Hivi aliyesema kwenye mafanikio ya mwanaume nyuma yake kuna mwanamke shujaa alikuwa na maana gani?

mr pipa

JF-Expert Member
Jul 26, 2021
2,331
4,857
Mpaka leo sijaelewa maana ya hii kauli, ngoja niwaambie kitu labda mnaweza kunijuza. Nimeingia kwenye ndoa nikiwa na miaka 19 sababu ya kufanya hivi binti kwao maisha yalikuwa magumu wazazi wake walifariki nikasema ngoja niokoe japo mwenyewe sikuwa na mishe. Uzuri mzee pesa alikuwa nayo ile paa nikamtoa kwao walikopanga wazee wake pamoja na wadogo zake nikamleta gheto tukawa tumepanga.

Mwezi ukapita nikampiga mzinga mzee nikajenga ila kwa kutumia mgongo wake mzee yaani hati za kiwanja pamoja na nyumba, mara paa nikawa bize kuwahudumia wao kuliko kujenga malengo yangu nikiwa na maana nikaacha chuo na mambo mengine.

Miaka 7 akapita maisha yakaanza kuniwia vigumu kazi zangu nyingi zilikuwa vibarua kama kulima na kuchimba vyoo, mke wangu alivyoona nayumba vikaanza visilani ooh hakuna unachofanya unashinda tu nyumbani huna lolote na miaka inapita kwanza nyumba yenyewe ya mzee wako sina cha kujivunia kwako, akasahau kwamba nilipambana mpaka wadogo zake wamekua, yeye kapata kazi.

Wakuu inaumiza sana grr grr nakuja maana bosi anapiga.
 
Inaendelea.....basi alivyoongea vile niliumia sana yaani nimeacha mambo yangu ya msingi kwaajili yake alafu leo matokeo yake haya, sio siri niliuzunika sana roho iliniuma hatar ila mwisho nikakaza roho japo inafikia hatua ananidharalisha mbele za watu ya kuwa sina chochote ila majiran wanajua historia ya mimi na huyu mke wangu wakawa wanashangaa, na kunionea huruma unajua kwanini sikutaka chukua maamuzi kwasababu ingewa asili waliopo nyuma yake basi nikapiga moyo konde japo ndoa ilikosa mvuto tunaishi tu kama masela, basi nikapata chance ya kazi kwenye migodi ya dhahabu mwisho nikapata m30 sikumwambia chochote ndio kwanza nikalud hom nikawa nakaa tu sifanyi kazi kwa miez miwili mwisho akatafuta room akaenda kupanga na kusema tutengane nikamruhusu ametoka amekaa wiki nikafungua duka la spea za pikipiki nakuanza maisha upya leo hiyi amerudi ananiambia mimi ndie niliekufanya ufikie hapa sasa wakuu huu usemi wa nyuma ya mwanaume kuna mwanamke uliku una mlengo gan?
 
Akirudi tena na huo utumbo mzabue kofi la maana Akili irudi. Haiwezekani mkuu,ukizembea atangangaza mtaji wa duka la spea kakupa yeye.
 
Mpaka leo sijaelewa maana ya hii kauli, ngoja niwaambie kitu labda mnaweza kunijuza. Nimeingia kwenye ndoa nikiwa na miaka 19 sababu ya kufanya hivi binti kwao maisha yalikuwa magumu wazazi wake walifariki nikasema ngoja niokoe japo mwenyewe sikuwa na mishe. Uzuri mzee pesa alikuwa nayo ile paa nikamtoa kwao walikopanga wazee wake pamoja na wadogo zake nikamleta gheto tukawa tumepanga.

Mwezi ukapita nikampiga mzinga mzee nikajenga ila kwa kutumia mgongo wake mzee yaani hati za kiwanja pamoja na nyumba, mara paa nikawa bize kuwahudumia wao kuliko kujenga malengo yangu nikiwa na maana nikaacha chuo na mambo mengine.

Miaka 7 akapita maisha yakaanza kuniwia vigumu kazi zangu nyingi zilikuwa vibarua kama kulima na kuchimba vyoo, mke wangu alivyoona nayumba vikaanza visilani ooh hakuna unachofanya unashinda tu nyumbani huna lolote na miaka inapita kwanza nyumba yenyewe ya mzee wako sina cha kujivunia kwako, akasahau kwamba nilipambana mpaka wadogo zake wamekua, yeye kapata kazi.

Wakuu inaumiza sana grr grr nakuja maana bosi anapiga.
Kwenye mafanikio ya Me kuna Ke nyuma yake = Mama Mzazi.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nilivyoelewa huu msemo ni kuwa
Kila kwenye maendeleo ya mtu kuna mwanamke au mke ni kuwa unafanya kazi na yeye anakusaidia kwa kila kitu anakuwa na wewe bega kwa bega kwa maendeleo yenu

Atabana matumizi, atahakikisha anakushauri kufanya mambo makubwa zaidi

Kila unapopata hela yeye pia anakushauri kuwekeza kitu au kuweka akiba na unapopinda anakunyoosha

Kuna kina mama wengine unampa hela anaificha kwa ajili ya raining day that's all
 
nimekuelewa pamoja mkuu
 
Back
Top Bottom