Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Wanabodi,
Kabla Magufuli hajawa rais wetu, sisi wengine wenu tulijua tangu mwaka 2014 na tukasema humu!.Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Miongoni mwa sifa zilizomuibua Magufuli ni sifa inayoitwa "uthubutu" unreasonably ambayo wengine huita ni udikiteta. Yaani kuachana na mambo ya kufuata sheria, taratibu na kanuni, ndiyo yametufikisha hapa, hawa viongozi wenye "uthubutu" hawahitaji kujua sheria, taratibu na kanuni, zinataka nini, bali hufanya lile linalowezekana,

Ndio maana tukasema humu, japo Magufuli kweli ni dikiteta, Tanzania mahali ilipofika ilimhitaji mtu kama Magufuli na Mwenyeenzi Mungu akaisikia sala yetu, akatupatia Magufuli!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Tukija kwa Makonda, muda mfupi baada ya kuteuliwa DC wa Kinondoni, akaonyesha uwezo, hivyo kama ilivyokuwa kwa Magufuli, mwaka 2014 tulisema ni Magufuli, na mwaka 2015 kweli akawa yeye. Vivyo hivyo kwa Makonda akiwa DC, akina sisi tukasema hivi Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Na kweli haukupita muda akawa!.

Hivyo kwa hii kazi nzuri yote anayoifanya Magufuli, atakapoondoka ile 2025, kama hatamuachia nchi mtu mwenye kufuata nyayo zake, hii kazi nzuri yote ya Magufuli itakuwa ni kazi bure! . Hivyo nimeshauri Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa vile katiba sio Msahafu, 2025 tuibadili katiba Magufuli aendelee indefinitely kama Mugabe, mpaka atakapo choka kabisa na kuwa hawezi tena kwa incapacitation, au tumsubirie Mungu, au Tanzania sasa na sisi tuanze mtindo wa spotting na headhunting na kumfantia grooming huyo headhunted.

Kwa maoni yangu Makonda atatufaa sana kumpokea Magufuli, maana kiukweli huyu Jamaa atatufaa sana kwa sababu ana uthubutu mkubwa zaidi kuliko hata Magufuli. Makonda akimpokea kiukweli kabisa Tanzania itanyooka.

Magufuli pamoja na mazuri yake, naye kama binadamu pia ana madhaifu na mapungufu yake, Vivyo hivyo Makonda pia sio malaika naye ana mapungufu yake, moja ya mapungufu makubwa ya Makonda ni inferiority complex inayopelekea ku practice superiority complex na kujikuta ana over do bila kujijua.

Mfano ni jinsi anavyojikomba komba kwa rais Magufuli mpaka kupindukia, karibu kila jambo lazima amtaje Magufuli tena kwa majina yake yote manne na sifa zake zote nne "Rais Wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli" (si mnajua watu wa Kanda yetu kwa kupenda masifa). Makonda lazima afike mahali aonyeshe anaweza kusimama on his own na sio kila wakati kutegemea apron strings za Magufuli.

2025 atatufaa sana. Kwa kuanzia 2020 akalichukue lile jimbo la yule mama pale, au akampumzishe Musukuma na kumshikisha adabu. Atashinda na kupewa moja ya portfolio zenye impact, ili 2025 ampokee Magufuli. Kitendo cha Magufuli kushika nchi, ni dalili ya Tanzania kutenda haki ya wengi wape, yaani wenye haki na uhalali wa kutawala nchi ni wale walio wengi. Baada ya Magufuli aje Makonda, na baada ya hapo kule kule mpaka na wengine wawe ni walio wengi! .

Makonda konyesha uwezo wa uthubutu, jee mnalionaje hili la kwanini asiwe Makonda kumpokea Magufuli?.

Kwa kwa wale mashabiki wa upinzani mtanisamehe bure, kwenye urais upinzani ni bado sana.

Paskali.
Sasa hivi umeamua kuandika articles controversial ili uone tuta react vipi. Paschal na wewe umekuwa mtu wa kutafuta kiki?
 
Na ile kanda huwa haishindwi,
Makonda akipitishwa na chama basi ndio atakuwa rais wetu 2025
 
Mzee Kassanda Tumbo Aliwahi Kusema Ili Umtawale Muafikra Kifikra Kwanza Mnyime Chakula Pia Na Mbinu Zote Zinazoweza Kufanikisha Hilo Basi Atakuwa Mtumwa Wako Milele.

Pili Muonyeshe Kwamba Wewe Ni "Antidote" Ya Matatizo Yake Na Ni Wewe Pekee Unao Uwezo Wa Kuyatatua Baaaaaaaaaaaasi Kwisha Kazi.

Hata Ukimwambia Ning'inia Kwenye Mti Afanya Tu Na Kukuheshimu Na Kukuogopa Zaidi Ya Mungu Wake.

Akiwa Na Maana Ukili-control Tumbo La Mtu Basi Ushamshika Kiakili Na Atakuheshimu Milele Kama Utamnyima Fursa Ya Uhakika Wa Kula

Na Kama Ukiwa Na Madaraka Na Kuyatumia Kwenye Mfumo Huo Utaongoza Milele Kama Utakosa Busara Ya Utawala

Hivyo Sishangai Sana Nikiona Mtu Kama Pascal Mayalla Akiandika Vitu Kama Hivi Kwa Kuwa Sababu Ziko Wazi

Mfano Mzuri Huu Uzi Wa Pascal Tayari Kisaikolojia Anajifanya Kama Vile Anajua CCM Haiwezi Kutoka Madarakani Ndiyo Maana Leo Anathubutu Kuzungumzia Uchaguzi Wa Uraisi Wa Mwaka 2025.

Na Hizi Ndiyo Changamoto Kubwa Vyama Vya Upinzani Wanatakiwa Watambue Kwanza Kwenye Jamii Yetu

Ili Kutawala Wanatakiwa Kwanza Kuweza Kuwekeza Kwenye Miradi, Elimu Na Uchumi Ili Wazee, Wakina Mama Na Vijana Wasiwe Na Akili Tegemezi

Waweze Kuwajengea Misingi Mizuri Ya Kuondokana Na Umaskini Badala Kuwekeza Nguvu Nyingi Kwenye Uwashawishi Wa Maandamano Na Mikutano Pekee

Swali Litakuja Watawezeshaje? Wawakusanye Vijana, Wazee Na Wakina Mama Kwa Makundi

Chama Kiwe Na Miradi Yake Kwenye Kila Tawi Itakayotoa Ajira Na Kuwapa Fursa Wengine Kujifunza Huku Wakieneza Sera Zao Kwa Vitendo Na Nadharia

Chama Pia Ki-support Na Kiwe Na Fungu La Kuwawezesha Hao Wenye Mafunzo Wajiajili Au Waajiliwe Kujikwamua Na Njaa

Watanzania Wanataka Mafanikio Ila Pa Kuyapata Ni Shida Hususani Ukiwa Na Njaa,

Tumeona Mifano Mingi Vijana Wakiwaona Viongozi Kwenye Maeneo Yao Cha Kwanza Kulia Ni Njaa Au Serikali Tusaidie Na Wao Wanafurahi Sababu Waanona Dawa Kweli Inawaingia

Kisaikolojia Vijana Hawajitambui Kuwa Wanaweza Kubadili Maisha Yao Na Kufanya Maamuzi Yao Bila Shuruti La Njaa

Na Hata Kama Wanajitambua Zile Njia Za Kujiwezesha Zimebanwa Ili Njaa Iwazofishe Kifikra Na Kuamini Serikali Ikiamua Kitu Haishindwi Hata Kukufirisi Ikiwezekana Hata Kama Umefanikiwa Kiuchumi

Ndiyo Maana Leo Tunaona Wenye Weredi Na Ushawishi MKubwa Kwenye Jamii Wanapoteza Mwelekeo Ili Wakae Mstari Mmoja Na Nyie Tayari Njaa Imewapoteza

Njaa Inakufanya Usifikiri Kwa Marefu, Njaa Inaweza Kukutia Upofu Usione Mbali, Njaa Inaweza Kukushawishi Ukafanya Mambo Ya Ajabu Sana

Leo Hii Ni Mwaka Na Miezi Kadhaa Pascal Mayalla Ameandika Uzi Huu Kwa Mawili Kwanza Kwa Mafumbo Pili Kama Vile Njaa Imempitia Hivyo Anashindwa Kifikiri

Najiaminisha Kwamba Alichoandika Sicho Alichomaanisha Sababu Pascal Mayalla Anamng'ong'a Tu Raisi Na Makonda

Sababu Sifa Kama Hizi Wale Mabwana Wakubwa Ndizo Wanazopenda Kusikia Na Ikiwezekana Pascal Akafanikisha Anayoyataka

Nami nimeshangaa sana mtu anayejiita mwanahabari mbobezi na msomi leo hata 2020 bado anazungumzia 2025!!! Na yupo na uhakika kwamba aliyepo atafika huko bila kuhesabu sababu zinazoweza mfanya asifike!!

Huyu kijana anatia kinyaa sana!
 
Jambo la kushukuru ji kwamba Watanzania ni wa aina moja tu, waliosoma na wasiosoma hawana tofauti yoyote ile.
Ukitaka kujua hebu fatilia kazi za wakuu wa mikoa halafu utajua watanzania ni wa aina gani. Wanatakiwa kufanya nini kwa wananchi? Nani anaiona kazi ya mkuu wa mkoa wa Simiyu ? hayupo kabisa kwasabau tuna tatizo kubwa moja la kuendeshwa na matukio.
Makonda ni mzuri ila sio kwa kiwango watu wanachotaka kuaminishwa, kipi ambacho amebuni na kimekuwa productive kwa wananchi wa jiji lake? Sio huyu anayehangaishana na machinga bila hata kupata suluhisho? Sio huyu anayehangaika na madada poa, shisha, kofia ngunu za pikipiki, utambuzi wa kila mtu ndani ya nchi, zoezi la kupanda miti na usafi(dar ishakuwa safi kama kigali?)
Hayo yote yangewezekana kiurahisi kama tungeanzia kwenye sheria zetu tulizojiwekea wenyewe.
Tanzania haitahitaji tena nguvu 2025 zaidi ya akili kwani wakati huo kila mtu atakuwa mjuaji, sheria tu tulizojiwekea ndio itakuwa rahisi kwetu na sio mtu mmoja.
 
Wanabodi,
Kabla Magufuli hajawa rais wetu, sisi wengine wenu tulijua tangu mwaka 2014 na tukasema humu!.Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Miongoni mwa sifa zilizomuibua Magufuli ni sifa inayoitwa "uthubutu" unreasonably ambayo wengine huita ni udikiteta. Yaani kuachana na mambo ya kufuata sheria, taratibu na kanuni, ndiyo yametufikisha hapa, hawa viongozi wenye "uthubutu" hawahitaji kujua sheria, taratibu na kanuni, zinataka nini, bali hufanya lile linalowezekana,

Ndio maana tukasema humu, japo Magufuli kweli ni dikiteta, Tanzania mahali ilipofika ilimhitaji mtu kama Magufuli na Mwenyeenzi Mungu akaisikia sala yetu, akatupatia Magufuli!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Tukija kwa Makonda, muda mfupi baada ya kuteuliwa DC wa Kinondoni, akaonyesha uwezo, hivyo kama ilivyokuwa kwa Magufuli, mwaka 2014 tulisema ni Magufuli, na mwaka 2015 kweli akawa yeye. Vivyo hivyo kwa Makonda akiwa DC, akina sisi tukasema hivi Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Na kweli haukupita muda akawa!.

Hivyo kwa hii kazi nzuri yote anayoifanya Magufuli, atakapoondoka ile 2025, kama hatamuachia nchi mtu mwenye kufuata nyayo zake, hii kazi nzuri yote ya Magufuli itakuwa ni kazi bure! . Hivyo nimeshauri Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa vile katiba sio Msahafu, 2025 tuibadili katiba Magufuli aendelee indefinitely kama Mugabe, mpaka atakapo choka kabisa na kuwa hawezi tena kwa incapacitation, au tumsubirie Mungu, au Tanzania sasa na sisi tuanze mtindo wa spotting na headhunting na kumfantia grooming huyo headhunted.

Kwa maoni yangu Makonda atatufaa sana kumpokea Magufuli, maana kiukweli huyu Jamaa atatufaa sana kwa sababu ana uthubutu mkubwa zaidi kuliko hata Magufuli. Makonda akimpokea kiukweli kabisa Tanzania itanyooka.

Magufuli pamoja na mazuri yake, naye kama binadamu pia ana madhaifu na mapungufu yake, Vivyo hivyo Makonda pia sio malaika naye ana mapungufu yake, moja ya mapungufu makubwa ya Makonda ni inferiority complex inayopelekea ku practice superiority complex na kujikuta ana over do bila kujijua.

Mfano ni jinsi anavyojikomba komba kwa rais Magufuli mpaka kupindukia, karibu kila jambo lazima amtaje Magufuli tena kwa majina yake yote manne na sifa zake zote nne "Rais Wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli" (si mnajua watu wa Kanda yetu kwa kupenda masifa). Makonda lazima afike mahali aonyeshe anaweza kusimama on his own na sio kila wakati kutegemea apron strings za Magufuli.

2025 atatufaa sana. Kwa kuanzia 2020 akalichukue lile jimbo la yule mama pale, au akampumzishe Musukuma na kumshikisha adabu. Atashinda na kupewa moja ya portfolio zenye impact, ili 2025 ampokee Magufuli. Kitendo cha Magufuli kushika nchi, ni dalili ya Tanzania kutenda haki ya wengi wape, yaani wenye haki na uhalali wa kutawala nchi ni wale walio wengi. Baada ya Magufuli aje Makonda, na baada ya hapo kule kule mpaka na wengine wawe ni walio wengi! .

Makonda konyesha uwezo wa uthubutu, jee mnalionaje hili la kwanini asiwe Makonda kumpokea Magufuli?.

Kwa kwa wale mashabiki wa upinzani mtanisamehe bure, kwenye urais upinzani ni bado sana.

Paskali.
No way, yani tuongozwe na wagonjwa wa akili kwa miaka 20? NO WAY!
 
Majanga haya,mtu kama makonda hafai kupewa madaraka makubwa
 
Kwa lugha yetu Mayala maana yake njaaaa,, Hivyo hatukushangai
 
Makonda awe rais sipati picha aisee! Labla awe waziri ila rais duh! Raia watapelekeshwa balaa yaana tutapangiwa hadi time ya kulala na wake zetu
 
Nami nimeshangaa sana mtu anayejiita mwanahabari mbobezi na msomi leo hata 2020 bado anazungumzia 2025!!! Na yupo na uhakika kwamba aliyepo atafika huko bila kuhesabu sababu zinazoweza mfanya asifike!!

Huyu kijana anatia kinyaa sana!
Haya mazungumzo ya wazee wenye ndevu na mvi za kutosha tunapojadili masuala ya Nchi na utawala tunajua...kabla ya kupeleka kwa wananchi.Wewe kaa kimya tukichoka tunakutuma gazeti
 
Huyu jamaa kwa kukurupuka ndiye mwenyewe! Sijui anataka kuchukua ushekh yahya!?

Makonda ana kipi special kiasi cha kumuona anafaa?
anza na mwaka wake mmoja wa ukuu wa mkoa ni innovation idea gan iliyowasaidia wananchi zaidi ya siasa za muda mfupi?
 
Uthubutu huu huweza kufika mahali mtoto akamwambia mzazi wake ungechelewa ningekuzaa!
 
Back
Top Bottom