Baada ya Mbowe kugeuka na kuwa kama kina Shibuda, John Cheyo na Mrema ni upi mustakbali wa siasa za upinzani Tanzania?

Kwa jicho la kawaida kabisa ni wazi kuwa Mbowe au CHADEMA imekurupuka kuchukua maamuzi haya na itawawia vigumu kufanya siasa kama tulivyo zoea mwanzo........

Kwa hali ya kawaida haya sio maridhiano.....hakuna maridhiano kati ya mtesi na mteswaji......bali ni mmoja kukubali yaishe ili mateso yasimame.......

Huu ni ushindi mkubwa Kwa serikali ya CCM lakini ni msiba mkubwa kwa Wana CHADEMA na waTanzania wenye maono na ndoto za kuiona Tanzania iliyo njema.........


CCM imejifia na imejichokea haina tena nguvu ya kufanya siasa kwani haina Cha kuwaambia waTanzania baaday miaka 50 ya utawala wao......wanachokifanya hapa kuwa ziba midomo waTanzania kupitia CHADEMA ambao ndio ilikuwa spika pekee Kwa waTanzania wanyonge..........
 
Katika nchi yoyote ukiona UPINZANI unafanya ROMANCE na Chama Tawala, Jua kuwa hakuna upinzani hapo bali kuna genge la wapiga dili wa kisiasa
Confrontational politics hazijawahi kuisaidia CDM, sana sana zimewaumiza sana, Ccm ina dola ya kuwashughulikia wapinzani ndio maana hata waliishia kupoteza makada wao maarufu kwa kupotezwa au kudhuriwa.

Acha wajaribu tu mbinu nyingine itakayowaweka salama.

If you can't fight them, then join them.
 
MSG kwa Mwenda zake na "GENGE" lake...
 
Ikiwa ACT inakuwa usaliti ila ikiwa chadema ni kuweka maslahi ya nchi mbele.
Muache double standards
 
70% ya watanzania hawajui kiingereza lakini utakuta na wao wapo kwenye mjadala wa kusema MAGUFULI hajui Kingereza.
Wao hawajasoma sana na huyo msomi Mwendazake alipokuwa akiongea , wakimwoma anaongea kiengereza kibovu kuliko wao
 
Basi uwe unatambua kivitendo huko kutofautiana mawazo, unaonyesha hauamini kwamba katika kutofautiana mawazo ndio maana unasema hajitambui mwana cdm mwenye mawazo tofauti na hiki kinachoendelea chadema bila kusikiliza na kupima hoja zake. Ndio maana umekuwa ukiwaita wenye kupinga kuwa ni wafuasi wa jiwe wakati wengine ni chadema.
 
Imethibitisha hakuna Upinzani TZ zaidi ya Njaa za wanaojiita viongozi wa upinzani. Wate wana njaa kali. wameonyeshwa pesa kidogo tuu lugha zimeguka, sio Mbowe wala sio Lisu.
 

Mimi naunga mkono chadema Kwa walichofanya, wametumia akili kubwa, coz uwez kubishana na serikali never

Chadema walikaa bila mikutano, walikaa bila mikutano ya ndani, walikuwa wanakamatwa kila siku, wanafungwa, na nyie mnao piga kelele sasa mlikuwa mnatengeneza watoto Tu nyumbani kwenu

Sasa now wameamua kusikilizana na serikali ili Tu warudi kwenye platforms upya, nyie mnaanza kelele sijui hata mnataka nn

Kudeal na serikali za kiafrika ni ngumu Sana, kushindana na serikali ni ngumu sana, serikali inaweza kufanya Jambo lolote

Mfano ishu ya wakina mdee, si unaona mpaka Leo ni wabunge? Na wote tunajua hawakutakiwa kuwa wabunge?

Hiyo ndio nguvu ya serikali,

Mbowe ameamua kuanza upya, chama kipate Ruzuku yake, Chama kishiriki Uchaguzi, Chama kipate wabunge hapo sasa ndio kitakuwa chama pinzani

Uwez kuwa chama pinzani na upinzani wako unafanya kwenye keyboard tu
 
As for the record wapo walichokifanya ikiwemo kuvimba na kesi hadi mwisho, wapo walio andamana nje ya viunga vya mahakama, at one hawakuruhusiwa kuingia mahakamani. Na mengi tu. Check your record bro
Hayo yote nayajua, ila hayakuwa yakitosha na hata waliyokuwa wakifanya hivyo walikuwa ni wachache sana kuliko wingi wa wanachadema kama hao waliyokuwa wakiandamana mahakamani walikuwa wachache mno.
 

Chama kinaitaji wafuasi, chama kinaitaji kushika dola

Sasa best candidate wenu Dr slaa alikimbia

Ulitaka chadema Kwa wakati ule wa msimamishe salum mwalimu?

Na lowasa alileta wabunge wengi chadema
 
Mkuu Tindo najua inaumiza wakati mwingine kutoelewa viongozi wanasimamia nini...kwa kweli mapokezi ya Lowasa yalituondoa kwenye reli.
 
Hata Mandela wenzake walimshangaa sana na habari za reconciliation lakini ni kwa maslahi mapana ya taifa kwasasa kazi kubwa ni kusafisha ile sumu ya chuki turudi square one kwenye minyukano ya hoja isiyo na chembe ya risasi.
 
Mbowe anafanya kazi nzuri sana,dawa imeanza kuingia vizuri huko😁😁😁
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…