Ujana na kujivunia mafanikio

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,223
56,875
Asalaam wana wa JamiiForums, husikeni na kichwa cha habari.

Sote twafahamu kila mmoja anafanya kila namna ili kufikia hatua ya mafanikio na sio hivyo tu kila mmoja ana namna yake ya kutafsiri mafanikio. Kwenye mada yangu nitaangazia mafanikio ya maisha zaidi maisha ya kawaida katika kuweza kumudu chakula, malazi na mavazi.

Wapo baadhi ya vijana hivi sasa wameweza kutoka katika lindi la kutokuwanacho na sasa kuwanacho. I have no problem with it, ndio msingi wa kile tunachokitaka.

Hivi sasa kumezuka tabia ya baadhi ya vijana kujitapa sana juu ya mafanikio waliyoyapata, still I have no problem with this kind of behavior. Wana magari mazuri, nyumba na wanaweza fanya wawezayo ambayo wengi wao wa kipato cha chini hawawezi kufanya.

Kujitapa juu ya mafanikio yako katika jamii yetu sio tamaduni ambayo inapendelewa na wengi, hii mindset imejengeka na imekuwa hivyo.

Zipo shuhuda kadha wa kadha hata nanyi mnawezakuwa shuhuda huko mitandaoni baadhi ya vijana wadogo tu wakisukuma engine kali na mijengo yakisasa, watu hawa wameshindwa kuwa na stahimili ya mdomo hivyo kwao kujitapa kwavyovyote wawezavyo.

Moja ya nilichogundua juu ya watu hawa ni kwamba ni watu waliotoka katika familia zenye maisha ya kawaida kabisa mpaka kutoboa.

Naweza sema ni ulimbukeni fulani uliojaa kichwani, ila nifahamuvyo ni kuwa kwa watoto waliozaliwa kwenye familia ambazo zimeshatoboa ni ngumu sana kuwa na majigambo kwani kwao tayari hakuna geni.

Sina tatizo na mafanikio ya mtu Sina tatizo na majigambo ya mtu isipokuwa majigambo yawe na hekima pamoja na lugha yenye staha ambayo italeta shauku ya wengine kutaka kufika ulipofika.
Tatizo nililoliona na wale wanao wa attack watu hawa wanaojigamba.

Labda niandike hivi katika hii dunia ni muhimu sana kuwa na akili ya ziada ama akili ya kwenda na kitu kichwani. Binadamu unatakiwa umsome na ujifunze kutoka kwake sio kila hoja anayoileta mbele yako inatakiwa iamshe mshawasha wa hisia zako, kuweza kumudu hisia zako ni fanikio moja kubwa sana, note that!

Binafsi tatizo sio kwa hao wanaojigamba maana huwenda wameteleza kwa ulimbukeni wao wa kufanikiwa kwao na ujana maji ya moto. Tatizo ni wewe unaeng'aka kuhusu wao kujitapa kwao! Muda mwengine sikiliza na usifanye chochote, muongeaji litamshuka tu nakujiona aliboronga akili ikija kumkaa sawa.

Sitaki kuandika sana kwa wenye uelewa wameelewa, tutafuteni pesa zakutosha mpaka tuitwe freemason.😂
 
🚮🚮🚮 Ni Ushamba tu Period! Kuna yule mwingine anaosha tyre na pombe ni ulimbukeni tu. Mtakaosema ni chuki nawasubiri nimekaa hapa. Shwaaaain!
 
.
 

Attachments

  • Screenshot_20230809_130606_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20230809_130606_WhatsApp.jpg
    79.1 KB · Views: 7
Ukichunguza sana ni kwamba hayo mambo hayana athari yeyote kwa vile mtu anajivunia kwa mpango wake.

Dunia ya sasa unaweza kuita ushamba ila kila mtu na mfumo wake wa maisha ,kuna vijana wengi wana stress fikirieni hawa kwanza ,hao wanajivunia maisha ya mtandao na mfanikio naona kama wamechagua furaha.

Kila mtu afanye lake analowez japo mimi sjipendelei hizi mambo kwetu ni ushamba ,ila akifanya mwingine sawa kwe vile kila mtu na misingi yake ya maisha ...Mapema sana kumkosoa mtu binafsi naona wamechagua furaha kama wazazi wao walikuwa maskini kwa nn wasijisifu kwa kupindua meza?

Mafanikio katika dunia ni mazuri zaidi na kufeli kweny mafanikio ni jambo baya sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom