Uchaguzi 2020 Tundu Lissu asema pingamizi ya kufanya kampeni kabla ya wakati ni kelele za kupuuzwa, awananga wahariri wa Vyombo vya Habari

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,075
1,864
Muda huu Lissu anazungumza na Vyombo vya Habari nchini
Update zaidi kuwafikia
====

Mgombea Urais kupitia chama cha CHADEMA ameelezea ziara yake kwenye mikoa 16 na kufanya mikutano mikubwa na wananchi, amesema vyombo vya habari hasa televisheni hazijaona mikutano hiyo kwa hivyo haikonyeshwa mahali popote.

Lissu amesema lakini mtandaoni unaweza kuona mamia na maelfu ya watanzania wamehudhuria mikutano hiyo. Mikutano inayoonyesha kwamba watanzania wako tayari kwa mabadiliko makubwa kwenye nchi.

Lissu ameendelea kusema watu hawakwenda kumshangaa mtu aliepigwa risasi 16 bali wameenda kumuona kiongozi wanaemfahamu licha ya matatizo aliyopitia amesimama imara kutetea maslahi ya Wananchi na hawakwenda kumshanga kama alivyosema mtu ambae hajamtaja jina.

Lissu amesema Watanzania hawatakuwa tayari kufanyiwa mchezo mchezo kwani ni ujumbe uliotolewa na wananchi kwenye mikutano hiyo.

Lissu amesema anasikia kelele kelele kwamba wanafanya kampeni kabla ya wakati na watawekewa pingamizi. Amesema hayo ni makelele na kwenye sheria ya uchaguzi hamna kosa la kufanya kampeni kabla ya wakati.

Amesema neno kampeni maana yake ni kampeni baada ya kuteuliwa wagombea ambayo amefanya Magufuli kwa miaka mitano kuonyesha anavyofaa hivyo makelele yanaweza kupuuzwa.

Lissu amezungumzia ofisi ya Arusha kuchomwa moto na watu wanaodaiwa wasiojulikana ambao wao tayari wamewajua ni CCM kwani amedai ofisi hiyo imekodishwa kwa mtu ambae ana mahusiano na mgombea udiwani wa CCM na huyo mgombea amesema waliochoma ni viongozi na wanachama wa CCM kata ya Kimandolwa, Arusha Mjini na wamezipeleka polisi kutimiza wajibu kwani hawatafanya lolote.

Pia Lissu amezungumzia barua za mawakili wake ambao wamemuandikia Rais na Jaji Mkuu na kusema mwaka huu hakuna rafu ya watu wasiojulikana tena kwani dunia inatazama na hakuna kujificha. Amesema yeyote ambae atajaribu kuvuruga uchaguzi mwaka huu kutakuwa na 'consequences' ndani ya nchi na nje ya nchi.

Ameendelea kusema kuwa wanataka kushindwa kwenye sanduku la kura na ushindi wa mezani haukubaliki kwa mujibu wa sheria za Tanzania na kimataifa na wao hawatakubali.

Amesema kutakuwa na 'consequences', nchi hii ni tegemezi sana, watoto hasomeshwi bila hela za benki ya dunia na haiwezakani kwenda popote bila misaada ya nchi za nje na nchi hizo zinafuatilia uchaguzi huu kwa karibu kwelikweli.

Mwisho ameviongelea vyombo vya habari, amesema tumekuwa kichekesho cha dunia, ukifungua ITV, Star TV, Channel ten, Uhuru, Jamvi la habari na gazeti lolote mziki ni uleule, CCM CCM, Magufuli Magufuli. Amesema ukitaka uthibitisho ni coverage.

Lissu amesema waandishi waliofika anaamini wakifika wanapeleka kwa wahariri wanaoamua kitu gani kiandikwa na kirushwe. Amesema ni wahariri na Abbas ambae amekuwa mhariri mkuu katika vyombo vyote vya habari nchini.
 
Ni kutishana tu. Lissu ni Lissu hakuna cha mzungu kumsapoti.

Tumuache tu agombee kwa uhuru na haki.


Vigezo na masharti kuzingatiwa, kama hatimizi atakatwa, wote tunapitia hayo kwenye maisha yetu, tusipotimiza vigezo vilivyowekwa aidha kwa kujua au kutokujua tunakatwa, ...
 
Back
Top Bottom