Baada ya Mkopo wa NSSF,Kiwanda cha Biotech bado kuanza kazi

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
14,594
5,568
Habari wadau,
Takriban mwezi mmoja nyuma,vyombo vya habari vilipata kuripot kuwa Kiwanda cha Biotech cha Kibaha kimeweza kupatiwa mkopo mnono na NSSF kwa ajili ya kukiwezesha kifanye kazi.Pia siku chache baadae Mama Jenista alinukuliwa akisema kuwa NSSF wamewakopa NDC ili kuwezesha utendaji wa Kiwanda hicho. Bado kiwanda hakijaanza kazi.
Tunataraj kuona kiwanda hiki kinaanza kazi ili walau serikali ikiulizwa iseme ndio "serikali hii ya viwanda na kiwanda cha kwanza ni cha Biotech".Ila kwa NDC hii ya sasa basi viwanda tutaendelea kuviona kwenye T.V. Mheshimiwa raisi ni lazima afanye marekebisho kwenye menejiment ya NDC ambayo itakuwa na uwezo wa kuumiza vichwa na kubuni miradi ya viwanda kwa ajili ya kwenda na kasi ya ya kauli mbiu ya "SERIKALI YA VIWANDA".
 
Mkuu wewe bado unaamini hizo hadithi za "Tanzania ya Viwanda" ?
Huo ni upepo tu, utapita kama ilivyopita MKUKUTA, MKURABITA, Kilimo Kwanza nk.

Wewe ukishaona Mhindi na Mchaga wanabadilisha Viwanda vyao kuwa Magodaoni ya kuhifadhia bidhaa kutoka nje basi ujue biashara ya viwanda ni pasua kichwa.

Mo Dewji, Bakhresa na Mengi labda wao tu ndio wanaweza biashara ya viwanda tena viwanda vya Vinywaji na chakula, kamwe serikali haiwezi huo mtiti wa viwanda hapa Tz.
 
Mdau,serikali imetuhakikishia viwanda ndo maana tunavisubiri,serikali hii ikiahidi inatimiza
 
Back
Top Bottom