Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Haya mazungumzo ya wazee wenye ndevu na mvi za kutosha tunapojadili masuala ya Nchi na utawala tunajua...kabla ya kupeleka kwa wananchi.Wewe kaa kimya tukichoka tunakutuma gazeti
Kweli umejaliwa ujinga
 
Duhh leo Makonda kamzidi JPM? Asee njaa mbaya
 
Kuanzia awamu hii ianze hamna cha maana kinachosaidia wananchi zaidi ya blaa blaa tu.
 
Mara nyingi kukaa kimya kunafaa sana ili kulinda heshima uliyonayo kuliko kuongea mambo yanayokupunguzia heshima yako katika jamii.

Hivi unazungumzia uthubutu wa kufanya nini? Uthubutu wa kufanya mambo hata ya kuwachafua na kuwaharibia wasiohusika? Au, uthubutu wa kufanya maamuzi yanayoonekana dhahiri kuwa na hasara kuliko faida?

Mayala lazima utambue kuwa uthubutu na nguvu ya maamuzi ni moja tu ya sifa za raisi ila siyo sifa pekee. Raisi wetu tutampima kwa vigezo vya kuyosha.
 
Paskali your analysis is shallow! Quite shallow! Unless you are telling the opposite!

Kwny Siasa chochote kinawezekana!

Miaka Mitatu iliyopita ulitegemea Edward Lowassa ndie awe Mgombea Urais wa UKAWA?

Ulitegemea JPM awe Rais?

Ulitegemea Seif Sharif agombane na Lipumba kwa sababu ya Lowassa?

Ulitegemea Yusuph Manji anaweza kunyea Ndoo kwa Maelekezo ya Mwanafunzi wa zamani Muccobs Paulo Makonda?
 
TUNAHITAJI RAISI MWENYE AKILI TIMAMU NA ASIYEKUWA NA PAPARA, I WISH AWE HUSSEIN MWINYI

Hahaha anzisha na wewe uzi shekhe wangu kwa kuweka hoja ambatanishi kama alivyofanya bwana Paskali hapo
 
Wanabodi,
Kabla Magufuli hajawa rais wetu, sisi wengine wenu tulijua tangu mwaka 2014 na tukasema humu!.Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Miongoni mwa sifa zilizomuibua Magufuli ni sifa inayoitwa "uthubutu" unreasonably ambayo wengine huita ni udikiteta. Yaani kuachana na mambo ya kufuata sheria, taratibu na kanuni, ndiyo yametufikisha hapa, hawa viongozi wenye "uthubutu" hawahitaji kujua sheria, taratibu na kanuni, zinataka nini, bali hufanya lile linalowezekana,

Ndio maana tukasema humu, japo Magufuli kweli ni dikiteta, Tanzania mahali ilipofika ilimhitaji mtu kama Magufuli na Mwenyeenzi Mungu akaisikia sala yetu, akatupatia Magufuli!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Tukija kwa Makonda, muda mfupi baada ya kuteuliwa DC wa Kinondoni, akaonyesha uwezo, hivyo kama ilivyokuwa kwa Magufuli, mwaka 2014 tulisema ni Magufuli, na mwaka 2015 kweli akawa yeye. Vivyo hivyo kwa Makonda akiwa DC, akina sisi tukasema hivi Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Na kweli haukupita muda akawa!.

Hivyo kwa hii kazi nzuri yote anayoifanya Magufuli, atakapoondoka ile 2025, kama hatamuachia nchi mtu mwenye kufuata nyayo zake, hii kazi nzuri yote ya Magufuli itakuwa ni kazi bure! . Hivyo nimeshauri Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa vile katiba sio Msahafu, 2025 tuibadili katiba Magufuli aendelee indefinitely kama Mugabe, mpaka atakapo choka kabisa na kuwa hawezi tena kwa incapacitation, au tumsubirie Mungu, au Tanzania sasa na sisi tuanze mtindo wa spotting na headhunting na kumfantia grooming huyo headhunted.

Kwa maoni yangu Makonda atatufaa sana kumpokea Magufuli, maana kiukweli huyu Jamaa atatufaa sana kwa sababu ana uthubutu mkubwa zaidi kuliko hata Magufuli. Makonda akimpokea kiukweli kabisa Tanzania itanyooka.

Magufuli pamoja na mazuri yake, naye kama binadamu pia ana madhaifu na mapungufu yake, Vivyo hivyo Makonda pia sio malaika naye ana mapungufu yake, moja ya mapungufu makubwa ya Makonda ni inferiority complex inayopelekea ku practice superiority complex na kujikuta ana over do bila kujijua.

Mfano ni jinsi anavyojikomba komba kwa rais Magufuli mpaka kupindukia, karibu kila jambo lazima amtaje Magufuli tena kwa majina yake yote manne na sifa zake zote nne "Rais Wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli" (si mnajua watu wa Kanda yetu kwa kupenda masifa). Makonda lazima afike mahali aonyeshe anaweza kusimama on his own na sio kila wakati kutegemea apron strings za Magufuli.

2025 atatufaa sana. Kwa kuanzia 2020 akalichukue lile jimbo la yule mama pale, au akampumzishe Musukuma na kumshikisha adabu. Atashinda na kupewa moja ya portfolio zenye impact, ili 2025 ampokee Magufuli. Kitendo cha Magufuli kushika nchi, ni dalili ya Tanzania kutenda haki ya wengi wape, yaani wenye haki na uhalali wa kutawala nchi ni wale walio wengi. Baada ya Magufuli aje Makonda, na baada ya hapo kule kule mpaka na wengine wawe ni walio wengi! .

Makonda konyesha uwezo wa uthubutu, jee mnalionaje hili la kwanini asiwe Makonda kumpokea Magufuli?.

Kwa kwa wale mashabiki wa upinzani mtanisamehe bure, kwenye urais upinzani ni bado sana.

Paskali.
Wewe huitakii mema nchi hii, kwa uthubutu wako wanzetu wana uthubutu wa kula uchafu kutoka kwenye jalala au kutembea uchi hadharani nao ni uthubutu. Wasukuma ni watu wependa sifa na huenda 2020 ukawa mbishi wao
 
Hapana. Anatakiwa apewe nafasi nyingine kwanza tuone.
 
NI ZAMU YA RAISI MUISLAMU; PUNGUZA MAPENZI PASCO

Nafikiri tuangalie competence na tuachane na hii biashara ya kidini. Imagine kila dini iwe na zamu tutaendelea kweli kama nchi? Haya na wengine nao waanze kuhoji kwanini nafasi zingine kama makamu wa Rais n.k zisiwe na zamu ya kidini hii nchi itakwenda mbele au tutajikuta tumehamisha magoli kutoka "kutafuta maendeleo" kwenda "kutafuta usawa wa kidini."

Natambua haipaswi dini moja au kadhaa kubaguliwa au kupendelewa kwa misingi ya dini zao ila kama tunavyosisitiza kwenye maendeleo tuache uchama then hata lugha na tafsiri za kidini tuziepuke unless kuna ubaguzi wa kudhamiria kabisa.
 
Makonda, hana cha kumfanya awe kiongozi wanchi; kwan hana hata chembe ya sifa ya kiongozi bora.

Anaonekana kama;
1/ mropokaji
2/ muingiliaji wa kazi za mihimi mingine
3/ hakuna busara.
4/ anajificha katika kivuli cha mtu, kinachompa nguvu.
..
Nina mashaka na dini yake, haonekani kama mkristo wala muislamu... nafikiri yupo kwenye dini ileèeeeeeeeeeeeee.........

Manji

"Anatafuta umaarufu kupitia mgongo yangu"

Dr. Josephat Gwajima

"Magufuli huyu mtu hana hekima za kua kiongozi, mpangie kazi nyingine."
 
Wanabodi,
Kabla Magufuli hajawa rais wetu, sisi wengine wenu tulijua tangu mwaka 2014 na tukasema humu!.Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Miongoni mwa sifa zilizomuibua Magufuli ni sifa inayoitwa "uthubutu" unreasonably ambayo wengine huita ni udikiteta. Yaani kuachana na mambo ya kufuata sheria, taratibu na kanuni, ndiyo yametufikisha hapa, hawa viongozi wenye "uthubutu" hawahitaji kujua sheria, taratibu na kanuni, zinataka nini, bali hufanya lile linalowezekana,

Ndio maana tukasema humu, japo Magufuli kweli ni dikiteta, Tanzania mahali ilipofika ilimhitaji mtu kama Magufuli na Mwenyeenzi Mungu akaisikia sala yetu, akatupatia Magufuli!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Tukija kwa Makonda, muda mfupi baada ya kuteuliwa DC wa Kinondoni, akaonyesha uwezo, hivyo kama ilivyokuwa kwa Magufuli, mwaka 2014 tulisema ni Magufuli, na mwaka 2015 kweli akawa yeye. Vivyo hivyo kwa Makonda akiwa DC, akina sisi tukasema hivi Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Na kweli haukupita muda akawa!.

Hivyo kwa hii kazi nzuri yote anayoifanya Magufuli, atakapoondoka ile 2025, kama hatamuachia nchi mtu mwenye kufuata nyayo zake, hii kazi nzuri yote ya Magufuli itakuwa ni kazi bure! . Hivyo nimeshauri Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa vile katiba sio Msahafu, 2025 tuibadili katiba Magufuli aendelee indefinitely kama Mugabe, mpaka atakapo choka kabisa na kuwa hawezi tena kwa incapacitation, au tumsubirie Mungu, au Tanzania sasa na sisi tuanze mtindo wa spotting na headhunting na kumfantia grooming huyo headhunted.

Kwa maoni yangu Makonda atatufaa sana kumpokea Magufuli, maana kiukweli huyu Jamaa atatufaa sana kwa sababu ana uthubutu mkubwa zaidi kuliko hata Magufuli. Makonda akimpokea kiukweli kabisa Tanzania itanyooka.

Magufuli pamoja na mazuri yake, naye kama binadamu pia ana madhaifu na mapungufu yake, Vivyo hivyo Makonda pia sio malaika naye ana mapungufu yake, moja ya mapungufu makubwa ya Makonda ni inferiority complex inayopelekea ku practice superiority complex na kujikuta ana over do bila kujijua.

Mfano ni jinsi anavyojikomba komba kwa rais Magufuli mpaka kupindukia, karibu kila jambo lazima amtaje Magufuli tena kwa majina yake yote manne na sifa zake zote nne "Rais Wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli" (si mnajua watu wa Kanda yetu kwa kupenda masifa). Makonda lazima afike mahali aonyeshe anaweza kusimama on his own na sio kila wakati kutegemea apron strings za Magufuli.

2025 atatufaa sana. Kwa kuanzia 2020 akalichukue lile jimbo la yule mama pale, au akampumzishe Musukuma na kumshikisha adabu. Atashinda na kupewa moja ya portfolio zenye impact, ili 2025 ampokee Magufuli. Kitendo cha Magufuli kushika nchi, ni dalili ya Tanzania kutenda haki ya wengi wape, yaani wenye haki na uhalali wa kutawala nchi ni wale walio wengi. Baada ya Magufuli aje Makonda, na baada ya hapo kule kule mpaka na wengine wawe ni walio wengi! .

Makonda konyesha uwezo wa uthubutu, jee mnalionaje hili la kwanini asiwe Makonda kumpokea Magufuli?.

Kwa kwa wale mashabiki wa upinzani mtanisamehe bure, kwenye urais upinzani ni bado sana.

Paskali.

Paskali
Wenzio wanadai ManhAsset. Thanks umejitambua

Tutakachowafanya 2020 hawatasahau milele count mya words.
 
Itakuwa Tanzagiza na si Tanzania Makonda? hahahaaaa umenifanya nicheke wakati ndani sina Mahindi kwa ajili ya Ugali na nalikuwa mnyonge nawaza
 
Mawazo yako hayawezi kuwa universal ...tutayaheshimu na kukuheshimu kama hayo ni mawazo yako na kwamba wengine tunasimamia vichwa vyetu pia
 
NI ZAMU YA RAISI MUISLAMU; PUNGUZA MAPENZI PASCO
iStock_000011819191Large-760x506.jpg
 
Ila tuache unafiq huyu dogo kazi anafanya tena sana.
Kuna wapuuzi wachache wanaishi kwa kutengeneza fitina ndo wanahangaika na Makonda, waliobaki tunamuelewa sana Makonda kama mwanaume asiyejificha chini ya uvungu. Mwanaume ana sifa ya kupigana na kuonesha determination ama iwe nzuri ama mbaya, ujasiri ni sifa namba moja kwa mwanaume make hata kuua ni lazima uwe jasiri.
 
NI ZAMU YA RAISI MUISLAMU; PUNGUZA MAPENZI PASCO
Ujinga mtupu, kila Mtanzania ana haki ya kuwa kiongozi pale anapofaa kufanya hiyo kazi na hakuna kuangalia dini wala kabila lake. Haya ndio mambo yanayochelewesha maendeleo.
 
Back
Top Bottom