UNYANYASAJI: Wafanyakazi wa Kiwanda cha Tanzania Biotech Products Limited (TBPL), hawajalipwa Mshahara miezi mitano

Anonymous

Senior Member
Feb 3, 2006
125
321
WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA VIUADUDU WA KUTOKOMEZA VILUILUI WA MBU, WALALAMIKA KUKOSA MISHAHARA KWA TAKRIBANI MIEZI MITANO SASA.

Wafanyakazi wa Kiwanda cha kutengenze viuadudu(biolarvicide) kwa ajili ya kuangamiza viluilui wa mbu kilichopo Kibaha mkoani Pwani na kinachomilikiwa na serikali kwa 100% chini ya shirika la maendeleo la Taifa (NDC) Wamelalamika kwamba hawajalipwa mishahara kwa takribani miez 5 sasa hali inayopelekea baadhi ya wafanyakazi (Wataalam) ikiwemo wa kigeni kutoka nchini Cuba kuanza kuondoka

Wamedai Suala hili la kukosa mishahara limekuwa likijirudia kila mara kwa kiwanda hiki kutokana na usimamizi usioridhisha kutoka shirika mama ambalo ni NDC kwani ndo waliopewa dhamana ya kusimamia kiwanda hiki.

Wameiomba Serikali kuingilia kati kwani maagizo na maelekezo ambayo yamekuwa yakitolewa na viongozi wakubwa (Rais na Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao kwa nyakati tofauti walipotembelea kiwandani hapo) hayatekelezwi na waliopewa dhamana hiyo.

Wamedai Wafanyakazi wapo katika hali mbaya kimaisha.
 
Poleni sana uzeni hizo dawa halafu mbona hatuoni huku mltaani sisi tunakutana na madawa ya Kichina kwani nyie masoko hamna.
 
Poleni sana.

Hicho kiwanda huwa nahisi hakifanyi kazi maana sioni pilikapilika zinazoendelea hata gari kuingia au kutoka kumbe kimekumbwa na masaibu haya
 
Hiko kiwanda hakina faida yoyote kwa wananchi. Ndio kishafungwa hivo. Mjiongeze.
 
Kawida inakuwa hivi

Watu wauzalishaji wazalishe bidhaa inayouzika na wa masoko wauze kitu kilichozalishwa.

Hapo watapata hela ya kuweze kuendesha kampuni

Pamoja na kulipana mishahara.

Wakishindwa watu wa masoko na mauzo tupo watuite
 
Back
Top Bottom