Baada ya RC Makonda kutoa saa 24 kwa Wabunge walioko Dar: Jeshi la Polisi lawataka Wabunge walioko Dar kuripoti Kituoni

Ngoja tuone nani ataenda. Wabunge wengi wa CCM na mawaziri wapo mjini wakizunguka tu. Polisi hawana mamlaka ya kumsummon mtu kwa matamko tu ya kisiasa as long as mtu hajavunja sheria yoyote. Mtu wa kudeal na Wabunge ni Speaker na tayari keshatoa maaizo ya kwamba hawa watu warudishe fedha za posho walizolipwa kabla hawajaamua kuji-isolate
Subiri kidogo utaelewa tuu.
 
Chadema tuliwaonya humu jamii forum

Tukatukanwa kila aina ya Matusi,matusi ya chadema huniharibia mudi ya kuchangia

Na utaharibikiwa sana ikiwa utaendelea kuwa huna tabia ya kujipa nafasi ya kufikiri.
TULIA na ujiulize; Kwani kuna kitu gani hapo?

Ninachokiona ni kuwa: hao mapolisi ni watu wanaolinda matumbo yao tu. Wakubwa baada ya kuchanganyikiwa wanashindana kutunga na kutoa amri kichekesho.
Mara

- Wasilipwe, wakati mnasema waliishalipwa kabla hata hawajaomba.
- Warudishe pesa mlangoni au hawataingia,sasa mnawaita wa nini?
- Sijui wakapimwe corona kwanza; kumbe nayo ni adhabu? Au ndio maana Ndugai alikataa wabunge wa CCM wasipimwe.

Naona hata Mzee wa kujificha KWAO hataki kupimwa, pengine ndio maana wanashindana kulazimisha eti wapimaji na maabara/kipimo ionekane havifai.

Uzuri wake, kwenye kitabu cha Daniel enzi za Nebuchadnezzar, Mfalme wa Babylon, wakati wanafungua mlango wa tanuri ili kuwasukumiza Shadrach, Meshach, na Abednego, kwenye tanuli la moto; moto uliyotoka uliwalamba na kuwaua kwanza askari wao 12.

Kwa kasi hii ya wakubwa, ninaiona karibu hii inatokea. AMEN
 
Kwa mambo haya ya hovyo!! Kunaumuhimu mkubwa kumchagua Lissu mtaalamu wa sheria kuwa rais. Tuachane na mapapai, mafenesi na mbuzi beberu wa Chato.
 
Back
Top Bottom