Baada ya video ya "Nikupe nini" ni muda sasa wa kutoa video ya "Ingekuwa vipi"

aka2030

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
2,630
3,578
Nmefurahi sana baada ya Mandojo na Domokaya kuamua kufanya video ya wimbo wao wa nikupe nini. Wimbo unazaidi ya miaka 19 ila bado unaishi,

Kwa kuutengenezea video leo itasaidia kuwaingizia kipato. Maana muziki wa sasa pesa, siyo mpaka kufanya tamasha tu.

Pia itawajengea kufahamika na kizazi cha sasa ambao wakati wimbo unatamba hawakuwa na ufahamu.

Shauku yangu na tamaa yangu kubwa sasa ni kuona Mbunge wa Muheza Mwana FA na yeye anaufanyia video wimbo wake wa "Ingekwa vipi" aliyomshirikisha mtunzi wa rap ya kisasa ya muda wote Tanzania Jaymoe.

Ni hilo tu!
 
Weka link ya kideo mzee baba
 
Wimbo classic sana kinachosikitisha video ya kisingeri singeri ugangstar mwingi tulitegemea kuona misuti kama yote yani uclassic furani hivi Bora wasingetoa video hawajaitendea haki
 
Kipindi kile ulikuwa gangstar kabla ya sasa kuachana nao wenyewe bado wapo maisha yale
 
Back
Top Bottom