Baada ya kumjali na kupigania mafanikio yake, leo nimegeuka kuwa mshamba

Feb 14, 2021
6
33
Nilimkuta akiwa ana stress za maisha baada ya kumaliza masomo yake katika chuo fulani. Nilimshika mkono, nikamfuta machozi kisha nikampenda na nikamfundisha kunipenda, nikaishi nae kwa zaidi ya miez kumi. sikuhitaji kumuona akiwa katika msongo wa mawazo bali nilitafiti nikagundua shauku yake ilikuwa ni kupata kazi au biashara ainue familia yake na ajenge mustakabali wa maisha yake.

Niliamini katika falsafa ya ushirikiano katika kujenga mustakabali wetu kwani kila mara alionyesha kuwa mimi ni chagua sahihi kwa kauli na matendo. Nilipambana kwa hali na Mali kwa kipato changu cha kawaida na hii exposure ndogo mpaka nikafanikiwa akapata kazi kwenye shirika moja la miradi ya afya hapa nchini akaenda kufanya kazi nje ya mkoa niliopo mimi.

Wiki mbili baada tu ya kuajiriwa alibadilika sana alibadilika sana, ninaweza kumpigia simu nakuta yuko busy kuanzia saa tano mpaka saa saba usiku na anaona simu yangu inaingia hapokei na akimaliza kuongea hanitafuti hata nikimuulza hatak kusema anaongea na nani, akaenda mbali zaid ukimtumia sms anakujib kwa mkato na ikafikia hatua hataki kunitafuta na nikimtafuta hapokei simu.

Nimewahi kwenda huko anakofanyia kazi nimekaa siku tatu yaani muda wote hajiamini na hawez kutoka nje akaongozana na mm. Dharau na kiburi ndio umekuwa mtindo wa maisha yake. Naishia kuitwa mshamba kwa kumfatilia eti nijiamini. Kifupi nimejitoa kwa mengi nikijua huyu atakuwa mke wangu halaf amekuja kunibadilikia ghafla, inauma sana na Niko katika wakati mgumu sana ukizingatia niko naandika tasnifu yangu niweze kumaliza shahada yangu ya uzamili lakini nashindwa hata kusimamia biashara zangu zinanishinda.

Nabaki muda wote ndani nimejifungia tu roho inaniuma sana kila nikiwaza mawazo yangu yananipeleka mbali zaidi ya jinsi ambavyo siwez kuelezea, nimepitia changamoto nyingi katika maisha yangu lakin hili naona linanizidi.. ndugu zangu naona kabisa jahazi linazama.

Mwenye ushauri mzuri utakaonisaidia na kunitoa ktk hii hali naomba aje PM au hapa hadharani anishauri. Jf naona ndio second home yangu naamini ndugu zangu wenye busara zaidi mtanisaidia.
 
inauma sana na Niko katika wakati mgumu sana ukizingatia niko naandika tasnifu yangu niweze kumaliza shahada yangu ya uzamili lakini nashindwa hata kusimamia biashara zangu zinanishinda..
Duh amekuchanganya kabisa hapa msomi, jaribu kuandika basi hata kama mwanafunzi wa O level, para na nukta
Huyo bibie achana nae hakutaki hukulazimishwa kumsaidia atakuumiza
 
Kama ni wa kwako atarudi, kama si wa kwako potezea. Na sio ndo ukae umsubiri. Fanya maisha yako jomba. Muache ajifunze na aone hayo anayoyafanya ni ya kawaida sana. Kama yana umuhimu kwake ataendelea nayo. Akiona wewe una umuhimu kwake atarudi.
 
Mkuu ulipaswa umpe hata kaujauzito kwanza ndio umsaidie! Hii ingeweza kujenga bond kati yenu! Otherwise wewe ni mwanaume bana, wapo wengi wenye mapenzi ya dhati! Nyanyuka jikung'ute mavumbi songa mbele utashukuru Mungu baadae!
 
Ushauri wangu

1. Acha kujifungia ndani jichanganye na watu muda mwingi ili muda wa kumfikiria yeye uwe mchache au usiwepo kabisa..
2.Acha kusikiliza nyimbo za mapenzi zenye maudhui ya kutendwa..


3.Umesema umepitia mambo mengi magumu lakini Mimi nakwambia wewe bado hujapitia magumu. ishi ukijua Kuna magumu mengi yanakuja mbele yako Tena zaidi ya hili hiyo itakuandaa kisaikolojia....

MWISHO..Kila watati jiambie Mimi ni MWANAUME hili ni dogo tu na litapita kwa uwezo wa MUNGU
 
Sometimes letting go is the best way to go!!



Kwa kuzingatia sasa Ana mshahara wake , nakushauri kama ifuatavyo

Embu wewe mwenyewe Jiondoe kwake.

Kata Nyuzi ya Mawasiliano iliyokuwepo.
Ndiooo ,usimtafute kwa meseji, kwa simu wala kwann,
Achana na hasra, chuki nakuwaza ulichowekeza, amini nakuambia kadri ambavyo unayawaza haya ndivo unazidi kuumia.

Kuwa Chanya...yaan jipende, kuanzia mavazi, mwonekano, maisha ,kazi ,kua mwenye furaha

HAKIKISHA UNAMUONYESHA KUA UNAFURAHA BILA KUMTAFUTA, ..WATU WABAYA WANAKAWAIDA YA KUTAKA KUONA UBAYA ALOKUFANYIA UNAKUONDOLEA FURAHA. NAHAPA UKIWAJULIA, NIWAO WENYEWE WATAUMIA ( ZINGATIA SANA HILI) .

Hakikisha Sanaaa Hauwi mtu wa mitandaoni sanaaaa , ila kua mtu wa mtandaon kwa 'Nadra yenye Uhakika".. Hapa lengo ni kumrudisha kama bado unamhitaj, nahapohapo lengo nikuendelea na Maisha yako wewe kama wewe.


Kwahiyo,
ACHA KUPOST POSTS ZINAKUONYESHA UNA HUDHUNI ,ACHA KABISAAAA.
kama ni jumbe ,tafuta zile jumbe zinazokuonyesha una furaha mfano"Life is full of surprises "..... Love and happiness ".
Yaaan ukipost leo, unatulia kama siku nne au wiki unapost tena , kama ni picha Weka zinazokuonyesha umecheka ,umetabasamu, uko na jamaa zako wakike au wakiume mkifurahi.

Hakikisha Asijue ratiba za Maisha yako kupitia mtandao..yaan hapa asijue upo wapi siku hizi, unafanya nn, upo na nani n.k


USITUMIE WATU KUMBEMBELEZA.


USIJE KUMBEMBELEZA, AU KUMUOMBA MSAMAHA, KUJARIBU KUHOJI KUNAN, KWANN KABADILIKA N.K ACHAAAAAAAAAAAAAA.


HIZI MBUZI ZISIZOJIELEWA ,HUJA KWENYE MAISHA KUFUNDISHA ..NAHIVO JIONE WEWE NI BORA, WA THAMAN, HB, MWENYE MAISHA. HUWEZ AMIN, ASIPOJIRUDI, ATAKUJA BOOOOONGE LA DEMU KISUUUUUUUU KIKALIIII PISI YENYE KUUMBWA NA KUUMBIKA, ACHANA NAHILO GARI LA MKAA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…