Baada ya kazi...... burudiko

Baada ya kazi...... burudiko

Kuna maswali kadhaa ambayo ningeomba unipe majibu yake Kasie.

Kwanza hongera kwa kuzaliwa, nitakuletea kichupa cha kunyonyea.
Asante kwa pongezi na zawadi, ntakiweka kabatini kama kumbukumbu ya zawadi yako ya siku ya kuzaliwa.

Umesema Wiki iliyopita ulikuwa Dar, hii inamaanisha wewe siyo mwenyeji wa Dar lakini mpaka unaleta huu uzi bado huko dar kwa nini umetumia haya maneno? "nilikuwa Dar"

Yeah tangu wiki iliyopita nilikuwa Dar, na huwa ninakuwa kila nipatapo off na likizo. Kikazi ninaishi nje ya Dar ma kwakuwa huku ndo nyumbani basi nipatapo mwanya huwa najiskia raha kujidai maeneo ya numbani maana hata kampani ya kwenda kupopo iko Dar, hata crush nyingi nazipata Dar.

Kumbe bado huko Dar?

Ndio bado niko Dar.

Hii inaonyesha kuwa wewe siyo mfuatiliaji mzuri wa vitu vyako, inakuwaje usigundue kuwa huna leseni yako.

Kiuhalisia leseni huwa siitumiagi hata kidogo japo huwa natemea nayo popote niendapo, labda nisimamishwe na askari wa barabarani na aniulize kuiona leseni yangu. Hapo ndo naweza ona kama ninayo au sina kwa kuingalia kwenye kipochi ninachoweka.
Ingekuwa kadi ya benki ningegundua siku ile ile maana matumizi yangu mengi nafanyaga kwa kadi.

Hapa kuna kitu kingine muhimu hukukiandika lakini sisi wa 40+ tunajua.

Mueleweshe na @GeneralGaladudu pia maana haelewiiii
Mwisho nikupongeze tena kwa siku yako ya kuzaliwa... happy birthday Kasinde.

Asante tena kwa pongezi, natumai umeelewa na maswali yako yamepata majibu.

Kasie.
 
Hehehehee mengine hufunikwa na kikombe wasijue wote na watu wazima wakipita na kuona kikombe kimefunikwa basi huelewa hiyo weka mbali na watoto ila watu wazima washaelewa kilichofunikwa kwa kuona tuu bila kuelezewa.

Sasa weye unataka kubaki ukubwani huku huelewi ya ukubwani. ..... ngoja waje wakubwa wenzangu wakupe tuition kidogo heheh
Kama umefunika kombe mwanaharamu apite basi hata mimi mwakani panapo majaaliwa nitakupa zawadi maalumu ya birthday ili tufunike kombe au unaonaje
 
Fiction!! Mambo ya Tin number na ishu zingine za ownership hazikuhusika hapa kabisa
 
Kama umefunika kombe mwanaharamu apite basi hata mimi mwakani panapo majaaliwa nitakupa zawadi maalumu ya birthday ili tufunike kombe au unaonaje

Hhahahahaaa nmuogopa mkeo asijenitegeshea kwa rafiki yake kama aavokufanyiaga wewe.

Kasie.
 
Asante kwa pongezi na zawadi, ntakiweka kabatini kama kumbukumbu ya zawadi yako ya siku ya kuzaliwa.

Yeah tangu wiki iliyopita nilikuwa Dar, na huwa ninakuwa kila nipatapo off na likizo. Kikazi ninaishi nje ya Dar ma kwakuwa huku ndo nyumbani basi nipatapo mwanya huwa najiskia raha kujidai maeneo ya numbani maana hata kampani ya kwenda kupopo iko Dar, hata crush nyingi nazipata Dar.

Ndio bado niko Dar.

Kiuhalisia leseni huwa siitumiagi hata kidogo japo huwa natemea nayo popote niendapo, labda nisimamishwe na askari wa barabarani na aniulize kuiona leseni yangu. Hapo ndo naweza ona kama ninayo au sina kwa kuingalia kwenye kipochi ninachoweka.
Ingekuwa kadi ya benki ningegundua siku ile ile maana matumizi yangu mengi nafanyaga kwa kadi.

Mueleweshe na @GeneralGaladudu pia maana haelewiiii

Asante tena kwa pongezi, natumai umeelewa na maswali yako yamepata majibu.

Kasie.
Asante kwa majibu yako mujarabu, uko vizuri kwenye kujibu hoja, nimeridhika na majibu.
 
Asante kwa majibu yako mujarabu, uko vizuri kwenye kujibu hoja, nimeridhika na majibu.

Feregudi.... velkam

Your satisfaction is my appreciation.

Kasie.
 
Feregudi.... velkam

Your satisfaction is my appreciation.

Kasie.
"My satisfaction is your appreciation" haya maneno nimeyapenda.
Nilichogundua Galadudu ni dot com hata vile viatu vya chachacha havijui.
 
Hhahahahaaa nmuogopa mkeo asijenitegeshea kwa rafiki yake kama aavokufanyiaga wewe.

Kasie.
Ha ha ha ha ha haaaaaaaaa. .......nilimkalisha kitako nikamuelewesha kwa kirefu ukubwa wa madhara anayoweza kuleta endapo ataendekeza tabia za kujipa kibarua kigumu cha kunichunguza, nikamtaka tu awe na amani na ajue kwamba yeye ni mke wangu na mi ndo mume wake.....alinielewa na kwa sasa ni raha mustarehe wala hana mpango wa kutegesheana kwa rafiki zake.....kwa hiyo usihofu juu ya kuwekewa mtego
 
"My satisfaction is your appreciation" haya maneno nimeyapenda.
Nilichogundua Galadudu ni dot com hata vile viatu vya chachacha havijui.

Karibuu....

Galadudu huyu ni mchokozi tuu nshamstukia.
 
Ha ha ha ha ha haaaaaaaaa. .......nilimkalisha kitako nikamuelewesha kwa kirefu ukubwa wa madhara anayoweza kuleta endapo ataendekeza tabia za kujipa kibarua kigumu cha kunichunguza, nikamtaka tu awe na amani na ajue kwamba yeye ni mke wangu na mi ndo mume wake.....alinielewa na kwa sasa ni raha mustarehe wala hana mpango wa kutegesheana kwa rafiki zake.....kwa hiyo usihofu juu ya kuwekewa mtego

Hahahahaa mie kunguru muoga bana nakimbiza mbawa zangu mbiooo
 
Mbona hapa sielewi elewi, movie si movie, ndoto si ndoto, ni nn hii mbona sielewi, Yaani ww umetoa leseni yako alafu hujashtuka mpaka jamaa alipokuja kukupa
 
Hey hey heey. .....

First of all today is my birthday, Happy birthday dear mimi.... Happy Birthday Kasie. ....

Wiki iliyopita nilikuwa Dar sasa kwenye mishe mishe zangu bana za hapa na pale kama ujuavyo pilikapilika za jiji la Dar, foleni bumper to bumper. Baada ya kupita mataa ya Morocco magari yakawa yanaenda speed kidogo na pale kwenye ofisi za halotel ndo likatokea range rover likawa linaingia barabarani kwa speed bila kuangalia.......... alinigonga mbaaaaa upande wa abiria gari imeumia mbaya thank God mie sikuumia. Tulisimama wote nikashuka kwenye gari na dereva wa ile range nae akashuka. Ni mkaka tuu aged about 40+ years.
Gari yake pia imeumia ila si sana alikuwa na ngao. Kabla traffic hajaja akaniambia dada nina safari leo natakiwa niwahi airport hapa nilipo nina driving licence yangu naomba nikuachie nikirudi nikutengenezee gari yako naomba uniamini ntakulipa najua makosa ni yangu.

Nikachukua ile driving licence yake nikawa naitizama sijamjibu chochote, nikaitia kwenye kipochi changu kidogo. Nikamwambia si rahisi kukuamini ila naomba nipige picha gari yako na plate number incase ukiniruka walau nna gari ya kuanza nayo (ushahidi) kama nayo ni ya kuiba basi ntajua hukohuko mbele kwa mbele. Wakati napiga picha ile gari niliacha kipochi kwenye gari. Kisha nikamwambia sawa wakati narudi kwenye gari nikasema kwa nini nikae na leseni ya mtu kama ni tapeli hata leseni anaweza iacha ila kama ni mkweli atanitafuta. Nikarudi kumpa leseni yake kisha nikamwambia ukirudi safari unitafute utengeneze hii gari sitaigusa ukitokome abasi Mungu atanilipia.

Nikamrudishia leseni yake nikasepa nae akasepa alikuwa anaelekea mjini. Kilichotokea sasa............

Leo mchana napigiwa simu na yule mkaka akajitambulisha kisha akaniambia naomba uje maeneo yaleyale tulipopata ajali nataka tuyamalize. Nilipofika ofisi za halotel nikampigia simu maana wakati huu nilikuwa na namba aliyonipigia. Akaniambia vuka barabara maeneo yale kuna yard ya magari nikafika akaniambia samahani kwa usumbufu niliokusababishia siku ile ya ajali. Kwanza akanipa leseni yangu nikashangaa kaipataje akaniambia ile siku wakati unanirudishia leseni yangu ulitoa yako (Kasie ) badala ya yangu( yule mkaka ). Hivyo nimekufahamu wewe ni Kasinde na nikajua leo ni Birthday yako.... refer kwenye leseni wanaweka tarehe mwezi na mwaka wa kuzaliwa. Daah akaniambia nilifikiria kuwa uliniamini ile siku na nilijisikia vibaya kukuharibia siku, tena ukaniruhusu niwahi safari yangu airport ambapo nilikuwa kuna deal naifukuzia na hiyo deal imenilipa barabara.

Namnukuu " kwa moyo mkunjufu Kasinde nimekununulia gari mpya hapa showroom same same kama ile ya kwangu tena hii ni new model yake...... kwasababu alikuwa na leseni yangu alishaifanyia usajili na akapata tin number yangu TRA kwa ku-search kwa jina langu. Na hii gari nimeona nikupe leo nikijua ni siku yako ya kuzaliwa. Happy Birthday Kasinde". Mwisho wa kunukuu.

Nikamwambia sasa ile gari uliyonigonga iko nyumbani sijaifanya chochote. Akasema waweza fanya chochote nayo, nikamwambia naomba dakika 10. Nikasogea pembeni nikampigia simu lawyer wangu nikamwelezea habari yote. Akasema chukua gari ila ile mbovu mwambie aichukue, na yeye ndo ajue aifanyie nini hivyo mtakuwa mmebadilishana. Hapo hakutakuwa na mbaya.

Baada ya kuhakikisha kuwa hakuna ubaya kutoka kwa mwanasheria nikamwambia ok thanks for the birthday gift in terms of repay the accident damage. Kisha nikamwambia ile gari ya zamani uliyonigonga nayo naomba nikukabidhi wewe ndo ujue cha kufanya nayo.

Akasema poa nikamwambia twende home ukaichukue akasema hapo yeye ana gari yake hawezi iacha hivo akampigia fundi wake aje aifate gari kwangu. Nikamkaribisha kwangu kwa chakula cha jioni akasema nashukuru ntakuja.

Hapa nnapoandika fundi alikuja chukua ile gari iliyogongwa nami nilirudi nyumbani na gari mupya new model kwa ile ya kwanza. Nikaingia jikoni mtoto wa kike nikaanza kukorofisha mapishi. Tukala tukaongea meengi na sasa ameshaondoka kurudi kwake (Deo.... his name is Deo).

Ndo hivo besdei imeisha salama. Pole kwa kusoma maelezo marefu, ndivyo nilivyo siwezi kuweka muhtahasari.

Thanks you for the gift Deo.🙂

Kasie's Luck.
Message nzuri sana nimeipenda
 
Back
Top Bottom