Habari wakuu,
Kwenye uzi huu nilieleza jinsi ambavyo nilikula msoto kwa miezi sita bila kazi. Kulikuwa na muda nakosa hata shilingi 100—ndiyo, shilingi 100 hii hii. Wakati huo pia nilikuwa naota ndoto nipo shule ya msingi.
Remember hapo nimepoteza kazi ya kuajiriwa ambayo nilikuwa na uwezo wa kupata 1.2M.
Ila Kuhusu ndoto ya kuota kijijini kwetu nakumbuka ndoto mbili,
-kuota nimekamatwa na polisi huku nimevaa mavazi ya wafungwa
-Kuota nipo na mama,baba tunatoka kulima kwenye mashamba ya watu.
Binafsi nadoubt kwa sababu mambo yangu yakiwa yanaenda vizuri huwa sioti hivo,huwa naota hivo pale tu...
Sasa naomba niendelee.
Basi, nimefanya interview si chini ya 15, na nyingine nilibargain mshahara mdogo ukilinganisha na uzoefu wangu, lakini bado sikufanikiwa.
Kuna siku nikaamka ndani hakuna chakula, na usiku wake tulikuwa tumekunywa chai tu.
Nikasema niende beach angalau nikaoge maji ya chumvi niondoe mikosi. 😂
Sasa bwana, nimefika njiani sendo ikakatika upande mmoja. Nikajua nikitembea hadi beach itakatika yote, hivyo nitarudi miguu peku. Nikaamua kugeuka nirudi home.
Njiani nikapita Kanisa Katoliki, nikaona bango linaonyesha kuna kongamano la maombi la Karismatiki. Kwa kuwa nilikuwa nimevaa pensi, nikapanga kesho yake nihudhurie.
KILICHOTOKEA KWENYE MAOMBI
DAY 1: Hakikutokea chochote.
DAY 2: Wakati mtumishi anaomba, nilikuwa nimesimama. Nikaanza kutetemeka mikono, nikahisi labda ni kwa sababu nilikuwa nimeinyanyua muda mrefu wakati wa maombi. Nilivyotoka pale, nikakuta nimetumiwa email ya online interview na kampuni ya nje ya Tanzania lakini inaoperate hapa Tanzania.
DAY 3: Ilikuwa siku ya interview, hivyo nikasema nikimaliza online interview sitaenda kwenye maombi.
Hivyo, one hour before interview nikasema nifanye maombi ya angalau dakika tano. Baada ya kama dakika tatu, nikajikuta natamka, "Kwa jina la Yesu, kwa jina la Yesu," huku nimeinua mikono juu. Ghafla nikaanza kutetemeka mikono tena kwa nguvu.
Nikatetemeshwa mwili wote, na mikono yangu ikawa inatembea yenyewe, inanigusa kuanzia mabegani, kifuani, tumboni hadi kwenye mapaja. Baadaye hali hiyo ikapoa, nikafanya interview ya online.
Siku iliyofuata nikaamka sina hela kabisa. Mke wangu akaomba hela kwa baba mkwe (what a shame). Tukala, kisha nikaenda maombi tena.
DAY 4: Nikaenda maombi, na safari hii sikutetemeka. Kesho yake nikapata email ya second interview (physical).
Kiufupi, hadi naandika hii, nipo kazini. Nimeshasaini mkataba, naendelea na training, na nimepokelewa vizuri sana hapa kazini. Kilichobaki kwangu ni kudeliver impact kwenye kazi.
I'm sorry kama sijaandika vizuri.
N.B.: Mimi nimeshare experience yangu, na andiko hili lisionekane kama napigia chapuo dini fulani.

Kuhusu ndoto ya shule ya msingi ni kawaida tu huwa naota tupo darasani n.kKuota upo shule ya msingi pekee haitoshi sababu ulipaswa useme
1. Ulikuwa unafanya nini
2. Ulikuwa na nani?
3. Asubuhi, mchana au jioni
4. Ulikuwa darasani, nje ya darasa
5. Mwanafunzi wa shule hiyo? Ulisomaga hapo?