Baada ya RC Makonda kutoa saa 24 kwa Wabunge walioko Dar: Jeshi la Polisi lawataka Wabunge walioko Dar kuripoti Kituoni

Ukihangaikia ujinga huwezi kushughulikia ya maana, huu mwezi wa toba embu tuache uovu kidogo tufanye ya maana tuheshimu mfungo wa wenzetu waislam
 
Waraka wa kuwaita machangu umetoka??

Wasidhanie tutasahau kuulizia takwimu sahihi za COVID-19...

Everyday is Saturday....................... :cool:
 
Sio utani watawakamata tu,Hii siyo Bongo movie ni katika juhudi za kuunga Makonda kwa mwendo wa fang fang.
 
Nchi hii tunasoma nakuajiriwa kwa kutumia vyeti ila ni bora tuweke vyeti vyetu kapuni na kuanza kuajiri kwa kuzingatia urefu, uwezo wa kukimbia, uwezo wa kuongea na sifa nyingine zinazohitaji mwonekano wa nje.

Haiwezekani kila mtu akiamka asubuhi anataka apange Nani awe wapi na awe sehemu gani kwa kuzingatia anavyotamani yeye. Leo sikutegemea kuona barua isiyo na kifungu chochote Cha sheria iliyovunjwa ikiandikwa na jeshi la polisi Tena ikisainiwa na kiongozi mwandamizi kabisa.
Tunasimamia sheria gani na imeandikwa wapi kwamba RC anaweza kufukuza watu kwenye mkoa wake kwa sababu anazojua yeye?

Kifo mnakijua? Watu wanakimbia kifo ninyi mnawalazimisha wafe kweli? Jitafakarini, mishahara na utu ni kipi Bora? Jifunzeni kwa wanaoanguka kila kukicha Tena wakiwa na siha njema kabisa, maisha haya tunapita tu
 
1588859097495.png


#HABARI Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema kuwa baada ya Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda kutoa saa 24 kwa Wabunge walioko jijini humo kurejea Bungeni, limewataka wale ambao bado hawajaondoka, kuripoti kwa hiyari yao katika ofisi ya Upelelezi, Kanda Maalum kwa ajili ya mahojiano./https://bit.ly/3dnBbIs
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar, limesema baada ya RC Makonda kutoa saa 24 kwa Wabunge walioko jijini humo kurejea Bungeni, limewataka wale ambao bado hawajaondoka, kuripoti kwa hiyari yao katika ofisi ya Upelelezi, Kanda Maalum kwa mahojiano

View attachment 1442715


Tanzania nchi ya ajabu sana msije mkashangaa kwanini watu hawaheshimu vyombo vya sheria. Huwezi kumlazimisha mbunge kwenda bungeni kama ana hofia afya yake kisheria. Pili Spika ameshatoa maelezo ya posho ndiyo boss wao sio mkuu wa mkoa
 
Back
Top Bottom