Uchaguzi 2020 Lissu mnyang'anye Magufuli advantage ya vyombo vya habari vya umma na wasanii

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,092
Kiukweli kabisa bila wasanii wakubwa na vyombo vya habari vya umma leo kampeni za Magufuli zingekuwa nusu kaputi.

Kiufupi kampeni za Magufuli za mwaka 2020 ni sawasawa na kampeni za Magufuli za mwaka 2015, hotuba ni zilezile yaani hakuna jipya.

Ila Magufuli ameifanya TBC kama TV yake binafsi, inamrusha yeye tu, wala haina mpango wa kurusha wagomnea wengine wa upinzani tishio kwake kama Lissu mwenyewe.

Pamoja na TBC kumsaidia Magufuli kusikika zaidi kuliko wagombea wengine kinyume cha sheria za Uchaguzi, upendeleo huo wa kupita kiasi kwa Magufuli dhidi ya wagombea wengine pia unawafanya wananchi Waikinai hiyo TV na hivyo indirectly kuanza Kumkinai Mgombea wa CCM.

Sasa Lissu anatakiwa afanye yafuatayo ili kumuondolea Magufuli advantage ya vyombo vya umma kwake

1. Discredit TBC, ichongee sana kwa umma kwenye kila mkutano wa kampeni, yaani ishushe thamani mpaka watu waidharau

Kila chombo cha habari kinapenda kukubalika, kuheshimika na kupata watazamaji au wasikilizaji. Kwa hiyo Lissu hapa anatakiwa aishushue, ailaani TBC TV na redio yake, aichongee mbele ya wananchi, aiite haifanyi kazi kwa weledi, aeleze jinsi inavyovunja sheria za uchaguzi, aeleze jinsi ilivyo na upendeleo na awatake wananchi Waipuuze mpaka wajirekebishe. Akifanya hivi Wananchi hawatoichukulia TBC serious na kwa hivyo ile advantage ambayo Magufuli anaipata kwenye hiyo TV na redio itapunguzwa sana. Lissu kuna haja ya kuiattack TBC verbally tena kwa nguvu nyingi sana mbele ya wananchi. Wakijiona wanapoteza mtaji wa watu kwa watu kuwapuuza watajirekebisha.

2. Kwa upande wa wasanii, endelea kumpiga vijembe Magufuli kwa kuwaletea watu disko badala ya kunadi sera za kusaidia kuboresha maslahi ya wafanyakazi, kuondoa kitambulisho cha wamachinga, kuleta katiba mpya, etc.

Wasanii wana nguvu, kuna haja ya kutengeneza Meseji ya Kuponda performance za wasanii zilizopitiliza kwenye kampeni za Magufuli. Hapa meseji iwe ni kuwa uchaguzi huu ni uchaguzi wa masuala yanayogusa maisha ya wananchi, elimu yao, afya yao, ugali wao mezani, pensheni zao, siyo kuletewa watu wa kukatakata viuno majukwaani eti iwe ndiyo sera ya kuombea kura.
Wakumbushe wananchi kisa cha mwanamuziki mkubwa Bob Marley aliyekataa katakata kumuendorse mgombea yeyote wa siasa huko Jamaica miaka ya 70 kitendo kilichomjengea heshima zaidi kwa watu wa Jamaica, Sembuse hawa akina Diamond? - Ni nani kati ya hao kafikia star power ya Bob?

Elezea kwa wananchi jinsi Wasanii hawa wasivyo na maono ya kuwasaidia wao wenyewe au kuwasaidia wenzao, Eleza jinsi BASATA ilivyowatesa wasanii kwa kufungia kazi zao mbalimbali lakini leo wako busy kuitetea CCM.

Kuna haja kubwa ya kuwadiscredit hawa wasanii mbele ya umma, lengo la kuwadiscredit siyo kwamba wananchi wasiwapende la hasha, Lengo ni wananchi wasilink performance zao majukwaani na kumpigia kura Magufuli. Lengo hapa ni kudiscredit political undertone katika performance za hao wasanii majukwaani.

Naamini ikiandaliwa meseji nzuri ya kuwakaanga TBC na wasanii mbele ya wananchi mpaka wananchi wakawaona kuwa ni adui wa mabadiriko wanayoyataka, Wasanii wakishaanza kuona wananchi hawana time nao kwenye ushawishi wa kisiasa isipokuwa burudani tu, Tutakuwa tumemnyang'anya Magufuli kete mbili anazodhani zinamsaidia kisiasa!

Lissu piga spana kisawasawa hivi vitu viwili kwenye kila mkutano, Hii itasaidia sana wapiga kura kufuta ushawishi wowote waliokwishajengewa na hivi vitu viwili, lakini pia itaweka kigingi kusaidia vitu hivi visiwe effective katika siku zifuatazo za kampeni.
 
ccm wanajua fika kbs bila wasanii mikutano yao itapwelepeta, jana nimemcheki chanel 10 Mama Samia akiwa Rukwa watu kiduchu kishenzi (hakuna wasanii) kama mkutano wa udiwani!.

sasa hilo halitakiwi kutokea kwa jiwe, kumbuka tunajaribu kuaminisha kwa nguvu zote anakubalika kwa mamilioni ya watu and so atapita kwa kimbunga!!!.
 
Lissu hana hizo akili unazompa. Yeye anachojua ni kubwabwaja tu jukwaani
kuwa mkweli japo ndani ya nafsi yako...hv chukulia kwa mfano umewapa mtihani unaofanana kati ya Jiwe na TL halafu matokeo yake TL akapata division III unadhani Jiwe yeye atakuwa kapata matokeo gani hapo?!?!.

keep left kingehusika hapo!!.
 
Lisu ni sikio la kufa, kachanganyikiwa haijielewi ameona wazi hawezi kupata hata %10 ya kura zote, bora hata angegombea ubunge
 
umekwama mzee sisi tunatizama maendeleo ya nayoonekana.wewe kaa kuwa missile ja siku missile utaipata
 
Inamaana hao watu ni misikule hawaoni wanasubiri Lissu aache kunadi Sera za mkoa husika aje awanange tbc? Basi huo utakuwa ujuha.
 
Akili kubwa kama hizi utazikuta upinzani tu!
CCM utawakuta vilaza kama bia yetu na wakudadavuwa wasio na ajira kutwa kutetea mashudu ya watawala
 
Mbowe aliwaambia TBC "ondoke, nawapa dakika 3 ondoka kwenye mkutano wetu!...." leo ndio mleta mada anashtuka kuwa "habari" ni muhimili mkubwa, cheza na wanahabari kama Yesu alivyokuwa anaenda na watoza ushuru kwa taadhari!
 
Zile siku za mwanzo ambazo Mbowe aliwaattack TBC na kuwasemea mbovu iliisaidia sana kampeni za Lissu maana wananchi walikuwa wameipuuza TBC. Baada ya TBC kuona move ile ya Mbowe imewaharibia sana mbele ya umma, wakatufuta namna ya kumalizana na Mbowe ili kulinda heshima yao. Walivyopata suluhu tu Wakaendeleza mchezo wao wa upendeleo kwa ari kubwa zaidi.

Kinachotakiwa sasa ni kuwamwagia kinyesi mpaka wananchi wasiwachukulie serious kabisa na hii itapelekea kumpunguzia Jiwe advantage ya vyombo hivi
 
Lisu ni galasa tu.......anapoteza muda kutimiza matakwa ya mabwana zake wa ulaya. Watanzania hawajawa wajinga kiasi hicho kukubali kuongozwa na beberu jeusi
Wewe utakuwa umevurugwa sana kimaisha,msongo wa mawazo pambana nao huko uliko,usituletee hapa!😁
 
Kiukweli kabisa bila wasanii wakubwa na vyombo vya habari vya umma leo kampeni za Magufuli zingekuwa nusu kaputi.

Kiufupi kampeni za Magufuli za mwaka 2020 ni sawasawa na kampeni za Magufuli za mwaka 2015, hotuba ni zilezile yaani hakuna jipya.

Ila Magufuli ameifanya TBC kama TV yake binafsi, inamrusha yeye tu, wala haina mpango wa kurusha wagomnea wengine wa upinzani tishio kwake kama Lissu mwenyewe.

Pamoja na TBC kumsaidia Magufuli kusikika zaidi kuliko wagombea wengine kinyume cha sheria za Uchaguzi, upendeleo huo wa kupita kiasi kwa Magufuli dhidi ya wagombea wengine pia unawafanya wananchi Waikinai hiyo TV na hivyo indirectly kuanza Kumkinai Mgombea wa CCM.

Sasa Lissu anatakiwa afanye yafuatayo ili kumuondolea Magufuli advantage ya vyombo vya umma kwake

1. Discredit TBC, ichongee sana kwa umma kwenye kila mkutano wa kampeni, yaani ishushe thamani mpaka watu waidharau

Kila chombo cha habari kinapenda kukubalika, kuheshimika na kupata watazamaji au wasikilizaji. Kwa hiyo Lissu hapa anatakiwa aishushue, ailaani TBC TV na redio yake, aichongee mbele ya wananchi, aiite haifanyi kazi kwa weledi, aeleze jinsi inavyovunja sheria za uchaguzi, aeleze jinsi ilivyo na upendeleo na awatake wananchi Waipuuze mpaka wajirekebishe. Akifanya hivi Wananchi hawatoichukulia TBC serious na kwa hivyo ile advantage ambayo Magufuli anaipata kwenye hiyo TV na redio itapunguzwa sana. Lissu kuna haja ya kuiattack TBC verbally tena kwa nguvu nyingi sana mbele ya wananchi. Wakijiona wanapoteza mtaji wa watu kwa watu kuwapuuza watajirekebisha.

2. Kwa upande wa wasanii, endelea kumpiga vijembe Magufuli kwa kuwaletea watu disko badala ya kunadi sera za kusaidia kuboresha maslahi ya wafanyakazi, kuondoa kitambulisho cha wamachinga, kuleta katiba mpya, etc.

Wasanii wana nguvu, kuna haja ya kutengeneza Meseji ya Kuponda performance za wasanii zilizopitiliza kwenye kampeni za Magufuli. Hapa meseji iwe ni kuwa uchaguzi huu ni uchaguzi wa masuala yanayogusa maisha ya wananchi, elimu yao, afya yao, ugali wao mezani, pensheni zao, siyo kuletewa watu wa kukatakata viuno majukwaani eti iwe ndiyo sera ya kuombea kura.
Wakumbushe wananchi kisa cha mwanamuziki mkubwa Bob Marley aliyekataa katakata kumuendorse mgombea yeyote wa siasa huko Jamaica miaka ya 70 kitendo kilichomjengea heshima zaidi kwa watu wa Jamaica, Sembuse hawa akina Diamond? - Ni nani kati ya hao kafikia star power ya Bob?

Elezea kwa wananchi jinsi Wasanii hawa wasivyo na maono ya kuwasaidia wao wenyewe au kuwasaidia wenzao, Eleza jinsi BASATA ilivyowatesa wasanii kwa kufungia kazi zao mbalimbali lakini leo wako busy kuitetea CCM.

Kuna haja kubwa ya kuwadiscredit hawa wasanii mbele ya umma, lengo la kuwadiscredit siyo kwamba wananchi wasiwapende la hasha, Lengo ni wananchi wasilink performance zao majukwaani na kumpigia kura Magufuli. Lengo hapa ni kudiscredit political undertone katika performance za hao wasanii majukwaani.

Naamini ikiandaliwa meseji nzuri ya kuwakaanga TBC na wasanii mbele ya wananchi mpaka wananchi wakawaona kuwa ni adui wa mabadiriko wanayoyataka, Wasanii wakishaanza kuona wananchi hawana time nao kwenye ushawishi wa kisiasa isipokuwa burudani tu, Tutakuwa tumemnyang'anya Magufuli kete mbili anazodhani zinamsaidia kisiasa!

Lissu piga spana kisawasawa hivi vitu viwili kwenye kila mkutano, Hii itasaidia sana wapiga kura kufuta ushawishi wowote waliokwishajengewa na hivi vitu viwili, lakini pia itaweka kigingi kusaidia vitu hivi visiwe effective katika siku zifuatazo za kampeni.
TBC is so discredited to the shitty level..everybody knows that...

Wasanii are shitted on online mpaka wanatia huruma...nobody takes them serious ukiacha burudani zao....
 
Back
Top Bottom