Mnyika apewa Uchifu Mwanza na kupewa jina la Chief Malonja, ataka marekebisho ya Katiba

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,947
95,237
Wana MWANZA wamempokea Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa shangwe na kuweka historia kwenye mkoa huo kwa kuamua kukabidhi hadhi ya Chifu wa Wasukuma.

Hakika huu ni msimamo wa kujivunia sana kwa wana MWANZA na inaonyesha kuwa sasa wameanza kujua mchele ni upi na chuya ni zipi kati ya CCM na CHADEMA.


MNYIKA APEWA UCHIFU WA WASUKUMA
IMG_20191229_162904.jpg
IMG_20191229_162851.jpg

Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amewasili mkoani Mwanza ambapo pamoja na mambo mengine amesimikwa kuwa Chifu wa Wasukuma na kupewa jina la Chifu Malonja lenye maana ya Mrekebishaji.

Sent using Jamii Forums mobile app

=====

Chadema chataka marekebisho ya mpito ndani ya Katiba ya sasa

Sunday December 29 2019


BY Jesse Mikofu, Mwananchi jmikofu@mwananchi.co.tz

IN SUMMARY

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tanzania, John Mnyika amesema ili kuwa na tume huru ya uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020, yafanyike marekebisho ya mpito kwenye katiba iliyopo sasa.

Mwanza. Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tanzania, John Mnyika amesema ili kuwa na Tume huru ya uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020, yafanyike marekebisho ya mpito kwenye katiba iliyopo sasa.

Amesema kwa muda uliobaki kabla ya uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba, 2020 haiwezekani kukamilika kwa mchakato mzima wa katiba mpya, lakini inawezekana kufanyika kwa marekebisho ya muda ili kukidhi matakwa ya Watanzania.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Desemba 29, 2020 katika ofisi za Chadema Kanda ya Victoria, baada ya kusimikwa kuwa chifu na wazee wakisukuma na kupewa jina la kichifu la Malonga likiwa na maana ya kutengeneza mambo yawe mazuri.

Mnyika amewaambia viongozi wa kanda hiyo kuwa hakuna budi vyama vya upinzani kuungana pamoja na kupeleka muswada bungeni kwa ajili ya mchakato huo.

“Yapo madai kwamba katiba mpya ni gharama kubwa, lakini Rais John Magufuli akikubali tupeleka muswada wa dharura bungeni tunaweza kufanya marekebisho ya mpito kwenye katiba tuliyonayo bila kusubiria mchakato mzima wa Katiba mpya,” amesema Mnyika.

Amesema Katiba ya sasa inaweza kuongezwa vipengele vitatu ambavyo ni; kuongeza Tume huru ya uchaguzi, ibara inayotaka matokeo ya uchaguzi wa Rais yapingwe mahakamani .

Pia kunaweza kuongezwa kifungu kinachosema ili mtu atangazwe kuwa mshindi wa urais, lazima awe amezidi asilimia 50 ya kura zote.

Amesema wakati wa uchaguzi mkuu kilikuwapo kipengele cha kupiga kura ya maoni kuhusu aina gani ya katiba inayotakiwa ili wananchi waipigie kura wakati wakichagua wabunge, madiwani na Rais.
 
Wana MWANZA wamempokea katibu mkuu wa cdm kwa shangwe na kuweka historia kwenye mkoa huo kwa kuamua kukabidhi hadhi ya chifu wa wasukuma.

Hakika huu ni msimamo wa kujivunia sana kwa wana MWANZA na inaonyesha kuwa sasa wameanza kujua mchele ni upi na chuya ni zipi kati ya ccm na cdm. View attachment 1306446

Sent using Jamii Forums mobile app
Wasukuma hawana urafiki na wachaga Mnyika aache kujikomba komba kwa wasukuma
 
Wana MWANZA wamempokea katibu mkuu wa cdm kwa shangwe na kuweka historia kwenye mkoa huo kwa kuamua kukabidhi hadhi ya chifu wa wasukuma.

Hakika huu ni msimamo wa kujivunia sana kwa wana MWANZA na inaonyesha kuwa sasa wameanza kujua mchele ni upi na chuya ni zipi kati ya ccm na cdm. View attachment 1306446

Sent using Jamii Forums mobile app
Hongereni chadema, wametoa msukuma, ameingia msukuma.hongereni.
 
Back
Top Bottom