Lazima watanzania tuelewe ukombozi wetu hautatokana na CDM au CCM. Ukombozi wetu utatokana na sisi wenyewe. Polisi wameua mwandishi wa habari ambaye si CDM wala CCM. Waandishi wa habari wako wapi na wana-msimamo gani? Kikao kilikuwa cha CDM na polisi na wala hakukuwa na mwakilishi wa marehemu. At the same point hatujui kikao kilikuwa kinahusu haya mauaji moja kwa maoja au vipi lakini kwa vyovyote vile CDM lazima wachukue hatua ambazo hawataonekana wao kama chama wanahamasisha vurugu. Pamoja na hayo sioni ni kwanini Dr. Slaa alikakaa kikao na hawa majambazi. However, naelewa yeye ana-represent grp yake -CDM na anawajibika kutoa info kutokana na taratibu zao walizojiwekea e.g. kufanya independent uchunguzi etc etc.
Watanzania hata tulioelimika tunashindwa kuona kwamba, haki zetu hakuna anayeweza kuzitetea bila sisi wenyewe kuamka. Ni rahisi sana kuwalalamikia viongozi wa vyama vya siasa kwasababu; ndio tunachopenda watanzania -blame game. Dr. Slaa amekwenda kwenye kikao kama mwakilishi wa CDM; je waandishi wa habari na watanzania wasio na vyama wamechukuliaje huu ukatili na wanamaamuzi gani? Personally, naona tukiingiza siasa kwenye hii issue tunakosea sana. Huyu mwandishi ameuwawa akiwa kazini, yule wa Morogoro naye ameuawa alikuwa muuza magazeti; Ulimboka yamemkosakosa akiwa kazini (whether una-agree kwenye mgomo or not waliomtesa walijichukulia sheria mikononi). Sasa je hii yakujichukulia maamuzi mikononi ndio mtindo wa sasa? Je wananchi tunakubaliana na hii mess? Wanasiasa wanahaki yaku-react wanavyotaka wao lakini mimi na wewe tunamajukumu mazito yakuhakikisha askari hawa hawaui mtu mwingine asiye na hatia. Ivi haki zako wewe na mimi ziko mfukoni wa mwanasiasa au kiongozi fulani? Haya ndio mambo ya Ulimboka na kumlalamikia Hellen Kijo Bisimba kwakutofanya a b and c. Mimi na wewe tuko wapi na tuna msimamo gani? Mpaka itokee close to home labda ndio tutapata akili.