Baada ya maombi nimepata kazi,ashukuriwe Mungu

Baada ya maombi nimepata kazi,ashukuriwe Mungu

Jina la Bwana libarikiwe, usiache uhusiano wako na Mungu kupitia kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Ukiipata baraka kupitia maombi utahitaji kuitunza kwa maombi na si vinginevyo.

Atakayeshangaa kukosa shng mia atakuwa hajawahi kupitia sehemu ngumu, binafsi naelewa vyema.
 
Baada ya juhudi na jitahada ZAKO nyingi sana kutafuta kazi, Sasa umepata.

Wala sio Mungu.

Huyo Mungu hakuwepo wakati huna kazi na wala hayupo wakati sasa umepata kazi.
 
Umaskini mkubwa na Ukosefu wa ajira barani Afrika unawafanya waafrika waamini getting employed ni Mungu.

Kumbe ni serikali za nchi zao zimewafelisha kwa kiwango cha kuona kupata kazi ni NGUMU mpaka wahangaike kusali na kusali na kuhonga sana

Mambo ambayo kwenye Dunia ya kwanza, Wananchi wanapata bila hata kuomba Mungu na kuhangaika, Kwa waafrika ni safari ndefu ya Kuhongana na Sala zisizo na mwisho.
 
Baada ya juhudi na jitahada ZAKO nyingi sana kutafuta kazi, Sasa umepata.

Wala sio Mungu.

Huyo Mungu hakuwepo wakati huna kazi na wala hayupo wakati sasa umepata kazi.
Whenever u hear that name!😎
 
Umaskini mkubwa na Ukosefu wa ajira barani Afrika unawafanya waafrika waamini getting employed ni Mungu.

Kumbe ni serikali za nchi zao zimewafelisha kwa kiwango cha kuona kupata kazi ni NGUMU mpaka wahangaike kusali na kusali na kuhonga sana

Mambo ambayo kwenye Dunia ya kwanza, Wananchi wanapata bila hata kuomba Mungu na kuhangaika, Kwa waafrika ni safari ndefu ya Kuhongana na Sala zisizo na mwisho.
Ww unamuona Mungu kwenye ajira tu mkuu
 
Habari wakuu,

Kwenye uzi huu nilieleza jinsi ambavyo nilikula msoto kwa miezi sita bila kazi. Kulikuwa na muda nakosa hata shilingi 100—ndiyo, shilingi 100 hii hii. Wakati huo pia nilikuwa naota ndoto nipo shule ya msingi.

Remember hapo nimepoteza kazi ya kuajiriwa ambayo nilikuwa na uwezo wa kupata 1.2M.

Sasa naomba niendelee.

Basi, nimefanya interview si chini ya 15, na nyingine nilibargain mshahara mdogo ukilinganisha na uzoefu wangu, lakini bado sikufanikiwa.

Kuna siku nikaamka ndani hakuna chakula, na usiku wake tulikuwa tumekunywa chai tu.

Nikasema niende beach angalau nikaoge maji ya chumvi niondoe mikosi. 😂

Sasa bwana, nimefika njiani sendo ikakatika upande mmoja. Nikajua nikitembea hadi beach itakatika yote, hivyo nitarudi miguu peku. Nikaamua kugeuka nirudi home.

Njiani nikapita Kanisa Katoliki, nikaona bango linaonyesha kuna kongamano la maombi la Karismatiki. Kwa kuwa nilikuwa nimevaa pensi, nikapanga kesho yake nihudhurie.

KILICHOTOKEA KWENYE MAOMBI

DAY 1: Hakikutokea chochote.

DAY 2: Wakati mtumishi anaomba, nilikuwa nimesimama. Nikaanza kutetemeka mikono, nikahisi labda ni kwa sababu nilikuwa nimeinyanyua muda mrefu wakati wa maombi. Nilivyotoka pale, nikakuta nimetumiwa email ya online interview na kampuni ya nje ya Tanzania lakini inaoperate hapa Tanzania.

DAY 3: Ilikuwa siku ya interview, hivyo nikasema nikimaliza online interview sitaenda kwenye maombi.

Hivyo, one hour before interview nikasema nifanye maombi ya angalau dakika tano. Baada ya kama dakika tatu, nikajikuta natamka, "Kwa jina la Yesu, kwa jina la Yesu," huku nimeinua mikono juu. Ghafla nikaanza kutetemeka mikono tena kwa nguvu.

Nikatetemeshwa mwili wote, na mikono yangu ikawa inatembea yenyewe, inanigusa kuanzia mabegani, kifuani, tumboni hadi kwenye mapaja. Baadaye hali hiyo ikapoa, nikafanya interview ya online.

Siku iliyofuata nikaamka sina hela kabisa. Mke wangu akaomba hela kwa baba mkwe (what a shame). Tukala, kisha nikaenda maombi tena.

DAY 4: Nikaenda maombi, na safari hii sikutetemeka. Kesho yake nikapata email ya second interview (physical).

Kiufupi, hadi naandika hii, nipo kazini. Nimeshasaini mkataba, naendelea na training, na nimepokelewa vizuri sana hapa kazini. Kilichobaki kwangu ni kudeliver impact kwenye kazi.

I'm sorry kama sijaandika vizuri.

N.B.: Mimi nimeshare experience yangu, na andiko hili lisionekane kama napigia chapuo dini fulani.
🙏🙏🙏
 
Whenever u hear that name!😎
Sio whenever I hear that name..

Haiwezekani mtu ahangaike kutafuta kitu mwenyewe, kwa nguvu na jitihada zake mwenyewe.

Halafu akishapata anasema ni Mungu.

Kumbe ni yeye mwenyewe ndio amehangaika kutafuta na kuhustle.

Huyo Mungu hakuwepo wakati una hustle, Na wala hayupo wakati umepata.

Sasa waafrika wengi, Dini zilishawapumbaza, Wakiteseka wanaambiwa ni Mungu anawajaribu, ili wakipata waone kwamba ni Mungu kajibu.

Kumbe ni ujinga tu, na manipulation tactics za dini kupumbaza watu.
 
So pale alikiwa anatetemeka nini?

Au mizimu imemsikia!
 
Back
Top Bottom