kupona bila hata kujua walikuwa na uviko na wengine kufariki? msilete dhihaka kwenye mambo ya msingi.​
Mosi, kumbe hoja ni kutaka atupe suluhisho la matatizo yetu lukuki kupitia hivyo vitabu basi ameanza vyema kwa kutuwekea JF list ya hivyo Vitabu ili wewe ,mimi na wengine tuvisome pia.....

ZZK ametukumbusha UMUHIMU WA KUSOMA VITABU....je ni vibaya ?!!!

Pili ,yeye ni maarufu ,anapotaja STATUS yake kuhusu UVIKO 19 anawahamasisha wafuasi wake na wengine WACHOME CHANJO DHIDI YA UVIKO 19,nalo kosa ?!!!

Lastly hebu basi nenda HATUA NDEFU ZAIDI kwa kutuwekea CONTENTS za kitabu kimoja ulichokisoma chenye utatuzi wa CHANGAMOTO zetu lukuki katika jamii......

Mkuu wangu Karibu Al Kasus kijiweni kwangu Tandale kwa Mtogole 🙏

#Siempre JMT
 
Hongera sana, mwaka huu ninesoma vitabu vingi ila huwa siorodheshi nitaanza kufanya hivyo mwakani ili niweke kumbukumbu sahihi.
 
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Dodoma
Disemba 17, 2021
Hongera sana Mwami Zitto as my Jf ID suggests, you really inspired me to love politics,economics, and leadership back in 2000s.

Hata passion ya kupenda kusoma vitabu, majarida ya taaluma, miswada, na hta kusomea uchumi ngazi ya M.A zote ni kutokana na kuwa inspired na political ideology zako za kuweka taaluma mbele.

Be blessed and have a prosperous 2022, and keep doing what you do best.
 
Baadhi ya Vitabu nilivyosoma mwaka 2021 – Zitto Kabwe

Mwaka 2021 nimejaaliwa kusoma vitabu 29 (2020:16, 2019:34). Nimesoma vitabu zaidi mwaka huu unaokwisha kwa sababu nilipata muda mzuri wa kutosha kusoma vitabu na majarida mbalimbali ya kitaalamu. Vile vile nimesoma ripoti nyingi za Serikali, mashirika ya kimataifa kama Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, IMF na majarida ya jumla yenye maarifa mengi kama Foreign Affairs na The Economist ambalo ninalisoma kila wiki. Vitabu kadhaa pia nimenunua na nimeshindwa kuvianza na nitavianza mapema mwaka 2022 Mungu akipenda.

Napenda kuwajulisha wasomaji wa safu hii ya kila mwaka ya #BooksIread kuwa Mwaka 2021 nimeanza kuandika kitabu kinachosimulia Maisha yangu katika Siasa za Tanzania katika kipindi miaka 15 iliyopita. Kitabu hicho kiitawacho A Transient Democracy: A Legislator reflects on Tanzanian journey towards Authoritarianism and what to do about it kinatarajiwa kuwa dukani mwaka 2022 Mungu atupe uhai, In Sha Allah.

Vitabu nilivyosoma 2021

Riwaya
Mwaka 2021 nimesoma riwaya 12 na kwa hakika nimefurahi sana. Watunzi wengi ni kutoka Afrika Mashariki. Huu ni mwaka ambao pia Mtanzania-Mzanzibari Abdulrazak Gurnah alipata tuzo ya Nobeli katika fasihi. Nilikuwa nimesoma kazi za Gurnah chache kabla ya tuzo yake. Baada ya Tuzo niliamua kusoma Riwaya zake zaidi. Riwaya za Watanzania zimeendelea kuwa katika orodha zangu kwa mwaka wa tatu mfululizo sasa. Nimefurahi sana kusoma Riwaya ya kwanza katika miaka zaidi ya arobaini ya Mshindi wa Tuzo ya Nobeli katika fasihi wa kwanza kutoka Afrika Prof. Wole Soyinka. Ndio kitabu nilichofungia mwaka.

Riwaya nilizosoma Mwaka huu ni Pamoja na;
  • The First Woman: Jeniffer Nansubuga Makumbi
  • Kololo Hill: Neema Shah
  • Abyssinian Chronicles: Moses Isegawa
  • Chronicles from the Land of the Happiest People on Earth: Wole Soyinka
  • Maji Mandiga: Mohamed Hamie Rajab
  • Chochoro za Madaraka: Lello Mmassy
  • Memory of departure: A Gurnah
  • Desertion: A Gurnah
  • Admiring Silence: A Gurnah
  • The Last Gift: A Gurnah
  • AfterLives: A Gurnah
  • Uhuru Street: M.G Vassanji
Wasifu (Biographies and Autobiographies)

Viongozi wastaafu nchini wameendelea kutoa vitabu vyao na mwaka 2021 tulitunukiwa Kitabu cha Maisha ya Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kitabu chenye mafunzo mengi katika kipindi kigumu cha mageuzi ya kiuchumi na kisiasa nchini. Kwangu Mimi, Mzee Mwinyi alikuwa ni kama Deng Xiaoping wa Tanzania na zaidi kidogo ya Deng kwani angalau Deng alifanya mageuzi Mao akiwa ameshafariki. Mwinyi alifanya mageuzi Mwalimu Nyerere akiwa hai.

Vile vile nilipata nafasi ya kutembelea nchini Zambia kwa shughuli za kiuchaguzi, ambapo Rafiki yangu aligombea na kushinda Urais wa Taifa hilo. Huko niliweza kupata vitabu viwili vya viongozi wa Zambia ambao nilitamani sana kuwasoma na kuwafahamu zaidi. Nilisoma kuhusu marehemu Mzee Levy Mwanawasa, Rais wa Tatu wa Zambia na Bwana Guy Scott, Makamu wa Rais wa Zambia, mzungu. Nje ya Afrika nilipata nafasi ya kumsoma Waziri Mkuu David Cameron wa Uingereza.

Wasifu niliosoma Mwaka huu ni Pamoja na;
  • Mzee Rukhsa: Ali Hassan Mwinyi
  • Levy Mwanawasa, An Incentive for prosperity: Amos Malupenga
  • Adventures in Zambian Politics: Guy Scott
  • Revolution Will Not Be Televised: Joe Trippi
  • For the Record: David Cameron
  • Fighting Corruption Is Dangerous: Ngozi Okonjo-Iweala
  • Mwanamke Mwanamapinduzi, Biubwa A Zahor: Zuhura Yunus
Kila mwaka, nikiwa na uwezo, huwa ninasafiri nje ya Tanzania pamoja na familia kwa ajili ya kufunza watoto wetu kuhusu nchi nyingine. Mwaka huu mimi na mke wangu, Anna Bwana pamoja na watoto wetu Aaron, Wiza-Chachage, Josina-UmmKulthum (Josina Machel) na Alaa-Angelika (Alaa Salah) tulisafiri kwenda Rwanda kwa ajili ya kutembelea Genocide Memorial na kuwafunza vijana wetu kuhusu Mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini humo. Katika kuwajua zaidi Wanyarwanda, tulisoma vitabu mbalimbali kuhusu Rwanda. Vitabu nilivyosoma ni pamoja na;
  • I am not leaving: Carl Wilkens
  • Rwanda Inc.: Patricia Cristafulli na Andrea Redmount
  • Stepp’d in Blood: Andrew Wallis
  • Do Not Disturb: Michela Wrong
Nilisoma pia Mchanganyiko wa vitabu mbalimbali kama kawaida. Ni katika kuongeza maarifa na kuendelea kujifunza kutoka sehemu mbalimbali za Dunia. Eneo hili mara nyingi ni vitabu vya eneo maalumu la kujifunza ama historia au uchumi nk. Vitabu mchanganyiko mwaka huu ni pamoja na;

Vitabu Mchanganyiko
  • Rai ya Jenerali Ulimwengu: J T Ulimwengu
  • Selous, The lost sanctity: Attilio Tagalile
  • Why Comrades Go to War: Philip Roessler na Harry Verhoeven
  • White Power, the rise and fall of the National Party of South Africa: Christi Van der Westhuizen
  • Expensive Poverty: Greg Mills
  • Poverty Within Not on the skin: Erasmus Mtui
Nimeandika orodha hii mapema kabla ya mwaka kuisha kwani nimepata nafasi bila kutarajia. Jana nimepima na kukutwa na virusi vya Korona (COVID 19). Sina maumivu yoyote mpaka sasa zaidi ya mafua tu, lakini nimekutwa positive. Naomba tuendelee kuchukua tahadhari.

Nawatakia kheri katika kumaliza mwaka 2021 na kila la kheri katika mwaka 2022. Nawashawishi kupata muda wa kujisomea japo kitabu kimoja kila mwezi. Kusoma ni kurutubisha ubongo.

Tunaoweza kuandika pia tuandike. Mungu akiniweka hai nitauanza mwaka na Kitabu cha Prof. Mark Mwandosya: Regulatory Challenges in Africa, an empirical analysis. Nitakisoma kwanza kwa ujumla kupata maudhui kisha kwa utaratibu ili kujifunza maana hiki ni kitabu rejea.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Dodoma
Disemba 17, 2021
Hongera sana Zitto
 
Mjengoni haupo, hivyo ni kazi yako kusoma vitabu. Ila Sina uhakika, huenda umeshajikita katika fani yako. "Politics is a dirty game"
 
Binafsi siko ACT Wazalendo ila wewe jamaa michango yako mingi dhidi ya ndg.Zitto Kabwe huwa ni KUMSHAMBULIA in person......

Jana ulicomment kuwa ndg.Zitto ni MDINI.....anamsapoti mh.Rais SSH kwa muktadha huo.....

Ukazidi kuonesha ulivyojaa ULEVI WENU WA KIDINI kwa kudai kuwa ndg.ZZK hana hata rafiki mkristo.....totally ignorance🤣🤣

Mzee punguza ARGUMENTUM AD HOMINEM na PTSD......

#Siempre CCM!
Mbona unatumia latini ya kuibia ibia? Au ndo ulisoma huko kwenye cheti cha sheria? Ukitaka kujitambua tumia syllogism kama unaifahamu. Mimi ni gwiji wa lugha hiyo boss! ukitaka tuelekezane angalia negans accipit negans. Pia angalia Debiles custodiendi sunt. Halafu angalia unavyokosea hata english yenyewe! unapoandika ".... totally ignorance.." una maana gani? Ni grammar gani hiyo? Ninyi ndo wale Lissu alisema munashindwa kuandika hukumu kule mahakama kuu?

Wewe kama unamuona Zitto analo la maana mpe support. Au kama ndo Zitto, jipe hongera. Mimi kwa usomi wangu na uelewa wangu sitaruhusu mtu mzembe apotoshe raia wa nchi kwa udhaifu wao. Si ni huyu aliyesema ndege zilizonunuliwa ni 'used' eti kwa kusoma kwenye vioo vya madirisha ya ndege. Mtu anayesoma vitabu vingi kiasi hicho anawezaje kuwa na ignorance kiasi hicho?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom