Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

"Mwanangu Endelea kupambana"

Hii line ni fupi sana lakini ina maana nyingi ndani yake,inaumiza,inasikitisha na inaliza pia. Leo nilikua napitia uzi wako flani jooohs kati kati ndio nikakuta link ya huu uzi wako,nikau click naangalia ni wa lini naona eti ni uzi wa APRIL nimeshangaa sana.

imekuaje sijaona uzi kama huu uliochangiwa mpk kufika page ya 64,yani ni sawa na member wa JF aseme haujui uzi wa mshanar ule wa snap it,show it au uzi wa kula tunda kimasihara hizo ni nyuzi ambazo huwezi kuwa member wa JF usizijue.

mimi leo ndio naona huu uzi nimesoma page kwa page nimejifunza mengi sana,unajua duniani bado kuna mapya mengi hatujayasikia namimi leo kuna mapya nilikua sijawahi yasikia ila nmeyasoma toka kwa muhusika kbsa,Asante kwa somo hili.

Jooohs "Mwanangu Endelea kupambana" usisahau kauli hii ya huyu rafiki yako ikawe chachu ya wewe kuinuka hata utakapoona umedondoka kabisa usichoke kupambana,kila mtu ana verse/line ambayo hatokaa aisahau ktk maisha yake iliyotoka kwa mtu anaemjua/mpenda/rafiki/mzazi/ndugu,nk

Mimi nakumbuka baada ya kuchokwa na ndugu/marafiki kwasababu ya tabia yangu ya kuomba hela wanisaidie,kuna kaka mmoja (si ndugu yangu) ni mkubwa kwangu nilimzoea kiasi huwa nilikua nikiomba hela kwa ndugu wote wakininyima yeye huwa ndio mtu wa mwisho mimi kumuomba,na alikua akinipa kweli.

siku 1 Baada ya kuchoka ile omba omba hela kwa ndugu nikaamua kwenda tafuta maisha,nikiwa njiani nikasema acha niombe ndugu na jamaa hela mara ya mwisho maana najua ndio sitokuja waomba tena na tena,kama ilivyo kawaida wote walinichomolea,Nikawa na mtu wa mwisho ambaae n yule kaka alikua akiitwa Thomas (tom) nikampgia simu Tom nikamwambia naomba nisaidie hela kidogo nimeamua kwenda tafuta maisha nimefika hapa sina pakulala wala sijala hadi saivi.

Akanipgia simu akaongea sana na ktk ongea yake alinieleza kwa kifupi historia ya maisha yake mpk pale alipo namwsho akaniambia line ambayo sitokaa niisahau hadi leo hiii

"Mdogo wangu Huko ulipo upo katika mkoa wa watu,hamna anaekujua ACHA AIBU fanya kazi yeyote ile inayokuja mbele yako ila tu Usiibe cha mtu/usiwe mwizi"

leo
sina hela kwenye simu nina 10,000 tu ila nitakutumia mdogo wangu uanzie maisha,TOM alinitumia sh.9000 kwenye simu baada ya pale akaniambia Ukabarikiwe mdogo wangu. akaniaga.

ile kauli yake imekua kama muhuri ktk maisha yangu,sijawahi isahau kila ninapoikumbuka Nimefanya kazi za ajabu sana mimi ktk haya maisha na yote ni kwasababu ya ile kauli ya TOM haikuwahi futika na haitofutika.

Jooohs kauli ya rafiki ako imebeba ujumbe mwingi ndani yake,si rahisi kuielewa lakini kama si zile kelele pale kwenye nyavu wakati umeenda msalimia mngepata kuongea angekwambia mengi sana sana lkn aliamua kufupisha yote na akayaweka yote aliyotaka kukwambia ile siku ktk line 1 tu.

"Mwanangu Endelea Kupambana"


Usimuangushe narudia tena

Usimuangushe Augustino..
Daa shukrani sana mkuu, kwa maneno yenye kutia moyo na faraja, mungu pia akujaalie kwenye malengo yako
 
Wakati mwingine unafika kipindi kigumu mpaka unaona mbele kote ni Giza tu, mpaka Leo nikimwona mtu anatembelea gari Kali nyumba na biashara iliyonona huwa namwogopa kabla ya kumheshimu, kwenye maisha kama huna roho ngumu hutoboi. Pole kiongozi wewe ni zaidi ya kamanda
Achana na hawa wa ajiriwa. Ukiona mfanyabiashara biashara amesimama kabisa na maendeleo ya kutisha, muogope sana asee, sii jambo rahisi rahisi
 
Achana na hawa wa ajiriwa. Ukiona mfanyabiashara biashara amesimama kabisa na maendeleo ya kutisha, muogope sana asee, sii jambo rahisi rahisi
Safi kwa story kuna la kujifunza hapa. Lakini story ni completely fiction story.
Bila shaka wewe ni tajiri tayari nenda pale Global Publishers upige mzingo
 
Back
Top Bottom