Mkoroshokigoli
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 14,593
- 5,583
kama kafariki unataka wewe ndio uwe mmewe??
sidhan kama kuna mtu ashawai muoa mamake,usitoke kwenye muktadha,kuna mahali umenijibu fresh huku umekuja kuharisha
kama kafariki unataka wewe ndio uwe mmewe??
Mimi naamini kuoa au kuolewa hakuwezi kuwa ni kutua mzigo kama una maanisha itakuwa njia ya kukimbia matatizo!teh teh teh waafrika ndio tulivyo, mambo yakiwa magumu tunakimbilia kwenye maandiko yaliyoandikwa miaka 1000 iliyopita. Lakini kwa sasa vijana (jinsia zote) wengi wanafurahia zaidi maisha ya mahusihano na wenza wao kuliko maisha ya familia zao walipotoka. Hii ni kwa sababu familia zetu nyingi zina migogoro isiyoisha, kwa hiyo kijana anapopata nafasi ya kujitegemea na kuoa ama kuolewa anakuwa ameshusha mzigo mkubwa.!!
Teh Teh umenichekesha ina maana unatingwa na shughuli kiasi cha kwamba unashindwa kukumbuka kama wazazi wako hawana sukari au chumvi?Sio wote wanawasahau mama zao.... ila maranyingi wanakua wametingwa nashughuli za hapa na pale za ubava...
Apart from the fact kwamba wamama wanashare a very special bond na watoto wao wa kiume ( just like we girls and our darlin pops).... malezi ya mtoto wa kike na wa kiume yanatofautiana pia.
Tangu tunazaliwa na kukua, binti unalelewa ili uje kuwa mke bora huko kwa mumeo, while mvulana analelewa kuja kuwa msaada wa familia ( yeye anahesabika kama ni mtoto wa nyumbani milele). Utamsikia mmama kabisa yani huyu baba angu ndo atakuja kunisaidia.
Kingine nafikiri wanawake tuna kaubinafsi fulani hivi. Vilivyo vyetu vizuri na tunavyovipenda sana hatupendi kushare kabisaa.
Haya kaka na dada mtapelekwa shule vizuri. Mungu amesaidia mmemaliza shule. Familia itashukuru kwa kuwa mmemaliza salama ila itashukuru zaidi kwa kuwa kaka akipata kazi ataanza kuisaidia familia instantly. Wewe dada hata usipopata kazi haina shida, utakuwa unaombewa tu uolewe basi. Haya kaka kapata kazi, anasaidia home vizuri, but siku akisema tu nimepata mchumba.... familia inahisi kama imepoteza baba na mtu wa kuisaidia. Na worse enough mama anahisi kama "mchumba/mke" atakuwa ndo mwanamke wa muhimu zaidi kwenye maisha ya mwanae. Ndo maana mabinti hadi tuolewe tunapitia mengi jamani, mara mama mkwe na mawifi wakukatae (God forbid), na sometimes ni bila hata ya sababu ya msingi.
Usiombe ukute ni single mother na mtoto pekee aliyenaye ndo huyo kaka, au kaka ndo mtoto wa pekee wa kiume kwao... mama anahisi kama binti/mchumba umekuja kuchukua furaha ya maisha yake. Kuna wamama wanafanya hata juu chini watoto wao wasioe kabisa. Wabaki tu kuishi nao wao
Bahati mbaya zaidi ukishaoa sasa, ole wako nyumbani waombe msaada fulani afu uwajibu wasubiri kidogo... itaonekana tu "mkewe ameshaanza kumbadilisha, kamshika akili". Lakini tunasahau kuwa mtoto wetu amekua, now ana familia yake so ana majukumu mapya. Mkewe ndo ubavu wake jamani, ingawa thamani ya mama itabaki palepale milele daima.
I think wamama inabidi tubadilike, tutambue kuwa vijana wetu wameoa, wana familia sasa hivi, majukumu yameongezeka pia so tusiwabane sana jamani, coz lazima kuna Vitu vitabadilika kidogo
.Na nyie vijana wa kiume msijisahau, manake kuna watu wakishaoa tu wanawake type za kina nanhii basi wanasahau kabisa kuwa kuna watu waliwazaa na kuwatunza kwa shida. Saidieni kwenu, mbona mabinti hatusahau kusaidia kwetu. Mtu unatanua tu huku hata mama ako umeshindwa kumjengea kakibanda. Upo na mama ako unaogopa hata kamtambulisha kwa wenzio au unapata hata msiba unaona aibu kwenda kwa wazazi wako maana hata hapaeleweki. Muache tabia hiyo
Na mabinti mnaoolewa msiwafanyie hivyo mama wa wenzenu. Ukishaolewa tu naamini mama mkwe wako ndo anakuwa mama yako. So mtreat kadri ambavyo utapenda wake wa kijana wako waje wakutreat au kadri unavyowish kumtreat mama yako mzazi. Hata kama huna uwezo wa kusaidia still unaweza ukawa unamkumbusha tu mumeo "baba nanhii unajua mama hatujamtumia hela mwezi wa pili huu". Utabarikiwa hadi ushangae ( samahani kwa huu mzalendo khaaa)
mkuu mimi niko tofauti sana, natumia sehemu kubwa kuwa karibu na wazazi kuliko hawa watu. Hadi mpenzi wangu huwa anashangaa muda mwingi naongea na mama kuliko yeye na zawadi lazima nimtumie kila nachoona kitampendeza.
Amen, na Iwe hivyo. Mbona wanawake wazuri (wake bora) wapo tu. Muombe tu Mungu akuoneshe wa kwako but na wewe umeshajiweka kuwa mume bora tayari. Kwa sababu Mungu anakupa yule wa kufanana na wewe.Dada una deserve Hilo jina, ana bahati sana aliye mume wako hata wanao wamebahatika kuwa na mama kama wewe, ni wapi nami nitapata kama wewe?
Dada una deserve Hilo jina, ana bahati sana aliye mume wako hata wanao wamebahatika kuwa na mama kama wewe, ni wapi nami nitapata kama wewe?
Amen, na Iwe hivyo. Mbona wanawake wazuri (wake bora) wapo tu. Muombe tu Mungu akuoneshe wa kwako but na wewe umeshajiweka kuwa mume bora tayari. Kwa sababu Mungu anakupa yule wa kufanana na wewe.
Mkuu si ungemuuliza tu ye mwenyewe kama yuko single au vipi..Huu uoga ndo uwa unatukosesha vitu vizuri..Embu jaribu bahati yako mkuu
Hahahaaaaa mkuu huyu dada huwa najipa perception ya kuwa she is already kwenye ndoa kutokana na post zake
Teh teh. Heaven Sent mama kuruthumu embu mtoe uoga kijana hapa..Huu ushenga mi nautaka..
Yani wewe ndo wa kuwa baba wangu wa kiroho kweli loooh... sikutaki hata bure. Ushenga hadi kwa mwanao khaaaa umenishinda tabia. Ngoja nimwambie baba kuruthumu
Teh teh. Heaven Sent mama kuruthumu embu mtoe uoga kijana hapa..Huu ushenga mi nautaka..
Hahahaaaaa fanya kazi mkuu shukrani ya mshenga tayari ishaandaliwa.
Yani wewe ndo wa kuwa baba wangu wa kiroho kweli loooh... sikutaki hata bure. Ushenga hadi kwa mwanao khaaaa umenishinda tabia. Ngoja nimwambie baba kuruthumu
Hahahah Hahaha liability mkubwa wewe . Ole wako utoe siri zanguTeh teh..Baba wa kiroho wa kidigital..Na shida zako zote ulizokuwa unaniambia nilikuwa nakurecord..