KADCO Yakabidhi KIA Rasmi Mikononi mwa TAA

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

UWANJA WA NDEGE WA KIA SASA KUSIMAMIWA NA TAA BAADA YA KADCO KUMALIZA MUDA WAKE

Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba leo tarehe 11 Novemba, 2023 ameshuhudia Makabidhiano kati ya KADCO na TAA baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa ridhio la Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) kuendeshwa na Serikali chini ya TAA.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya PAC, Mjumbe wa Kamati ya PAC, Condester Sichalwe amesema kuwa Kamati na Bunge wamefurahishwa na hatua ya Wizara iliyochukua ya kuheshimu maelekezo ya Kamati ya PAC na Bunge kuhamisha KIA kwenda TAA kutoka KADCO

Aidha, Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa Makabidhiano ya KIA kutoka KADCO kuja TAA linafanyika baada ya agizo la Bunge na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuagiza KADCO kukabidhi KIA kije TAA baada ya KADCO kumaliza muda wake.

Makabidhiano kati ya TAA na KADCO yameshuhudiwa na Menejimenti ya KADCO, Menejimenti ya TAA, Watumishi Wizara ya Uchukuzi, Kamati ya Bunge ya PIC na PAC.
 

Attachments

  • DSC00126.jpg
    2.6 MB · Views: 9
  • DSC00422.jpg
    2.4 MB · Views: 10
  • DSC00443.jpg
    1.7 MB · Views: 8
  • DSC00416.jpg
    2.3 MB · Views: 10
  • DSC00390.jpg
    2.2 MB · Views: 8
KADCO ... The Government of Tanzania signed a 25-year Concession Agreement in July 1998 with the Kilimanjaro Airports Development Company (KADCO), which grante
 
Zama za Wapigaji hizi mkuu, Nchi iko kwenye mikono ya Matajiri na Watoto wa Mjini ukizubaa imetoka hiyo!
Waliongezewa muda wakati wa magu au mama?

Maana kila kitu siku hizi ni zama
 
KADCO ... The Government of Tanzania signed a 25-year Concession Agreement in July 1998 with the Kilimanjaro Airports Development Company (KADCO), which grante
Kwahiyo walitakiwa waondoke 2018?? Mwamba hakuona hili?
 
Back
Top Bottom