Baada ya kumuona Serukamba kwenye uteuzi nimewakumbuka wengi sana. Jiwe alikuwa mtu hatari sana!

Serukamba, Hawa Ghasia, Vicky Kamata, Dr. Kafumu, Adadi Rajabu na Andrew Chenge, hawa wote walikuwa wenyeviti wa kamati za kudumu za bunge 2015-2020 (isipokuwa Vicky yeye alikuwa makamu mwenyekiti)

Uchaguzi wa 2020 majina yao yalikatwa na jiwe pale Lumumba japokuwa waliongoza ktk kura za maoni za chama. Sababu kubwa ni kwenda kinyume na hisia za jiwe wakati wakiziongoza kamati zao.

Mifano
1. Hawa Ghasia alipinga zoezi zima la serikali kuingilia ununuzi wa korosho kule Mtwara

2. Serukamba alipinga kuandikwa kwa somo la historia kwa kiswahili, ili jiwe aandikwe na kusomwa na watoto wetu.

Ghasia na Serukamba hoja yao zilikuwa na maana na ndiyo maana waliyoyapinga yamebatilishwa na rais Samia
Jiwe hakuwa mtu mzuri
 
Iko siku jiwe mwingine atarudi, kama baadhi ya waliokuwa watu wake wameanza kurudishwa bora kujiandaa kujua ipo siku atarudi jiwe mwingine, Makonda mwingine, na Sabaya mwingine.

Naamini kiwanda chao [CCM] kinaendelea kuwazalisha wengi tu, hakuna maana kupoteza muda mwingi kushangilia "kupotea" kwa jiwe.
Jiwe hatarudi asilani.
Tumezika na mabaya yake yote.
 
Back
Top Bottom