Baadhi ya MABENKI WEZI !

KakaNanii

JF-Expert Member
Sep 28, 2008
325
52
Kuna siku moja nilikwenda Banki ambayo ipo karibu sana hapa ofisi zetu zilipo eneo la Kibaha jina lake linaanzia na herufi "N". Nilikwenda kuchukua shilingi laki moja tu, kupitia dirishani yaani kwa Teller.Cha ajabu nilipokwenda siku nyingine si nikakuta eti Statement ya Account yangu inaonesha siku ile nilitoa milioni moja.


Yaani nimehangaika kumuona Bank Manager wa tawi lile lakini wapi, mpaka sasa sijapata pesa zangu. Jamani huu si wizi lakini ? Je nifanyeje kupata pesa zangu ?
 
sa si utaje tu mkuu,ilikuwa nmb au nbc? We dare to talk openly here...
 
Hili ni jukwaa la Siasa Mkuu.

Anyway, kwa kukusaidia, je una copy ya risiti uliyopewa siku ulipowithdraw hiyo laki moja?
Kama unayo hiyo ndiyo itakusaidia kupata ufumbuzi wa tatizo lako. Nadhani typing error ya teller ndiyo imesababisha hilo.
Hiyo copy itakusaidia wewe na teller kusahihisha makosa.
Aking'ang'ania kuwa ulitoa milioni na wewe umwulize iko wapi statement inayoonyesha kuwa ulitoa laki, wakati huo utakuwa na copy yako uliyotumia kutoa laki.
 
Andika barua Benki Kuu, ambatanisha kumbukumbu za transaction uliyofanya, peleka nakala kwa Chief Executive Officer wa hiyo benki! Utaona kimbembe chake.
 
nenda kwa manager wa ilo tawi,mwambie akuonyeshe iyo vocha ya siku iyo,na linganisha na statement,watakurudishia
 
Kwani unapotoa/withdraw pesa yako benki si unatakiwa upewe na balances statement ya account yako! au walau kiasi ulichotoa! au?

Tellers nao ni binadamu ..............wakati mwingine na wao hukosea....isipokuwa na wewe ulipo-withdraw pesa ulitakiwa kuwa makini........all the best though............
 
Tunza withdrawal slip yako mkubwa usitupe huo ndio usalama wako. Nenda benki ukamuone hata head of customer service, swala lako dogo sana linaweza kutatuliwa na ma ofisa wengine sio meneja.

Inawezekana siku hiyo teller alipata excess ya laki 9 wakaona uvivu kutafuta waka suspend kwenye overs and shorts. Au inawezekana pia teller alijichanganya akamu over pay mtu akawa na short ya pesa inayofanana na yako kwahiyo hakujua. Pia inawezekana teller kaona laki 9 imezidi kaibana na huo ni wizi. Beba deposit slip ukaonane na mhusika usinganganie kumuona meneja unachemsha. Ukichelewa zile records kwenye camera huwa zinajifuta zinaandika nyingine.plz wahi ukaongee nao.
 
Hii imenishtua sana kwa sababu kwa Nbc unapotoa hela ndani huwa tunajaza withdrawal sheet moja tu na inabaki kwa teller. Ukishapewa pesa unsepa! Nimestuka itabidi nijaze mbili. Uzoefu wako umenifundisha kuwa makini zaidi.
 
Unapoficha jina unamaanisha nini ? We ufahi kusahidiwa we taja tu jina la benki wamekuibia una ficha nini ? Au hela za ufisadi ?
 
Kwani unapotoa/withdraw pesa yako benki si unatakiwa upewe na balances statement ya account yako! au walau kiasi ulichotoa! au?

Tellers nao ni binadamu ..............wakati mwingine na wao hukosea....isipokuwa na wewe ulipo-withdraw pesa ulitakiwa kuwa makini........all the best though............
Ku-deposit/withdraw ni issue moja,
Request of statement ni issue ingine.
Pia hapo hakuna ubinadamu, ni wizi tu. Huyo teller mwisho wa siku alifungaje mahesabu??
Au ulishaonaga ubinadamu wa mtu kutoa laki moja kisha ikaandika ametoa alfu 10 tu??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom