Baada ya maombi nimepata kazi,ashukuriwe Mungu

Habari wakuu,

Kwenye uzi huu nilieleza jinsi ambavyo nilikula msoto kwa miezi sita bila kazi. Kulikuwa na muda nakosa hata shilingi 100—ndiyo, shilingi 100 hii hii. Wakati huo pia nilikuwa naota ndoto nipo shule ya msingi.

Remember hapo nimepoteza kazi ya kuajiriwa ambayo nilikuwa na uwezo wa kupata 1.2M.

Sasa naomba niendelee.

Basi, nimefanya interview si chini ya 15, na nyingine nilibargain mshahara mdogo ukilinganisha na uzoefu wangu, lakini bado sikufanikiwa.

Kuna siku nikaamka ndani hakuna chakula, na usiku wake tulikuwa tumekunywa chai tu.

Nikasema niende beach angalau nikaoge maji ya chumvi niondoe mikosi. 😂

Sasa bwana, nimefika njiani sendo ikakatika upande mmoja. Nikajua nikitembea hadi beach itakatika yote, hivyo nitarudi miguu peku. Nikaamua kugeuka nirudi home.

Njiani nikapita Kanisa Katoliki, nikaona bango linaonyesha kuna kongamano la maombi la Karismatiki. Kwa kuwa nilikuwa nimevaa pensi, nikapanga kesho yake nihudhurie.

KILICHOTOKEA KWENYE MAOMBI

DAY 1: Hakikutokea chochote.

DAY 2: Wakati mtumishi anaomba, nilikuwa nimesimama. Nikaanza kutetemeka mikono, nikahisi labda ni kwa sababu nilikuwa nimeinyanyua muda mrefu wakati wa maombi. Nilivyotoka pale, nikakuta nimetumiwa email ya online interview na kampuni ya nje ya Tanzania lakini inaoperate hapa Tanzania.

DAY 3: Ilikuwa siku ya interview, hivyo nikasema nikimaliza online interview sitaenda kwenye maombi.

Hivyo, one hour before interview nikasema nifanye maombi ya angalau dakika tano. Baada ya kama dakika tatu, nikajikuta natamka, "Kwa jina la Yesu, kwa jina la Yesu," huku nimeinua mikono juu. Ghafla nikaanza kutetemeka mikono tena kwa nguvu.

Nikatetemeshwa mwili wote, na mikono yangu ikawa inatembea yenyewe, inanigusa kuanzia mabegani, kifuani, tumboni hadi kwenye mapaja. Baadaye hali hiyo ikapoa, nikafanya interview ya online.

Siku iliyofuata nikaamka sina hela kabisa. Mke wangu akaomba hela kwa baba mkwe (what a shame). Tukala, kisha nikaenda maombi tena.

DAY 4: Nikaenda maombi, na safari hii sikutetemeka. Kesho yake nikapata email ya second interview (physical).

Kiufupi, hadi naandika hii, nipo kazini. Nimeshasaini mkataba, naendelea na training, na nimepokelewa vizuri sana hapa kazini. Kilichobaki kwangu ni kudeliver impact kwenye kazi.

I'm sorry kama sijaandika vizuri.

N.B.: Mimi nimeshare experience yangu, na andiko hili lisionekane kama napigia chapuo dini fulani.

Hongera sana. Usiache kushare hiyo experience ya maombi na usijali watu watasema nini. Kama mtu hatoamini au atakwazika hiyo siyo shida yako. Mungu amefanya hivyo ili sasa nawe umtukuze kwa kutoa huu ushuhuda ili na wengine wapone pia.
 
utumishi watatusababishia ukichaa qbaaabake watoe tu tangazo pale plecement kila mtu akaripoti anapotaka..
 
We jamaa kwahy maombi yamesaidia? Au muda wako ulikuwa bado kuna siku nilienda kuomba kazi ikulu ya kulisha taus nikapata mshahara milion 5 nikarud nyumban nikajiambia mi wakurisha taus nikaacha kuja kusikia kumbe taus wanakula chips, piza, nyama choma bia nikasema dah nimekosa dili la maana ashukuliwe mungu kwa kukosa kazi mana ningenenepa
 
Hongera sana. Usiache kushare hiyo experience ya maombi na usijali watu watasema nini. Kama mtu hatoamini au atakwazika hiyo siyo shida yako. Mungu amefanya hivyo ili sasa nawe umtukuze kwa kutoa huu ushuhuda ili na wengine wapone pia.
Sahihi kabisa mkuu yaani nimetendewa muujiza katika maisha yangu,
Previously nilikuwa na mashaka na uwepo wa Mungu
Ila naona Mungu kaamua kunionesha ukuu wake.
 
Habari wakuu,

Kwenye uzi huu nilieleza jinsi ambavyo nilikula msoto kwa miezi sita bila kazi. Kulikuwa na muda nakosa hata shilingi 100—ndiyo, shilingi 100 hii hii. Wakati huo pia nilikuwa naota ndoto nipo shule ya msingi.

Remember hapo nimepoteza kazi ya kuajiriwa ambayo nilikuwa na uwezo wa kupata 1.2M.

Sasa naomba niendelee.

Basi, nimefanya interview si chini ya 15, na nyingine nilibargain mshahara mdogo ukilinganisha na uzoefu wangu, lakini bado sikufanikiwa.

Kuna siku nikaamka ndani hakuna chakula, na usiku wake tulikuwa tumekunywa chai tu.

Nikasema niende beach angalau nikaoge maji ya chumvi niondoe mikosi. 😂

Sasa bwana, nimefika njiani sendo ikakatika upande mmoja. Nikajua nikitembea hadi beach itakatika yote, hivyo nitarudi miguu peku. Nikaamua kugeuka nirudi home.

Njiani nikapita Kanisa Katoliki, nikaona bango linaonyesha kuna kongamano la maombi la Karismatiki. Kwa kuwa nilikuwa nimevaa pensi, nikapanga kesho yake nihudhurie.

KILICHOTOKEA KWENYE MAOMBI

DAY 1: Hakikutokea chochote.

DAY 2: Wakati mtumishi anaomba, nilikuwa nimesimama. Nikaanza kutetemeka mikono, nikahisi labda ni kwa sababu nilikuwa nimeinyanyua muda mrefu wakati wa maombi. Nilivyotoka pale, nikakuta nimetumiwa email ya online interview na kampuni ya nje ya Tanzania lakini inaoperate hapa Tanzania.

DAY 3: Ilikuwa siku ya interview, hivyo nikasema nikimaliza online interview sitaenda kwenye maombi.

Hivyo, one hour before interview nikasema nifanye maombi ya angalau dakika tano. Baada ya kama dakika tatu, nikajikuta natamka, "Kwa jina la Yesu, kwa jina la Yesu," huku nimeinua mikono juu. Ghafla nikaanza kutetemeka mikono tena kwa nguvu.

Nikatetemeshwa mwili wote, na mikono yangu ikawa inatembea yenyewe, inanigusa kuanzia mabegani, kifuani, tumboni hadi kwenye mapaja. Baadaye hali hiyo ikapoa, nikafanya interview ya online.

Siku iliyofuata nikaamka sina hela kabisa. Mke wangu akaomba hela kwa baba mkwe (what a shame). Tukala, kisha nikaenda maombi tena.

DAY 4: Nikaenda maombi, na safari hii sikutetemeka. Kesho yake nikapata email ya second interview (physical).

Kiufupi, hadi naandika hii, nipo kazini. Nimeshasaini mkataba, naendelea na training, na nimepokelewa vizuri sana hapa kazini. Kilichobaki kwangu ni kudeliver impact kwenye kazi.

I'm sorry kama sijaandika vizuri.

N.B.: Mimi nimeshare experience yangu, na andiko hili lisionekane kama napigia chapuo dini fulani.
Hongera mkuu your story matches exactly with mine kasoro kuoa na kanisanj ila kila kitu kinafanana…inshort MUNGU ukimuomba kwa dhati anakupa mimi ni shuhuda na sitoacha kuwambia watu hivi…MUNGU mkubwa sana aisee
 
Kindly share your story,story zetu zinaweza kuwasaidia wengine,
Binafsi nitamtegemea Mungu maisha yote yaliyobaki.
 
Yeah upo sahihi mkuu kilele ilikuwa ni Leo,ila hili kongamano sitolisahau maishani mwangu
Kwahiyo kumbe kongamano huwa ni mara moja kwa mwaka?
Yap huwa ni mara moja kwa mwaka

Lakin maombi huendelea kwa kila parokia kulingana na utaratibu wa parokia husika
 
Sio whenever I hear that name..

Haiwezekani mtu ahangaike kutafuta kitu mwenyewe, kwa nguvu na jitihada zake mwenyewe.

Halafu akishapata anasema ni Mungu.

Kumbe ni yeye mwenyewe ndio amehangaika kutafuta na kuhustle.

Huyo Mungu hakuwepo wakati una hustle, Na wala hayupo wakati umepata.

Sasa waafrika wengi, Dini zilishawapumbaza, Wakiteseka wanaambiwa ni Mungu anawajaribu, ili wakipata waone kwamba ni Mungu kajibu.

Kumbe ni ujinga tu, na manipulation tactics za dini kupumbaza watu.
Criticize hizi dini/dhehenu ama imani ila si Mungu,wewe usingewaona wazazi wako wakikulea labda muda huu ungebisha kuwa hatuzaliwi/hatutokani na wazazi.
Kwa namna yeyote ipo asili ya tuvionavyo na sisi pia,hicho chanzo ndio Mungu mwenyewe.
 
Back
Top Bottom