copernicucci98
JF-Expert Member
- Jul 28, 2018
- 1,223
- 2,319
1. Jeepeers and creepers!! Kama nakumbuka vzr ni muvi moja ya kibabe sana..Nilimkuta akiwa ana stress za maisha baada ya kumaliza masomo yake katika chuo fulani. Nilimshika mkono, nikamfuta machozi kisha nikampenda na nikamfundisha kunipenda, nikaishi nae kwa zaidi ya miez kumi. sikuhitaji kumuona akiwa katika msongo wa mawazo bali nilitafiti nikagundua shauku yake ilikuwa ni kupata kazi au biashara ainue familia yake na ajenge mustakabali wa maisha yake.
Niliamini katika falsafa ya ushirikiano katika kujenga mustakabali wetu kwani kila mara alionyesha kuwa mimi ni chagua sahihi kwa kauli na matendo. Nilipambana kwa hali na Mali kwa kipato changu cha kawaida na hii exposure ndogo mpaka nikafanikiwa akapata kazi kwenye shirika moja la miradi ya afya hapa nchini akaenda kufanya kazi nje ya mkoa niliopo mimi.
Wiki mbili baada tu ya kuajiriwa alibadilika sana alibadilika sana, ninaweza kumpigia simu nakuta yuko busy kuanzia saa tano mpaka saa saba usiku na anaona simu yangu inaingia hapokei na akimaliza kuongea hanitafuti hata nikimuulza hatak kusema anaongea na nani, akaenda mbali zaid ukimtumia sms anakujib kwa mkato na ikafikia hatua hataki kunitafuta na nikimtafuta hapokei simu.
Nimewahi kwenda huko anakofanyia kazi nimekaa siku tatu yaani muda wote hajiamini na hawez kutoka nje akaongozana na mm. Dharau na kiburi ndio umekuwa mtindo wa maisha yake. Naishia kuitwa mshamba kwa kumfatilia eti nijiamini. Kifupi nimejitoa kwa mengi nikijua huyu atakuwa mke wangu halaf amekuja kunibadilikia ghafla, inauma sana na Niko katika wakati mgumu sana ukizingatia niko naandika tasnifu yangu niweze kumaliza shahada yangu ya uzamili lakini nashindwa hata kusimamia biashara zangu zinanishinda.
Nabaki muda wote ndani nimejifungia tu roho inaniuma sana kila nikiwaza mawazo yangu yananipeleka mbali zaidi ya jinsi ambavyo siwez kuelezea, nimepitia changamoto nyingi katika maisha yangu lakin hili naona linanizidi.. ndugu zangu naona kabisa jahazi linazama.
Mwenye ushauri mzuri utakaonisaidia na kunitoa ktk hii hali naomba aje PM au hapa hadharani anishauri. Jf naona ndio second home yangu naamini ndugu zangu wenye busara zaidi mtanisaidia.
2. Shahada ya uzamili, hii si ni master degree?
Mapenzi yana nguvu hivi??
All in all, kama ulimpeleka kwa miradi ya afya ya HIV, huko kuna vihela hela vya kununua mboga.
Amekutumia kama daraja, maisha ndivyo yanavyohitaji.. Kila mtu anahitaji daraja la kumfikisha sehemu.
Move on bro.