Baada ya kazi...... burudiko

Baada ya kazi...... burudiko



Can we have a tost tomorrow evening 1900 hours East African time if you don't bother..... you may come with Halle Berry wa bongo or alone.

Thanks msuli ake mtu.😉

Kasie.🙂
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sio kajitahidi.... kafanya mambo.

Najua jamaa anataka vitu in return. kfanya mambo mazuri ningekugonga mimi lazima tungesubiri traffic apime. Halafu ningekuwa tayari kwa matengenezo!
Yaeezekana unalipa ndio maana mshikaji katanguliza salamu.
All the best!
 
Hahahahaaaa nimejaribu kupunguza ukali wa maneno ili watoto wasisikie mambo ya kikubwa. Ila weye mkubwa mwenzangu umenielewa basi ujue kuna jambo lilitokea na lilikuwa vizuri tuu na likaisha salama.

Kasie.
Papuchi ulimpa. Mkiambiwa mnajiuza mnabisha ila ulijiuza prepaid. Hongera
 
Hey hey heey. .....

First of all today is my birthday, Happy birthday dear mimi.... Happy Birthday Kasie. ....

Wiki iliyopita nilikuwa Dar sasa kwenye mishe mishe zangu bana za hapa na pale kama ujuavyo pilikapilika za jiji la Dar, foleni bumper to bumper. Baada ya kupita mataa ya Morocco magari yakawa yanaenda speed kidogo na pale kwenye ofisi za halotel ndo likatokea range rover likawa linaingia barabarani kwa speed bila kuangalia.......... alinigonga mbaaaaa upande wa abiria gari imeumia mbaya thank God mie sikuumia. Tulisimama wote nikashuka kwenye gari na dereva wa ile range nae akashuka. Ni mkaka tuu aged about 40+ years.
Gari yake pia imeumia ila si sana alikuwa na ngao. Kabla traffic hajaja akaniambia dada nina safari leo natakiwa niwahi airport hapa nilipo nina driving licence yangu naomba nikuachie nikirudi nikutengenezee gari yako naomba uniamini ntakulipa najua makosa ni yangu.

Nikachukua ile driving licence yake nikawa naitizama sijamjibu chochote, nikaitia kwenye kipochi changu kidogo. Nikamwambia si rahisi kukuamini ila naomba nipige picha gari yako na plate number incase ukiniruka walau nna gari ya kuanza nayo (ushahidi) kama nayo ni ya kuiba basi ntajua hukohuko mbele kwa mbele. Wakati napiga picha ile gari niliacha kipochi kwenye gari. Kisha nikamwambia sawa wakati narudi kwenye gari nikasema kwa nini nikae na leseni ya mtu kama ni tapeli hata leseni anaweza iacha ila kama ni mkweli atanitafuta. Nikarudi kumpa leseni yake kisha nikamwambia ukirudi safari unitafute utengeneze hii gari sitaigusa ukitokome abasi Mungu atanilipia.

Nikamrudishia leseni yake nikasepa nae akasepa alikuwa anaelekea mjini. Kilichotokea sasa............

Leo mchana napigiwa simu na yule mkaka akajitambulisha kisha akaniambia naomba uje maeneo yaleyale tulipopata ajali nataka tuyamalize. Nilipofika ofisi za halotel nikampigia simu maana wakati huu nilikuwa na namba aliyonipigia. Akaniambia vuka barabara maeneo yale kuna yard ya magari nikafika akaniambia samahani kwa usumbufu niliokusababishia siku ile ya ajali. Kwanza akanipa leseni yangu nikashangaa kaipataje akaniambia ile siku wakati unanirudishia leseni yangu ulitoa yako (Kasie ) badala ya yangu( yule mkaka ). Hivyo nimekufahamu wewe ni Kasinde na nikajua leo ni Birthday yako.... refer kwenye leseni wanaweka tarehe mwezi na mwaka wa kuzaliwa. Daah akaniambia nilifikiria kuwa uliniamini ile siku na nilijisikia vibaya kukuharibia siku, tena ukaniruhusu niwahi safari yangu airport ambapo nilikuwa kuna deal naifukuzia na hiyo deal imenilipa barabara.

Namnukuu " kwa moyo mkunjufu Kasinde nimekununulia gari mpya hapa showroom same same kama ile ya kwangu tena hii ni new model yake...... kwasababu alikuwa na leseni yangu alishaifanyia usajili na akapata tin number yangu TRA kwa ku-search kwa jina langu. Na hii gari nimeona nikupe leo nikijua ni siku yako ya kuzaliwa. Happy Birthday Kasinde". Mwisho wa kunukuu.

Nikamwambia sasa ile gari uliyonigonga iko nyumbani sijaifanya chochote. Akasema waweza fanya chochote nayo, nikamwambia naomba dakika 10. Nikasogea pembeni nikampigia simu lawyer wangu nikamwelezea habari yote. Akasema chukua gari ila ile mbovu mwambie aichukue, na yeye ndo ajue aifanyie nini hivyo mtakuwa mmebadilishana. Hapo hakutakuwa na mbaya.

Baada ya kuhakikisha kuwa hakuna ubaya kutoka kwa mwanasheria nikamwambia ok thanks for the birthday gift in terms of repay the accident damage. Kisha nikamwambia ile gari ya zamani uliyonigonga nayo naomba nikukabidhi wewe ndo ujue cha kufanya nayo.

Akasema poa nikamwambia twende home ukaichukue akasema hapo yeye ana gari yake hawezi iacha hivo akampigia fundi wake aje aifate gari kwangu. Nikamkaribisha kwangu kwa chakula cha jioni akasema nashukuru ntakuja.

Hapa nnapoandika fundi alikuja chukua ile gari iliyogongwa nami nilirudi nyumbani na gari mupya new model kwa ile ya kwanza. Nikaingia jikoni mtoto wa kike nikaanza kukorofisha mapishi. Tukala tukaongea meengi na sasa ameshaondoka kurudi kwake (Deo.... his name is Deo).

Ndo hivo besdei imeisha salama. Pole kwa kusoma maelezo marefu, ndivyo nilivyo siwezi kuweka muhtahasari.

Thanks you for the gift Deo.🙂

Kasie's Luck.
heri ya siku ya kuzaliwa.

ila jihadhari na kifuatacho.......box bag!

lots of guys splash cash out after they realise that their days are numbered.
 
Sijui nikueleweshe vipi!
Ah...Karibu anyway.

Asantii ...hehehehee Kasie amekuelewa sana, baasi tuu amejiskia kukuchosha akili. Pole usijali amekutania tuu.

Kasie.
 
im waiting for feedback...............................kwich kwich

Okeee feedback has already board the plane not yet departure.... once depart and when arrive you'll be notified 🙂

Kasie.
 
heri ya siku ya kuzaliwa.

ila jihadhari na kifuatacho.......box bag!

lots of guys splash cash out after they realise that their days are numbered.

Thanks for the alert!!

Kasie.
 
ni kweli jamani,na mimi ndio fundi niliyekwenda kulichukua lile gari lililogongwa na boss deo.sikujua kuwa jana ni bday yako.happy belated birthday by the way.
 
Kasie ..unapatikana wapi na mie nikugonge nikupe new ride ...ila jamaa kafaidi kuliko wewe ..kala kashiba .maongezi ...mengineyo na gari kachukua ..ulichopata wewe ni new number plate
 
Kasie ..unapatikana wapi na mie nikugonge nikupe new ride ...ila jamaa kafaidi kuliko wewe ..kala kashiba .maongezi ...mengineyo na gari kachukua ..ulichopata wewe ni new number plate

Hahahaa aliyetoa cheni feki ya dhahabu, kapokea hela feki.... na aliyepokea hela feki katoa cheni feki ya dharau. .. Ngoma droo by: Profesa J
 
ni kweli jamani,na mimi ndio fundi niliyekwenda kulichukua lile gari lililogongwa na boss deo.sikujua kuwa jana ni bday yako.happy belated birthday by the way.

Hahahahaha... fundi mchundooooo hehehehe ntakusemea kwa bosi wako looh
Thanks for late birthday wishes
 
Endelea kuniacha huko huko lakini nilitaka kujua zaidi

Hehehehee mengine hufunikwa na kikombe wasijue wote na watu wazima wakipita na kuona kikombe kimefunikwa basi huelewa hiyo weka mbali na watoto ila watu wazima washaelewa kilichofunikwa kwa kuona tuu bila kuelezewa.

Sasa weye unataka kubaki ukubwani huku huelewi ya ukubwani. ..... ngoja waje wakubwa wenzangu wakupe tuition kidogo heheh
 
  • Thanks
Reactions: irk
Back
Top Bottom