Baada ya utata wa ndoa mpya ya Mrema, je, ni kweli ndoa zinaruhusiwa Kipindi cha Kwaresma?

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
32770b33-00b6-40ce-8911-cc10e9f54ab7.jpg


Baada ya mzee Lyatonga Mrema kufunga ndoa mpya Machi 24, 2022 mitandaoni kukaibuka maneno mengi kuwa inakuwaje mwanasiasa huyo mkongwe anafunga ndoa wakati wa kipindi cha mfumo wa Kwaresma, imebidi niingine chimbo kutafuta majibu.


MDAU WA KWANZA (KATEKISTA)
Kwanza kabisa nimewasiliana na Katekista mmoja wa Kanisa la Roma, ambaye majibu yake kwa ufupi aliniambia: “Inawezekana kufunga ndoa lakini lazima kuwe na sababu maalum, mfano mmoja wa wanandoa alipata dharura wakati wakijiandaa kufunga ndoa awali.

“Pia inaruhusiwa kufunga ndoa kama wahusika wamekaa pamoja kama mume na mke muda mrefu bila ndoa…na sababu nyingine kama hizo zile maalum.”


MDAU WA PILI
Fr Esperius amelitolea ufafanuzi huu:
“Mhe Mrema amefunga ndoa Kanisa Katoliki. Mrema amepewa kibali maalum/dispensation kutokana na afya yake.

“Kawaida ndoa wakati mwingine zinafungwa hospitalini on hospital bed kwa kigezo cha afya sakramenti ya ndoa hutolewa wakati wowote. Siyo kawaida sakramenti ya ndoa kutolewa wakati wa Kwaresma, inapotokea mtu yupo katika ukimada na ana hatari ya kuweza kupoteza maisha, basi ndoa hufungwa ili kumuepusha na vipingamizi vya huduma ya kanisa👍.”


MDAU WA TATU
Huyu hapa mdau mwingine anafafanua kuhusu suala hilo, huyu hapa msome:

JE NDOA ZINARUHUSIWA KIPINDI HIKI CHA KWARESMA?

katika mitandao ya kijamii, kumekuwa na mjadala mzito kuhusu ndoa mpya ya Mzee wetu Dkt Augustino Mrema, iliyofanyika hivi punde huko mkoani Kilimanjaro.

Watu wengi wamekuwa wakihoji sana kuwa, je ni halali kufunga ndoa wakati huu wa Kwaresma? Na wengine wameenda mbali zaidi wakisema, siku hizi dini imekuwa ni biashara tu kama biashara zingine, tena pesa imekuwa na nguvu kuhalalisha jambo fulani lionekane jema hata kama ni haramu.

Mpendwa! Hakika nimesikitika mno baada ya kuona mada hii ikishika kasi mno huko mitandaoni, na kibaya zaidi watu wasio Wakatoliki ndio wanaovumisha vitu hivyo vya uongo kuhusu imani yetu.

Ukweli ndoa ni zawadi nzuri ya ajabu na yenye nguvu, kwa kuwa Mungu alituumba kwa upendo na anataka tuudumishe uhusiano huo katika mahusiano yetu na watu wengine.

Ndoa sio uhusiano tu wa mwanaume na mwanamke, bali ni zaidi ya hayo kwa sababu Kristo ameinua ndoa na kuwa Sakramenti.

Hii inamaanisha kwamba, ndoa ni ishara inayoonekana inayomfunua Bwana Yesu na upendo wake usioonekana wala hauna mwisho.

Pia Katekisimu ya Kanisa Katoliki namba 1601 inasema, ndoa ni agano la maisha kati ya mwanaume na mwanamke, ambalo huamriwa kwa ustawi wa mwenzi na malezi ya watoto.

Baada ya kuona hayo, turudi sasa katika mada yetu kuu inayosema: Je ni halali kufunga ndoa wakati wa Kwaresma?

Jibu: Sheria za Kanisa Katoliki haijakataza mtu kufunga ndoa wakati wa Kwaresma, kwa sababu ndicho kipindi maalumu cha toba ambacho mwanadamu anaamua kwa dhati kumrudia Mungu wake kwa kuacha dhambi na kutenda yaliyo mema.

Hivyo mtu anapotaka kufunga ndoa kipindi hiki cha Kwaresma, anaruhusiwa kabisa kufunga. Maana Kanisa haliwezi kumkataza mtu asifunge ndoa ili aendelee kuishi kwenye uchumba sugu, kitu ambacho ni kinyume na Mafundisho ya Neno la Mungu linavyosema.

Kadhalika ndoa inaweza kufungwa wakati wowote ule, lakini siku ya Alhamisi kuu na Ijumaa kuu ndizo siku pekee ambazo Kanisa haimruhusu mtu kufunga ndoa. Kwa sababu ndani ya siku hizo mbili, Kanisa linakuwa na tafakari kubwa yenye huzuni kuhusu mateso na kifo cha Yesu pale Msalabani.

Kwahiyo nihitimishe kwa kusema kuwa, ndoa wakati huu wa Kwaresma zinaruhusiwa kabisa ila kinachokatazwa pale ni kwamba, pasiwepo na shamra shamra yeyote, sherehe wala vifujo vya furaha yaani ndoa inakuwa kimya kimya pasipo na makelele yeyote.

Na ndio maana watu kutaka ufahari, wanaamua kufunga ndoa zao kabla na baada ya kipindi hiki cha Kwaresma. Na siyo kwamba Kanisa linawazuia, hapana, naomba ieleweke hivyo.

...TUMSIFU YESU KRISTO... Cc@Angelus Gladson
 
Itakuwa ni kwa sababu maalum


Kwamba walikuwa wanaishi wote na Mr. hali ndo hiyo hata kusimama hawezi.

Ila kweli hujafa hujaumbika, pole mrema
 
ana hatari ya kuweza kupoteza maisha, basi ndoa hufungwa ili kumuepusha na vipingamizi vya huduma ya kanisa.”

Daah hio kauli
 
Itakuwa ni kwa sababu maalum


Kwamba walikuwa wanaishi wote na Mr. hali ndo hiyo hata kusimama hawezi.

Ila kweli hujafa hujaumbika, pole mrema
Sasa kama kusimama tu ni shida vipi huyo Abdallah kichwazi hapo chini anasimama? Tena ukizingatia Mrema ana kisukari?
 
Back
Top Bottom