Uchaguzi 2020 Baada ya Vyombo vya Habari kuminywa kutoa habari za CHADEMA, wagombea Ubunge wabuni mbinu mpya ili kuwafikia wapiga kura

Sera tunaongea tu kama sehemu ya kusherehesha, ila kiukweli wapiga kura wengi hawapigi kura kwa kujali sera, bali sababu nyingine kama mazoea, rushwa, hamasa nk. Ni asilimia chache sana wanachagua kwa sera. Na sasa hivi chini ya Magufuli, kumeibuka aina nyingine ya kupata uwakilishi kwa kupita bila kupingwa.
Kama ndio hivyo SASA naanza kuelewa ni Kwa nini vyama vingi ndivyo uchagua mgombea na kumpandikiza Kwa wananchi ili wampigie Kura...Wenye uelewa katika Siasa hasa Viongozi hawana Imani na machaguo ya wananchi au uwezo wao wa kujichagulia Viongozi Bora.
 
Kupita bila kupingwa ipo tangu siasa za vyama vingi mkuu!! Kuna uwezekano ulikuwa bado kinda ndiyo maana hujui kuwa kupita bila kupingwa ilikuwapo!

Kwa sasa chini ya Magufuli imekuwa ni fashion kwa wanaccm. Kabla ya Magufuli kuwa rais, ukiacha Magufuli mwenyewe akiwa mbunge kuhujumu uchaguzi ili apite bila kupingwa, ni wagombea wachache sana walikuwa wanapita bila kupingwa. Chaguzi karibia zote chini ya awamu hii zimetawaliwa na wagombea kupita bila kupingwa, yaani tabia binafsi ya Magufuli kupita bila kupingwa, ndio imegeuka kuwa tabia ya wanaccm wote kwenye chaguzi zote za nchi hii.
 
Ila sio fear kwa anachofanya rais wetu? Sasa hivi ukitaka kupigwa faini na TCRA we rusha vipindi vya wapinzani.
ANANICHUKIZA HAPA TU
Kama hakuna maneno ya chuki na matusi wewe rusha tu ,hakuna atakae kusumbua
 
Kwa sasa chini ya Magufuli imekuwa ni fashion kwa wanaccm. Kabla ya Magufuli kuwa rais, ukiacha Magufuli mwenyewe akiwa mbunge kuhujumu uchaguzi ili apite bila kupingwa, ni wagombea wachache sana walikuwa wanapita bila kupingwa. Chaguzi karibia zote chini ya awamu hii zimetawaliwa na wagombea kupita bila kupingwa, yaani tabia binafsi ya Magufuli kupita bila kupingwa, ndio imegeuka kuwa tabia ya wanaccm wote kwenye chaguzi zote za nchi hii.
Sema CCM kwa sasa imekubalika zaidi kuliko awamu ya nne. Huo ndiyo ukweli uliona watia nia tu walikuwa 44 elfu hivyo wagombea wazuri walikimbilia CCM. Siku za nyuma wakikosa CCM walikuwa wanakimbilia upinzani mwaka huu siyo sana. Hivyo wagombea wengi wa upinzani ni magalasha hata kujaza fomu ni shida. Angalia hapa chini
IMG-20200829-WA0038.jpg
 
Kanuni zipo wazi....! Mnatakiwa kubalance story....!

Siyo mwanasiasa anatoa tuhuma nzito na mbaya kwa mwenzake...halafu nyinyi kwanza hamuombi ushahidi wa kuzipa nguvu tuhuma hizo pili hamuendi upande wa pili wa aliyetuhumiwa kupata majibu ya tuhuma hizo....!!! Badala yake mbio mnaenda mitamboni kurusha tuhuma hizo tena kwenye " prime time"!

Hivyo, lazima mshughulikiwe msipofuata maadili yaliyowekwa wazi na Tume ya uchaguzi pamoja na TCRA.
Unafikili mimi mgeni kwenye hii awamu ya kishindo? Vyote vilenga kuua upinzani hata sisi CCM tunakwazwa na hii tabia mbaya.TUNATAKA KUSHINDANA MBIO NA MTU MWENYE MIGUU MWENZETU SIO MUMKATE MIGUU THEN MUMUITE NI MSHINDANI HALALI
 
Sema CCM kwa sasa imekubalika zaidi kuliko awamu ya nne. Huo ndiyo ukweli uliona watia nia tu walikuwa 44 elfu hivyo wagombea wazuri walikimbilia CCM. Siku za nyuma wakikosa CCM walikuwa wanakimbilia upinzani mwaka huu siyo sana. Hivyo wagombea wengi wa upinzani ni magalasha hata kujaza fomu ni shida. Angalia hapa chini
View attachment 1553483

Kwa sasa kila mtu anajua ukiwa ccm una uwezo wa kutangazwa mshindi, sio kwa sababu ccm ina nguvu au kukubalika sana, bali ni kwakuwa mwenyekiti wake anaweza kuiagiza tume ya uchaguzi imtangaze mgombea wa ccm. Achia mbali mazingira ya kuweza kupita bila kupingwa. Ni vigumu kwa sasa wagombea kutoka ccm kwenda upinzani, kwani kuwa upinzani ni kutaka kudhalilishwa na vyombo vya dola, kuhujumiwa shughuli zako za kukuingizia kipato, kutekwa na hata kuuwawa. Ni mwanaccm gani anaweza kumudu madhila hayo?
 
Kama ndio hivyo SASA naanza kuelewa ni Kwa nini vyama vingi ndivyo uchagua mgombea na kumpandikiza Kwa wananchi ili wampigie Kura...Wenye uelewa katika Siasa hasa Viongozi hawana Imani na machaguo ya wananchi au uwezo wao wa kujichagulia Viongozi Bora.

Yaani wewe ndio unajua haya leo?
 
Back
Top Bottom