ChescoMatunda
JF-Expert Member
- Jan 7, 2009
- 1,232
- 444
Kutokana na kuitoa application bora kabisa ya kujivunia BBM ya BURE ndani ya android na apple store,blackberry Rim Company yahofiwa ITAFILISIKA kabisa. Sababu kuu ni jinsi gani blackberry watanufaika kibiashara kwa kutoa bure app pendwa na watumiaji blackberry tangu zamani? Pia watu wengi walinunua bb sababu ya bbm ambayo ilipatika bb pekee sasa unaweza kutumia bbm hata kama huna blackberry je hili linasaidia vipi kukua kwa mauzo ya bb? pili inajulikana mwenendo wa kibiashara bb haukuwa mzuri hivyo kutoa bbm bure ni suruhisho? Watetezi wa hili wanaona kuwa bb wanajiuza sura kibiashara kwa kuondoa urasimu kwa baadhi ya apps zao lakini pia watauza matangazo hasa kwakuwa lazima ujisajili kutumia bbm pin, pia huduma Yao ya BIS ndio imara zaidi mpaka sasa ukilinganisha na washindani wenzake, mjadala ni mkubwa hasa baada ya mafanikio katika download zaidi ya watu milioni kumi ndani ya masaa 12 tangu kutolewa bbm ndani ya android ambapo inaonyesha ni app no 1 kupata download kubwa kwa muda mfupi ulaya pia ni no 2 kwa America. Wadau maoni yenu kwa hili. Bb wanawezabadilika wakaanza kucharge bbm!?