Baada ya Tundu Lissu, mwingine ambaye hatawasahau Watanzania ni Bernard Membe

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
Hawa wanasiasa wawili hawatawasahau Watanzania katika maisha yao yote!

Tundu Lissu alikuja nchini na ''mkwara mzito'' aliouanzia akiwa nje ya nchi alipokuwa anatoa hotuba mara kwa mara kwa Watanzania kama vile ameshakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu!

Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, Tundu Lissu alikuwa anatoa vitisho vikali kwa kila mtu aliyejaribu kumpinga na kumkosoa! Watu wanaoifahamu vizuri nchi hii hasa watanzania wakawa wanamwangalia na kumhurumia huku wengine waliodhani kwa elimu yake anaijua vizuri Tanzania na wananchi wake wakihitimisha kwa kukubali methali isemayo ''akili nyingi huondoa maarifa''. Yaani Tundu Lissu ana akili nyingi lakini hana maarifa.

Watu wengine hawakujua kuwa kwa Watanzania ule ulikuwa ni ''mkwara mbuzi'' mpaka pale alipotangaza maandamano na baada ya kutangaza akakimbilia kwenye balozi za nchi za Ulaya kujificha.

Tukio la Tundu Lissu kukimbilia kwenye balozi za nchi za Ulaya lilihitimisha safari yake ya kuwa Rais wa Tanzania 2020 aliyekuwa amejaa ''mikwara mbuzi''.

Kwa dhana ile ile ya ''akili nyingi huondoa maarifa'', Tundu Lissu aliporudi Ubelgiji akaanza eti kuwalaumu watanzania kwa kutomuunga mkono huku akisema hawana uelewa mpana wa siasa.

Kuwalaumu watanzania ni kuonyesha jinsi ambavyo hawezi kuwasahau watanzania kwa yale walimfanyia. Hii ndio ikawa mwisho wa makelele mengi yenye mikwara mingi ambayo ilikuwa ni ''mikwara mbuzi''.

Bernard Membe naye ni mwanasiasa ambaye hatawasahau Watanzania baada ya kumpandisha juu na kumshusha haraka sana bila hata ya yeye kuelewa kinachoendelea.

Mitandao ya kijamii ilimuibua na kumpandisha juu bila ya yeye kujua kuwa wanaompandisha juu wanamfanya kama ni sehemu ya burudani ya kisiasa.

Membe alipewa majina yote ya ushujaa lakini majina ambayo alipenda kuitwa ni ''kachero mbobezi'' au ''nguli wa siasa za tanzania na kimataifa'' Kwenye mitandao ya kijamii kukaanzishwa alama ya reli (hashtag) inayosema ''Twende na Membe''! wapambe na mashabiki wakamjaza ''ujinga''.

Sifa alizokuwa anapewa kwenye mitandao ya kijamii zilimfanya akaanza kujiona ni ''invincible''.

Membe akaanza kudhani bila yeye wapinzani hawawezi ''kutoboa'' na kuingia Ikulu! Yaani yeye ndiye ''messiah'' wa wapinzani! Akaanza kutoa kejeli kwa Rais wa sasa wa Tanzania kuwa hana ''exposure'' huku akisema, "Ninataka kukabiliana na Rais aliyeko madarakani mimi peke yangu pamoja na kwamba wamenifukuza ndani ya chama''.

Akaanza kuwaambia wapinzani kama wanataka awasaidie kumtoa madarakani Rais Magufuli ni lazima kwanza waungane na kuunda kile alichokiita ''coalition'' na yeye kazi yake itakuwa kumtoa Ikulu aliyemuita ''yule mtu na kumpeleka nyumbani kwake Chato akapumzike''.

Kampeni zilipoanza, watu wenye uelewa wa mambo ya kisiasa wakajua huyu hawezi kufika mbali pale walipomuona anaingia kwenye uwanja wa kuhutubia akiwa ndani ya gari aina ya Range Rover Autobiography lakini akatumia matofali yaliyopangwa kama jukwaa kuhutubia.

Membe akiwa Mgombea Urais akatumia wiki mbili akizunguka katika kata ya Chiponda huko Lindi kama vile amekuwa mgombea Udiwani. Baada ya wiki mbili akapotea

Akaibuka Airport akidai anaenda Dubai kwenye kikao muhimu! Baada ya kurudi kutoka Dubai ikawa ndio mwisho wa ''mbio za sakafuni'' za Urais wa Tanzania!

Viongozi wa ACT-Wazalendo hawakutaka tena kumsikia au kumuona na badala yake wakahamia kwa Tundu Lissu mwenye ''mikwara mizito'' kumbe naye pia ni ''mikwara mbuzi''

Membe kwa sasa haonekani tena kwenye mitandao lakini kubwa zaidi, anaona aibu hata kuonekana mitaani

Huu pia ndio ukawa mwisho wa Bernard Membe kama ''Kachero Mbobezi'' asiyejitambua ambaye nadhani hata kurudi CCM anaona aibu kwa jinsi ambavyo alikuwa anawabeza
 
Haahaa membe ni kachero aliyemteka zitto kijanja Sana, mzee wa dk 89.Lissu tungekuwa na tume huru leo tungesema mengine, Kuna sehemu kijijini jamaa alizidiwa na jpm kura 5, jamaa wakabidi wampe 5 hizohizo lissu sasa
Tundu Lissu na Bernard Membe hawatawasahau Watanzania!

Tundu Lissu alisema akiibiwa kura atawaingiza wananchi barabarani na hatakubali kuibiwa kura!
 
Lissu kukaa Ulaya kulimzuzua akajiona yeye na kingereza chake anajua sana kuliko Watanzania wengine yeye kazi yake ikawa kutukana Rais, kutukana Bunge, kutukana Polisi, kutukana majaji ohh hawajui kingereza, tukana tume n.k.

Tusi la mwisho alilitoa alipofika Ubelgiji akatukana Watanzania kuwa hawako tayari kwa mabadiliko!!!! baada ya kumuonyesha cha mtema kuni sanduku la kura.

Sasa hivi akikumbukia uchaguzi Tanzania lazima BP itakuwa inampanda.
 
Tundu Lissu na Bernard Membe hawatawasahau Watanzania!

Tundu Lissu alisema akiibiwa kura atawaingiza wananchi barabarani na hatakubali kuibiwa kura!
Haahaa hili la barabarani kafeli, limebaki la kutokubali kuibiwa.Kuingizwa barabarani na wapinzani siwezi kuingia, mwisho wa siku wanatulizwa na vyeo ili wapige marupurupu Kama alivyofanya babu seif hapana
 
Alimhadaa Maalim kuwa watazuia majeshi toka Tanganyika yasiende Zanzibar hivyo maalim atashinda safari hii.
Haahaa Maalim kaona isiwe shida, kama huwezi mshinda ungana naye. Anajilia vitamu tu kwa kisingizio cha maridhiano. Mbaya zaidi kwenye hayo maridhiano wamekubaliana nini?
 
Tatizo aliwaona Watanzania kama wajinga walipokuwa wanamshangilia akadhani ameshakuwa Rais wa Tanzania kwa kudhani akiwaambia lolote watafanya!
 
Back
Top Bottom