Uchaguzi 2020 Baada ya Vyombo vya Habari kuminywa kutoa habari za CHADEMA, wagombea Ubunge wabuni mbinu mpya ili kuwafikia wapiga kura

Mkuu wala usinitake radhi kwani huwa sichoki kusoma mabandiko yenye pointi za msingi kama hili lako, hata liwe refu vipi. Mkuu haya mabadiliko yameanza ya kuzuia elimu ya uraia kipindi hiki Magufuli alichokuwa rais. Ni kama wananchi wameshurutishwa kuamini kuwa elimu ya uraia ni adui wa maendeleo. Taratibu kwa sasa tunaanza kwenda kwenye nchi ambayo viongozi wanafanya wanachoona ni sawa, na sio wanachoona wananchi ni sawa. Wananchi wamesadikishwa kuwa mtatuzi wa matatizo yao ni rais na wale anaowamini tu.

Kwa sasa ni ngumu kutoa elimu ya uraia bila kukutana na vyombo vyenye udhibiti kwa nia ya kudhibiti elimu gani inatolewa kwa wananchi. Ni kweli kwa sasa wananchi wanaweza wakakaa kimya, kwa huu uhuni unaofanywa na taasisi za kimamlaka dhidi ya kundi fulani wakidhani watakuwa salama, ila athari za kuwa na viongozi ambao hawako kwa ridhaa ya wananchi lazima itawarudia tu, tena sio muda mrefu kutoka sasa. Kutaanza kutoka amri za shuruti kwa wananchi, kwani hawana tena uwezo wa kuhoji, na hapo ndio kilio kitashika kasi. Unapoanza kuona kwenye kampeni burudani ndio kivutio cha mkutano na sio sera za mgombea, kuwa makini sana.
Uko sahihi kabisa ..kuna haja ya hii miaka mitano ijayo vyama vya Siasa (Tawala na upinzani) kuinvest katika public relation, natambua si Viongozi wote wanavipaji vya kuwa engage wananchi ili wa rally na ku support idea zao lakini kuna haja kubwa Sana kuwepo na harmonisation Kati ya wananchi na Viongozi wao.. lazima nchi iwe na umoja na maridhiano hata kama kuna tofauti za mitazamo. The next five years ni muhimu sana katika kutuliza roho za baadhi ya wananchi ambao wameshaonesha kila dalili ya kutoridhika na namna Mambo yanavyoenda..No one should be left behind, kama nchi inabidi tufaulu wote na ikitokea failure iwe ni yetu sote, isitokee akalaumiwa MTU au kikundi cha watu wachache tuu.. uongozi unahitaji uwe na skills za salesman na negotiation Technics za Shrewd businessman , products hapo ni Sera zako kuwashawishi wananchi waone kwamba unatenda Kwa ajili Yao wote, na wale wanaobaki na mashaka ni lazima ufanye negotiation nao ili uwapatie mbadala..ni kosa kuignore /kukebehi wachache wasiokubaliana coz wakiwa wengi ni hatari Kwa ustawi wa Taifa.
 
Mkuu hayo yatawezekana tu iwapo Magufuli hatakuwa rais wa nchi hii. Kinyume na hapo, the worst is yet to come.
 
CAG mwaka ujao ripit yenu ya fedha itaonyesha maambo mengi sana hewa.
 
MNATUKANA MEDIA HALAFU MNATEGEMEA NINI?
FB_IMG_1598816700559.jpg
 
Msimsingizie mh.Rais kwa kila Jambo mnalopitia..Mambo mengine yanawataka mfuate Sheria za nchi
Sheria zimeanza kutekelezwa kwenye muhula huu tu au? Mbaya zaidi kuna maboresho ya sheria ambayo yanaonekana yana nia mbaya kwa uhai wa vyama pinzani
 
Sheria zipo duniani kote siyo TZ tu. Hata USA huruhusiwi kutangaza matokeo kabla hayajathibitishwa na Tume ya Uchaguzi.
Nani anakudanganya wewe mpumbavu! Kwa ujinga sijui kama kuna mwana JF anayekushinda wala hata kukukaribia. Hiyo Marekani yako ni ya wapi, Mtaa wa Lumumba? Huo utaratibu ni kwa madikteta uchwara tu.
 
Ila sio fear kwa anachofanya rais wetu? Sasa hivi ukitaka kupigwa faini na TCRA we rusha vipindi vya wapinzani.
ANANICHUKIZA HAPA TU

Wapinzani hawako fare ndo maana wanadhibitiwa. Kwa sababu hawaoni chochote cha maana alichofanya Magufuli, wakati wao pia wamejaa makashifa kibao, uongo kibao, nk, lazima wadhibitiwe wasiharibu jamii yetu kwa uongo wao. Ukiwapa nafasi watakuja na uongo wa kuwachochea wananchi. Hatutaki kuzambaza chuki kwa Watanzania.
 
Back
Top Bottom