Baada ya Miaka 2, natamani Ndoa yangu ivunjike

Hiyo siri nimekumegea tunajua ya kwenye chakula mmegundua😁😁😁
Aiseee asante sana sasa ntajuaje na kujinasuaje kwenye huu mtego wa kwenye mbosousou embu nielezee kidg bibie mambo yasije kuwa mengi 😄
 
Kujinasua we baki njia kuu vinginevyo Mwanamke hana historia ya kushindwa toka enzi za Adam na Hawa hasa akitaka jambo lake 😁😁
 
Daah tangu naanza mahusiano sijawahi kufumania au kuonyeshewa kwamba mtu ana cheat na naomba Mungu isinitoke nikajua bora afanye kimyakimya Maana nahisi Kama inauma vile
Ndoa yko bdo mbichi ikikomaa utanielewa
 
The bottom line is mpenzi/mke/ mume anayecheat tena severally huwa HASAMEHEWI!!!....regardless ukiondoka atapata mwingine au la....kwani ulivyomkuta wewe ulikuwa wa kwanza??...kutunzwa sio hoja, akikuambukiza ukafa nani atakutunza huko kaburini?? nani atatunza wanao????...........
Wewe Mungu ameshakusamehe mara ngapi? Mara ngapi umemkosea Mungu na kila unapomwomba msamaha yeye husamehe!! Vinginevyo angekubania oxygen yake saa hii ingeshakuwa historia!! Kusamehe ni muhimu!!
 
Pole sana shoo. Tabia ya ulevi inakera sana hasa hasa Kwa wanaume. Ukiwaambia wanakua wakali kama pilipili. Mimi wangu ni mlevi pro max!

Hebu fikiria inajiogelesha ili mfurahie chakula Cha usiku halafu jitu linarudi saa Saba. Ananuka pombe na mzigo anataka! Keroo kerooo! Basi tu tunavumilia ili watoto wasitange tange.
Duh aisee mnavumilia
 
Natamani kuvunja ndoa yangu.

Habari zenu wakuu, natumai mko poa. Nimekuja na nia ya dhati kutafuta ushauri kuhusu jambo langu ambalo linanitatiza.

Mimi ni msichana mwenye umri chini ya miaka 30. Nina mtoto mmoja wa kiume. Nimekuwa katika ndoa na mume wangu kwa takriban miaka miwili sasa.

Sababu za maamuzi yangu ni kama ifuatavyo:

1. Uchepukaji uliokithiri: Huyu mume wangu amekuwa akinihadaa sana. Sijawahi kuona kitu kilichoniumiza zaidi ya kugundua kuwa anatoka na wanawake wengine. Ameomba msamaha kila mara ninapomfumania, lakini bado anarudia tabia hiyo. Kesi zetu zimekuwa nyingi kwa wazazi na nadhani wamechoka kutusuluhisha.

2. Ulevi uliopitiliza: Mume wangu ni mlevi sana. Kurudi nyumbani asubuhi ni jambo la kawaida kwake. Nimeshazungumza naye na kumweleza jinsi ninavyojisikia kuhusu tabia yake ya kunywa kupindukia, ingawa anahudumia familia vizuri. Lakini, hupati muda na familia kabisa. Inanidhalilisha sana kwa sababu tunakaa na mdogo wake nyumbani, hivyo najihisi vibaya sana anaporudi asubuhi.

Ndoa yetu imefungwa kanisani na tumekuwa tukiishi pamoja kwa miaka miwili tu. Nashauriwa nifanye nini kuhusu maamuzi yangu haya, maana sijisikii furaha kabisa katika ndoa hii. Na mimi ni mchanga sana kuishi kama hivi hadi kifo kitutenganishe.
Jambo baya sikuzote ni kuachana,, vumilia muombee sala kaniSa,Yesu ndio jibu la yote Muombee Mumeo fanya ibada usiwaze kuachana kabisa.
 
Pole sana shoo. Tabia ya ulevi inakera sana hasa hasa Kwa wanaume. Ukiwaambia wanakua wakali kama pilipili. Mimi wangu ni mlevi pro max!

Hebu fikiria inajiogelesha ili mfurahie chakula Cha usiku halafu jitu linarudi saa Saba. Ananuka pombe na mzigo anataka! Keroo kerooo! Basi tu tunavumilia ili watoto wasitange tange.
Tulia hpo hpo wewee ulikula kiapo mtavumiliana kwa hali na Mali, ila yatakwisha tu sweetie ondoa Shaka trust me ooh
 
Wewe ndo mwanamke mzuri!! Maisha ni kuvumiliana!! Hata wewe unajua kabisa kuwa kuna mapungufu yako mengi tu na kama mumeo angeyajua naye angelazimika kukuvumilia!! Nakupongeza sana. Ukisikia wife material ni kama wewe hapo!! Hawa wanaodai eti kwani ndoa ni adhabu ukute walishaachika na wengine ni single mothers, wangetamani kuwa na ndoa lakini imeshindikana!!
 
Sijaona sababu ya msingi cha muhimu acha kumkoromea mumeo ndo hataki kurudi nyumbani
 
Tulia hpo hpo wewee ulikula kiapo mtavumiliana kwa hali na Mali, ila yatakwisha tu sweetie ondoa Shaka trust me ooh
Duh Yani mtu aolewe Ili ateseke na tabia za mtu mzima mwenzie ndoa ni masikilizano kma mwenzio hapendi tabia flani ni mbaya Kuna ulazima kuiendealeza?
 
Natamani kuvunja ndoa yangu.

Habari zenu wakuu, natumai mko poa. Nimekuja na nia ya dhati kutafuta ushauri kuhusu jambo langu ambalo linanitatiza.

Mimi ni msichana mwenye umri chini ya miaka 30. Nina mtoto mmoja wa kiume. Nimekuwa katika ndoa na mume wangu kwa takriban miaka miwili sasa.

Sababu za maamuzi yangu ni kama ifuatavyo:

1. Uchepukaji uliokithiri: Huyu mume wangu amekuwa akinihadaa sana. Sijawahi kuona kitu kilichoniumiza zaidi ya kugundua kuwa anatoka na wanawake wengine. Ameomba msamaha kila mara ninapomfumania, lakini bado anarudia tabia hiyo. Kesi zetu zimekuwa nyingi kwa wazazi na nadhani wamechoka kutusuluhisha.

2. Ulevi uliopitiliza: Mume wangu ni mlevi sana. Kurudi nyumbani asubuhi ni jambo la kawaida kwake. Nimeshazungumza naye na kumweleza jinsi ninavyojisikia kuhusu tabia yake ya kunywa kupindukia, ingawa anahudumia familia vizuri. Lakini, hupati muda na familia kabisa. Inanidhalilisha sana kwa sababu tunakaa na mdogo wake nyumbani, hivyo najihisi vibaya sana anaporudi asubuhi.

Ndoa yetu imefungwa kanisani na tumekuwa tukiishi pamoja kwa miaka miwili tu. Nashauriwa nifanye nini kuhusu maamuzi yangu haya, maana sijisikii furaha kabisa katika ndoa hii. Na mimi ni mchanga sana kuishi kama hivi hadi kifo kitutenganishe.
Mpe nafasi ondoka kakae kwenu usitafute talaka kwa hasira. Mpe fundisho kwa kukaa mbali nae. Lasivyo utavuna kifo kutokana na maradhi ya umalaya.
 
Wewe Mungu ameshakusamehe mara ngapi? Mara ngapi umemkosea Mungu na kila unapomwomba msamaha yeye husamehe!! Vinginevyo angekubania oxygen yake saa hii ingeshakuwa historia!! Kusamehe ni muhimu!!
Wewe zunguka,sisi ni binadamu sio Mungu, there's limit of what we can do!!!...ingekua amecheat mara moja ningeshauri asamehewe,sio severally...halafu ni mlevi kupindukia which is even more risky sababu akilewa ataokoteza tu huko....Ufe unajiona kisa Mungu anasamehe mara kibao, Hakuna Mungu atakayesimama kwenye ujinga wako...jisaidie nami nitakusaidia...
 
Back
Top Bottom